Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 5/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Je, Nicheze Michezo ya Kompyuta au ya Vidio?
    Amkeni!—1996
  • Je, Kuna Hatari kwa Wachezaji?
    Amkeni!—2002
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 5/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Michezo ya Kompyuta Nina umri wa miaka 15, na nataka kuwashukuru sana kwa makala “Vijana Huuliza . . . Je, Nicheze Michezo ya Kompyuta au ya Vidio?” (Agosti 22, 1996) Hiyo ilionyesha kwelikweli ubaya wa michezo hiyo, nayo itasaidia Wakristo wachanganue mazuri na mabaya ya kuicheza.

F. R., Indonesia

Nina umri wa miaka 17, na nilikuwa napenda michezo yenye jeuri ya kompyuta. Nilifikiri kwamba michezo hiyo haikuniathiri, lakini nikawa mraibu kwelikweli wa michezo hiyo—hasa aina yenye jeuri mliyotaja. Sasa nimeharibu diski zangu zote za kompyuta ambazo zinahusika na ujeuri na damu. Tokeo limekuwa nini? Nahisi vizuri zaidi, na nina wakati mwingi zaidi wa kusoma, kujifunza, na kuzungumza juu ya Yehova Mungu.

S. A., Ugiriki

Ubikira Asanteni kwa makala yenu fupi lakini nzuri ajabu yenye kichwa “Ubikira—Kwa Nini?” (Agosti 22, 1996) Katika siku hizi za kisasa watu wafikiriapo ni lazima uwe na sura mbaya ukichagua kuwa bikira, nilitiwa moyo sana kuona watu wachanga warembo wanaotegemeza viwango vya Yehova. Asanteni tena!

R. D., Marekani

Wahindi wa Amerika Nataka kuonyesha uthamini wangu kwa mfululizo “Wahindi wa Amerika—Wakati Wao Ujao Una Nini?” (Septemba 8, 1996) Nilizisoma makala hizo sana na nitazisoma tena. Sehemu ya ufufuo hasa ilinigusa moyo sana.

S. B., Italia

Makala hizo zilinigusa moyo kuliko makala nyinginezo zote. Zilinisaidia kutambua kwamba nilikuwa nawabagua Wahindi na hilo halipatani na kanuni za kimungu. Tangu siku zangu za shule, nilikuwa na maoni kwamba Wahindi walikuwa tu wakatili wabaya. Vitabu vya historia havikutupa kamwe maoni sahihi juu ya ulimwengu unaotuzingira. Makala zenu zilinisaidia kuona hali mbaya ya Wenyeji wa Amerika—kikiwa kielelezo kingine cha ‘mtu kuwa na uwezo juu ya mwenzake kwa kumwumiza.’—Mhubiri 8:9, ZSB.

M. M., Marekani

Nikiwa mzao wa Wenyeji wa Amerika, nilisoma makala zenu kwa msisimko mwingi. Nililia machozi niliposoma juu ya mateseko yaliyovumiliwa na watu ambao walikuwa wamependa sana uumbaji. Jinsi ninavyotamani siku ambayo Mungu atabadilisha ukosefu wote wa haki ambao wanadamu wote wamefanyiwa na sisi sote kuweza kushiriki pamoja dunia hiyo iliyo paradiso.

N. S., Marekani

Pompeii Majuzi nilisoma kwa makini makala yenu “Pompeii—Mahali Palipobaki Vilevile.” (Septemba 8, 1996) Ilikuwa ni kana kwamba nilikuwa huko! Lakini ningependa jambo fulani lieleweshwe wazi. Makala hiyo yasema kwamba mtu yeyote azuruye Pompeii “bado aweza kuona vinu vya kusagia mahindi.” Labda mnisahihishe, lakini je, mahindi si nafaka ambayo ilipatikana katika bara la Amerika pekee ambayo haikujulikana kwa Wazungu hadi siku za Christopher Columbus?

R. D., Marekani

Pole kama tulitokeza utatanishi kwa jambo hilo. Ingekuwa afadhali kama tungesema kwamba vinu vya kusagia “nafaka” vyaweza kuonekana huko. Kwa kupendeza neno la Kiingereza “corn” laweza kumaanisha tu “mbegu za nafaka za nyasi,” kama vile ngano au oti.—Mhariri.

Tangu utotoni nimevutiwa na historia ya kale. Historia ya Pompeii hasa imenivutia siku zote. Niliposoma makala hiyo, nilihisi kana kwamba nilikuwa nasafiri kupitia jiji hilo. Ajabu! Nilijifunza mambo mengi madogo-madogo ambayo sikuyafahamu. Pia nilipenda ulinganifu uliofanywa na wakati wa mwisho katika siku zetu. Asanteni kwa kunisaidia kujua sehemu ambazo siwezi kuzuru.

J. S. A., Brazili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki