Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 10/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Masaibu ya Maggy na Baraka Yangu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 10/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kushughulikia Fedha Ninashukuru sana kwa ule mfululizo “Waweza Kushughulikiaje Fedha Zako?” (Desemba 22, 1996) Nilikuwa nikitumia pesa nyingi sana na sikujidhibiti. Ingawa hivyo, baada ya kusoma makala hizo, nilianza kudhibiti matumizi yangu. Sasa macho yangu yatamanipo kitu, najiuliza ikiwa kweli nahitaji kile ninachoona.

J. B., Brazili

Mume wangu hajakuwa na kazi ya kuajiriwa kwa miezi mitano, na tuna watoto watatu wa kutunza. Kwa hiyo nilianza kutumia madokezo fulani yaliyotolewa katika makala hizo. Nilichukua kitabu, nikachora mistari, nikatengeneza bajeti. Kwa njia hii tumeweza kusimamia pesa zetu kwa miezi mitatu iliyopita na bado tuna pesa kidogo zilizobaki kwa ajili ya mambo yasiyotazamiwa. Kupanga bajeti kwafanya kazi kwelikweli!

L. S., Jamhuri ya Cheki

Kukabili Majaribu Nahisi kushurutishwa kueleza kuhusu ile makala “Niliimarishwa Kukabili Majaribu Yaliyokuwa Mbele.” (Desemba 22, 1996) Niliguswa na vile Edward Michalec alivyovumilia baadhi ya hali zilizo ngumu zaidi. Upendo wake kwa Yehova, kwa wanadamu wenzake, na jinsi alivyopenda kweli ulionyeshwa wazi na mwenendo wake wenye uaminifu na uvumilivu wake wenye saburi.

K. B., Marekani

Masaibu ya Maggy Asanteni sana kwa kuchapisha ile makala “Masaibu ya Maggy na Baraka Yangu.” (Desemba 22, 1996) Nilipata ugumu wa kuzuia machozi nilipokuwa nikisoma kuhusu dhabihu alizofanya mama huyu katika siku za mwisho za uhai wake ili binti yake aweze kuzaliwa akiwa mwenye afya. Nilithamini pia elezo la mume wake kwamba uchungu wake uliondoka polepole kadiri alivyozungumza kuhusu kumpoteza mke wake—jambo ambalo huenda tukaelekea kuepuka tuzungumzapo na jamaa za aliyekufa. Natumaini kupata kumjua Maggy katika ufufuo.

L. S. C., Hispania

Makala hiyo yaonyesha jinsi sisi katika kutaniko tuwezavyo kuonyesha hangaiko halisi kwa mmoja na mwenzake. Wakristo wenzi walimpa mume wa Maggy chakula kwa miezi mingi na pia wakampa mavazi ya mtoto wake. Ni somo lililoje kwetu kuliko kupeleka tu kadi au kupiga simu tu!

P. L., Marekani

Nataka kuwashukuru kwa moyo wangu wote kwa ajili ya makala hii. Mke wangu alikufa katika aksidenti ya barabarani majuma matatu baada ya kifo cha Maggy, akiniacha na watoto wanane. Naelewa uchungu aliouhisi Lorne Wilkins na lazima awe auhisi bado. Asanteni kwa kuchapisha mambo yaliyoonwa kama haya kwa ajili yetu. Kwa kweli ni tegemezo na kitia-moyo kwa wote wanaopitia masaibu kama hayo.

B. B., Ufaransa

Rafiki Bora Zaidi Ahama Nataka kutoa shukurani kutoka moyoni kwa ile makala “Vijana Huuliza . . . Kwa Nini Rafiki Yangu Bora Zaidi Alihama?” (Desemba 22, 1996) Ilifika kwa wakati unaofaa. Karibuni, mmoja wa rafiki zangu atahama; yeye na mume wake wanaenda kutumikia katika kutaniko ambalo kuna uhitaji wa wahubiri zaidi. Ijapokuwa nimefurahi sana kwa ajili yake, najua nitamkosa sana. Asanteni kwa shauri lenu bora kabisa.

R. A., Italia

Hamwezi kuwazia jinsi makala hiyo ilivyonigusa wakati mwangalizi wetu wa mzunguko, aliye mwangalizi asafiriye, alipotuacha ili kutumikia eneo jipya. Alikuwa ametunza sana mahitaji yangu ya kiroho na ya kihisia-moyo. Kama vile picha kwenye makala hiyo ilivyoonyesha, kumuaga lilikuwa ono lenye maumivu. Madokezo yenu ni ya wakati ufaao kama nini katika kunisaidia kukabili upweke.

J. D., Nigeria

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki