Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 6/22 uku. 3
  • Ulaji—Jambo la Kuhangaikiwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ulaji—Jambo la Kuhangaikiwa
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Ikiwa Mimi Nilipunguza Uzito, Yeyote Aweza!
    Amkeni!—1993
  • Kuchagua Mlo Wenye Afya
    Amkeni!—1997
  • Nifanye Nini Ili Nipate Chakula Chenye Lishe?
    Vijana Huuliza
  • Je, kuna faida Kupunguza Uzito?
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 6/22 uku. 3

Ulaji—Jambo la Kuhangaikiwa

“ENENDA zako, ule chakula chako kwa furaha,” yasema Biblia kwenye Mhubiri 9:7. Kwa hakika, kula si jambo la lazima tu bali pia ni moja ya raha kubwa zaidi katika maisha.

Fikiria Thomas mwenye umri wa miaka 34. Yeye hufurahia nyama. Naye huila kila siku—mara nyingi mara kadhaa kwa siku. Kiamshakinywa chake cha kawaida hutia ndani maziwa, mayai kadhaa, mkate au tosti iliyopakwa siagi, na soseji au bekoni. Katika mahali pa vyakula vya kutayarishwa haraka, yeye huagiza cheeseburgers, chipsi, na maziwa baridi yaliyokorogwa sana na kuchanganywa na aiskrimu. Anapokula mkahawani, yeye huchagua steki ya nyama ya ng’ombe kuwa chakula chake kikuu. Mkahawa aupendao sana huandaa steki ya gramu 680 na kiazi kilichookwa na kurundikiwa krimu chenye chachu, jinsi tu apendavyo. Keki ya chokoleti iliyoongezewa juu aiskrimu ya chokoleti ndiyo kitindamlo chake akipendacho zaidi.

Thomas ana kimo cha sentimeta 178 na uzito wa kilo 89; kulingana na miongozo inayohusiana na ulaji ya serikali ya Marekani, yeye ni mzito kupita kiasi kwa kilo 9. “Mimi sina wasiwasi na uzito wangu,” asema Thomas. “Afya yangu ni bora. Sijapata kukosa hata siku moja kazini kwa miaka 12 ambayo imepita. Wakati mwingi, mimi huhisi vizuri na mwenye nishati—isipokuwa, bila shaka, baada ya kula steki ya gramu 680.”

Ingawa hivyo, je, yaweza kuwa kwamba ulaji wa Thomas unamwathiri kwa njia mbaya, pole kwa pole ukimfanya awe hatarini mwa kupatwa na mshiko wa moyo? Katika kitabu chake How We Die, Dakt. Sherwin Nuland asema juu ya ‘namna za kuishi ambazo ni za kujiangamiza’ na hutia ndani yazo ulaji wa ‘nyama nyekundu, vipande vikubwa vya bekoni, na siagi.’

Vyakula fulani huongozaje kwenye maradhi ya moyo kwa wengi? Vina nini ambacho husababisha hatari? Kabla ya kuzungumzia maswali hayo, acheni tuchunguze vizuri hatari za kiafya za kuwa mzito kupita kiasi.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Kwa nini mlo kama huu ni jambo la kuhangaikiwa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki