Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 1/8 uku. 31
  • Jeuri Dhidi ya wanawake

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jeuri Dhidi ya wanawake
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Wanawake Je! Wanastahiwa Nyumbani?
    Amkeni!—1992
  • Jeuri Dhidi ya Wanawake—Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2008
  • Maoni ya Mungu Ni Nini Kuhusu Jeuri?
    Amkeni!—2002
  • Jeuri Iathiripo Nyumbani
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 1/8 uku. 31

Jeuri Dhidi ya wanawake

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA NIGERIA

TANGU tumboni mwa uzazi hadi kaburini, wanawake huwa wahasiriwa wa jeuri, kulingana na Human Development Report 1995 ya Umoja wa Mataifa. Uchunguzi kutoka ulimwenguni pote hufunua yafuatayo:

Kabla ya kuzaliwa. Katika nchi fulani uchunguzi hufanywa ili kupambanua ikiwa kijusu ni cha kiume au cha kike. Mara nyingi vijusu vya kike hutolewa.

Utotoni. Katika Barbados, Kanada, Marekani, New Zealand, Norway, na Uholanzi, mwanamke 1 kati ya 3 huripoti kuwa alitendwa vibaya kingono utotoni au wakati wa ubalehe. Katika Asia na kwingineko, watoto milioni moja hivi—hasa wasichana—wanalazimishwa kuingilia ukahaba kila mwaka. Mamilioni ya wasichana ulimwenguni pote hutahiriwa.

Katika utu uzima. Katika Chile, Jamhuri ya Korea, Mexico, na Papua New Guinea, wanawake 2 kati ya 3 walioolewa ni wahasiriwa wa jeuri ya nyumbani. Katika Kanada, Marekani, New Zealand, na Uingereza, mwanamke 1 kati ya 6 amepata kubakwa.

Katika maisha ya baadaye. Zaidi ya nusu ya wanawake waliouawa kimakusudi katika Bangladesh, Brazili, Kenya, Papua New Guinea, na Thailand waliuawa na wenzi wa kingono wa zamani au wa wakati huu. Katika Afrika, Amerika Kusini, visiwa kadhaa vya Pasifiki, na Marekani, jeuri ya kindoa ndicho kisababishi kikuu cha ujiuaji wa wanawake.

Jeuri dhidi ya wanawake ni jambo la kawaida katika kile ambacho Biblia huita “siku za mwisho,” ambazo katika hizo watu wengi watakuwa “wenye kuudhi,” “sugu,” na “wakatili.” (2 Timotheo 3:1-5, New American Bible) Twaweza kuwa na shukrani kwa ahadi ya Yehova Mungu kwamba baada ya hizi “siku za mwisho” zenye taabu, ataleta ulimwengu mpya wenye amani ambao katika huo wakazi wa dunia “watakaa salama salimini, wala hapana mtu atakayewatia hofu.” (Ezekieli 34:28; 2 Petro 3:13) Chini ya Ufalme wa Mungu, Yesu Kristo “atamkomboa mhitaji aliapo, na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu.”—Zaburi 72:12, 14.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki