Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 12/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 12/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Urafiki Nina umri wa miaka 16, na ninataka kuwashukuru kwa makala kuhusu Shangazi Louie, yenye kichwa “Rafiki Yangu Mpendwa.” (Februari 22, 1996) Nilivutiwa na picha na nilisoma makala hiyo mara hiyo. Nilihisi kukataliwa kidogo kwa sababu wengi wa rafiki zangu waligeuka kuwa si marafiki wa kweli. Makala hiyo ilinitia moyo kweli kweli kutafuta urafiki na watu ambao ni wenye umri mkubwa kuliko mimi.

L. N., Italia

Michezo ya Shule Asanteni sana kwa makala “Vijana Huuliza . . . Michezo ya Timu—Je, Yanifaa?” (Februari 22, 1996) Ilionekana kana kwamba iliandikwa hasa kwa ajili yangu. Ilinifanya nitambue kwamba labda mpaka sasa nimekuwa nikiabudu wanamichezo. Makala hiyo pia ilinisaidia kuthamini kwamba “kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo.”—1 Timotheo 4:8.

Y. T., Japani

Fira Nilifikiri kwamba fira walikuwa wanyama-watambazi wabaya sana ambao walipaswa kuangamizwa kabisa. Lakini baada ya kusoma makala “Je, Ungependa Kukutana na Fira?” (Machi 22, 1996), sasa nina mawazo tofauti kuwaelekea. Asanteni kwa kuweka huru watu kama mimi na mawazo yasiyo sahihi kuhusu viumbe hawa wa kufurahisha.

P. E., Nigeria

Ingawa nililelewa katika eneo la mashamba ambalo lilikuwa na nyoka wengi, kwa kweli sikujua mengi kuwahusu. Kusoma kuhusu hadhari ya fira katika kuepuka mapambano kulinisaidia kuelewa zaidi maneno ya Yesu katika Mathayo 10:16 (NW): “Jithibitisheni wenyewe kuwa wenye hadhari kama nyoka.”

J. F. S., Brazili

Uigizaji-Vitu Asanteni kwa mfululizo “Uigizaji-Vitu—Pigo la duniani pote.” (Machi 22, 1996) Mimi hufanya kazi katika shirika fulani la benki na hivi majuzi tulimaliza semina juu ya uzuiaji wa udanganyifu. Habari mliyotoa ilikuwa ya karibuni zaidi. Asanteni kwa makala zenu zote zenye kutegemeka na zenye kuarifu.

B. P., Marekani

Kwa vile mimi hufanya kazi nikiwa keshia katika benki, nilithamini makala hizo. Tofauti na majarida mengine ambayo huchapisha habari za uwongo ili kufanyiza mshtuko, mlichapisha maoni yenye usawaziko sana. Benki ninayofanya kazi hutoa shauri lifuatalo kwa wauzaji katika maduka: ‘Tunza makala ya fedha halali. Ukiwa na mashaka, linganisha fedha yenye kushukiwa (karatasi, chapa na alama zenye kutambulisha) na fedha halisi.’

L. G., Ufaransa

Usawaziko Asanteni kwa makala “Zawadi ya Mungu ya Usawaziko.” (Machi 22, 1996) Miaka mitatu iliyopita nilisumbuliwa na kizunguzungu kwa majuma manane. Kwanza nilifikiri nilikuwa mtu pekee ambaye alipata kuwa na ugonjwa huu, kwani sikuwa nimeusikia kabla ya hapo. Makala yenu ilinifariji, ikionyesha kwamba wengine wamepatwa na tatizo hili na wamelishinda.

D. P., Jamaika

Nzi Asanteni sana kwa makala yenye kupendeza sana “Wale Nzi Wachukizao—Wenye Faida Kuliko Ufikirivyo?” (Machi 22, 1996) Kiangazi kilichopita nilitumia wakati fulani kufanya uchunguzi juu ya nzi, lakini sikupata habari yoyote yenye kuridhisha. Mimi hufikiria wao ni wasumbufu na wasio safi, kama makala hiyo isemavyo. Lakini sasa natambua kwamba wao hufanya jambo lenye manufaa—kama si hivyo Muumba wetu asingewaumba. Mimi huthamini sana makala mchapishazo.

T. G., Italia

Nimemaliza tu kusoma makala kuhusu nzi na nililazimika kuandika. Mara nyingi nimewaambia watu kiutani kwamba ningependa kujua Yehova alifikiria nini alipoumba kiumbe hiki chenye kusumbua. Sasa ninaelewa kwamba nzi hakuwekwa duniani ili kutusumbua tu!

P. P., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki