Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 4/22 uku. 3
  • Kuua Katika Jina la Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuua Katika Jina la Mungu
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Waisraeli wa Kale Walipigana Vita—Kwa Nini Sisi Hatupigani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • Maoni ya Mungu Kuhusu Vita Katika Nyakati za Kale
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Je! Tunaishi Katika Siku za Mwisho?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Ni Dini Gani Inayokubaliwa na Mungu?
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 4/22 uku. 3

Kuua Katika Jina la Mungu

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UFARANSA

“Katika Jina la Mungu, Tunaua na Tutaendelea Kuua”

CHINI ya kichwa kilichonukuliwa juu, International Herald Tribune lilitaja hivi: “Karne hii, ambayo watazamiao mazuri wa pindi kwa pindi hupenda kuiona kuwa iliyoerevuka, kama karne yoyote iliyotangulia, imetiwa madoa na mwelekeo wenye kuogofya wa watu kuuana katika jina la Mungu.”

Mwandikaji huyo alitaja vielelezo vya machinjo ya kidini katika karne za mapema. Kisha, akitaja machinjo ambayo yametokea katika karne ya 20, yeye alimalizia hivi: “Tunachoona ni mwendelezo wenye kuogofya wa ukosefu mbaya sana wa ustahimilivu wa mihula iliyopita. Ibada yabaki ikiwa udhuru wa jeuri ya kisiasa na utiishaji wa kieneo.”

Wengine hujaribu kutetea vita vya leo vya kidini kwa kutaja kwamba Mungu alikubali uuaji wa Wakanaani uliofanywa na Waisraeli wa kale. Hata hivyo, huo si ujiteteaji wa wadaio kuwa Wakristo kupigana vita leo. Kwa nini? Kwa sababu Waisraeli waliagizwa moja kwa moja na Mungu watende wakiwa watekelezaji wa hukumu zake adilifu dhidi ya watu wenye kuabudu roho waovu, ambao ibada yao ilitia ndani ukosefu mbaya sana wa adili na kudhabihu watoto.—Kumbukumbu la Torati 7:1-5; 2 Mambo ya Nyakati 28:3.

Uthibitisho wa kwamba vita vya Israeli la kale havikuwa mapambano ya kawaida tu ni asili ya kimuujiza ya ushindi ambao Mungu alilipa taifa hilo. Kwa kielelezo, Waisraeli wa kale wakati mmoja waliagizwa watumie pembe, mitungi, na mienge—kwa hakika vifaa ambavyo havifai kwa vita halisi! Katika pindi nyingine waimbaji waliwekwa mbele ya jeshi la Israeli ambalo lilikuwa likikabili uwezo mkubwa mno wa majeshi yenye kushambulia kutoka mataifa kadhaa.—Waamuzi 7:17-22; 2 Mambo ya Nyakati 20:10-26.

Isitoshe, wakati pindi kwa pindi Waisraeli walijihusisha katika vita ambavyo havikuwa vimeagizwa na Mungu, hawakubarikiwa naye na walishindwa. (Kumbukumbu la Torati 28:15, 25; Waamuzi 2:11-14; 1 Samweli 4:1-3, 10, 11) Kwa hiyo, vita vya Israeli haviwezi kutajwa vikiwa mamlaka ya kutetea vita vinavyopiganwa katika Jumuiya ya Wakristo.

Katika jina la dini, Wahindu wamepigana na Waislamu na Wasikh; Waislamu wa Shia wamepigana na Waislamu wa Sunni; na katika Sri Lanka, Wabuddha na Wahindu wamechinjana.

Kielelezo halisi ni mauaji katika jina la Mungu yaliyotokea Ufaransa katika karne ya 16. Simulizi la vita hivi lina baadhi ya matukio makuu yaliyojaa damu kupita yote ya historia ya Katoliki ya Kiroma na dini za Protestanti katika Ulaya. Acheni tuchunguze vita hivi, tuone tuwezacho kujifunza kutokana navyo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Picha ya U.S. Army

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki