Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 3/8 kur. 9-10
  • Ulimwengu Usio na Uhalifu Utapatikanaje?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ulimwengu Usio na Uhalifu Utapatikanaje?
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuachana na Magenge ya Uhalifu
  • Achana na Roho ya Ulimwengu
  • Kwa Nini Uhalifu Uliopangwa Unasitawi?
    Amkeni!—1997
  • Jinsi Uhalifu Uliopangwa Unavyokuathiri
    Amkeni!—1997
  • Naacha Uhalifu Uliopangwa—“Nilikuwa Yakuza”
    Amkeni!—1997
  • Wewe Unataka Uhalifu Umalizwe?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 3/8 kur. 9-10

Ulimwengu Usio na Uhalifu Utapatikanaje?

VITA dhidi ya uhalifu uliopangwa imeanzishwa duniani pote. “Maendeleo makubwa yamefanywa dhidi ya Mafia kwa muda mfupi sana,” likatangaza U.S.News & World Report, “sanasana kwa sababu ya sheria moja, ile Sheria dhidi ya Mashirika ya Hila na Ufisadi, ama RICO.” Sheria hiyo huruhusu kushtakiwa kwa mashirika ya uhalifu kwa msingi wa kujulikana kuendesha mambo kwa hila, bali si kwa tendo moja moja tu. Sheria hiyo pamoja na habari zinazopatikana kupitia udukuzi wa simu na kutokana na washiriki wa magenge wanaotoboa siri wakitaka kusamehewa zimechangia sana mafanikio ya vita dhidi ya Mafia katika Marekani.

Katika Italia pia wenye mamlaka wameyakaba sana magenge. Katika maeneo kama vile Sicily, Sardinia, na Calabria, ambako uhalifu uliopangwa ni wenye nguvu, vikosi vya kijeshi vimepelekwa kushika doria kwenye majengo ya umma na maeneo muhimu ili kuzuia mashambulio ya wahalifu. Serikali yaiona harakati hiyo kama vita ya wenyewe kwa wenyewe. Baada ya viongozi sugu wa magenge ya uhalifu kufungwa gerezani na aliyekuwa waziri mkuu kushtakiwa kwa madai ya kuhusika na Mafia, Italia inapata matokeo mazuri.

Katika Japani serikali ilikaba yakuza ilipoanzisha Sheria Dhidi ya Uhalifu Uliopangwa mnamo Machi 1, 1992. Chini ya sheria hii, mara shirika la majambazi ambalo limetajwa kuwa genge la uhalifu uliopangwa, linazuiwa kufanya matendo 11 ya kulazimisha mambo kijeuri, kutia ndani kudai pesa kwa vitisho, kushiriki katika hila za ulinzi, na mwingilio wa kusuluhisha mizozo kwa kulipwa fedha kiasi fulani. Kwa kutekeleza sheria hii, serikali inanuia kukomesha vyanzo vyote vya mapato ya magenge. Sheria hiyo imepiga vibaya magenge ya uhalifu. Vikundi fulani vimevunjika, na kiongozi mmoja wa uhalifu akajiua—yaonekana kwa sababu ya kutekelezwa sana kwa sheria.

Kwa kweli, serikali na mashirika ya kutekeleza sheria yanapigana vikali na uhalifu uliopangwa. Na bado, Mainichi Daily News, likiripoti juu ya kongamano la mahakimu na maofisa wa polisi kutoka ulimwenguni pote lililofanyika katika 1994, lilisema hivi: “Uhalifu uliopangwa unaendelea kuwa wenye nguvu zaidi na kutajirika zaidi katika karibu kila sehemu ya ulimwengu, ukichuma mapato yawezayo kufikia dola trilioni 1 kwa mwaka.” Kwa kusikitisha, jitihada za wanadamu za kuondosha magenge ya uhalifu duniani haziwezi kufaulu sana. Sababu moja ni kwamba katika visa vingi sheria haitekelezwi haraka nayo haina uhakika. Kwa watu wengi, sheria mara nyingi huonekana kana kwamba inapendelea mhalifu, wala si mhasiriwa. Biblia ilisema hivi miaka ipatayo 3,000 iliyopita: “Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya.”—Mhubiri 8:11.

Kuachana na Magenge ya Uhalifu

Kwa kuongezea kuangamiza uhalifu uliopangwa kutoka nje, serikali zimejaribu kusaidia wale ambao wamo katika magenge hayo waachane nayo. Si rahisi kufanya hivyo. Kulingana na msemo mmoja wa kale, “njia ya pekee ya kuacha Mafia ni katika jeneza.” Kwa mhuni kuacha genge la yakuza, anahitajika kulipa pesa nyingi au kidole chake kidogo au sehemu yacho ikatwe. Kwa kuongezea hofu inayotokezwa na kuachana na genge, mtu aliyekuwa jambazi ni lazima akabili uhalisi wa kuishi maisha manyoofu. Mara nyingi maombi yake ya kutaka kazi yatakataliwa. Hata hivyo, katika nchi fulani kuna nambari za simu za polisi za kuwasaidia majambazi wanaojaribu kuachana na ujambazi lakini wanapata ugumu wa kupata kazi nzuri.

Ili kukabili misongo kutoka kwa familia ya genge na ubaguzi wa jamii, mhuni ahitaji kichocheo kingi sana ili aache uhalifu wake. Ni nini kiwezacho kumchochea? Kinaweza kuwa upendo kwa familia yake, tamaa ya kuishi maisha matulivu, au tamaa ya kufanya yaliyo sawa. Hata hivyo, kichocheo chenye nguvu zaidi kinaonyeshwa na masimulizi ya Yasuo Kataoka katika makala ifuatayo.

Yasuo Kataoka ni mfano wa mamia ya watu ambao wamebadili kabisa maisha yao. Sifa za kihayawani ambazo walionyesha zamani zimebadilishwa na utu mpya “ulioumbwa kulingana na mapenzi ya Mungu katika uadilifu wa kweli na uaminifu-mshikamanifu.” (Waefeso 4:24) Sasa, watu ambao walikuwa kama mbwa-mwitu wanakaa kwa amani miongoni mwa watu wapole, wenye mfano wa kondoo, nao hata wanasaidia wengine!—Isaya 11:6.

Achana na Roho ya Ulimwengu

Kama ilivyotajwa katika makala iliyotangulia, si magenge yote ya uhalifu pekee yaliyo chini ya mamlaka ya Shetani Ibilisi, bali ni ulimwengu wote. Watu hata hawatambui jambo hilo, lakini Shetani amepanga ulimwengu ili kutimiza makusudi yake ya uhalifu. Kama tu magenge ya uhalifu yanavyoandaa mali na mfumo bandia wa familia, yeye ndiye bwana-mkubwa mfadhili kwa kuwapa watu mali, anasa, na hisia ya umoja. Ingawa huenda usijue, huenda umenaswa na hila zake. (Waroma 1:28-32) Biblia yatuambia kwamba “urafiki na ulimwengu ni uadui na Mungu.” (Yakobo 4:4) Si salama kuwa rafiki ya ulimwengu huu, ambao uko chini ya uvutano wa kishetani. Muumba wa ulimwengu wote mzima ana majeshi ya malaika chini ya Yesu Kristo wakiwa tayari kumkamata Shetani na mashetani wake ili kuiondolea dunia uvutano wao mwovu.—Ufunuo 11:18; 16:14, 16; 20:1-3.

Basi unaweza kuachanaje na uvutano wa ulimwengu wa Shetani? Si kwa kuishi maisha ya upweke bali ni kwa kuacha mitazamo na njia za kufikiri ambazo zimeenea sana ulimwenguni leo. Ili kufanya hivyo, utalazimika kupigana na mbinu za Shetani za kujaribu kukuogopesha na kukataa matoleo yake ya kunasa watu. (Waefeso 6:11, 12) Hilo litahusisha dhabihu, lakini unaweza kuachana nao kama wengine walivyofanya maadamu umeazimia na ukiwaendea Mashahidi wa Yehova wakupe msaada.

Ni nini kitakachofuata tendo la Mungu la kuondoa uhalifu kwenye dunia yenye mvurugo? “Mzao wa wasio haki ataharibiwa,” yasema Biblia, nayo yaendelea kusema: “Wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele.” (Zaburi 37:28, 29) Kisha, hakutakuwa na sababu za kuhofu wale ambao walikuwa na sifa za kihayawani, kwa kuwa hao watakuwa wamegeuzwa na ‘ujuzi wa BWANA,’ ambao utaijaa dunia.—Isaya 11:9; Ezekieli 34:28.

Leo, kugeuzwa huko tayari kumetukia, kama ionyeshwavyo na masimulizi ya maisha yafuatayo ya aliyekuwa mshiriki wa yakuza katika Japani.

[Picha katika ukurasa wa 10]

Katika ulimwengu mpya wa Mungu, wote watafurahia kazi ya mikono yao

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki