Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 12/8 uku. 31
  • Tandala Huyu Alikumbuka

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tandala Huyu Alikumbuka
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Tandala Afanya Simba Waaibike
    Amkeni!—1993
  • Mjue Tandala Mwenye Kuepa
    Amkeni!—1991
  • Hawaogopi Mwisho Tena
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Ukimwi—Wazidi Kuenea
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 12/8 uku. 31

Tandala Huyu Alikumbuka

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA AFRIKA KUSINI

TANDALA mwenye kupendeza wa kiume, mwenye pembe zenye kupendeza zilizojiviringa na masikio ya kipekee, ana kimo cha karibu sentimeta 150 mabegani akiwa amekomaa. Jike, ingawa kwa kawaida hana pembe, pia hutofautishwa kwa masikio yake makubwa. Tandala ni mnyama mwenye haya, sikuzote akiwa chonjo na tayari kukimbilia maficho. Hivyo, kilichompata Karen katika Zimbabwe ni chenye kutokeza.

Kama ilivyoripotiwa katika gazeti African Wildlife, ndama mdogo wa kike wa tandala, ambaye alipatwa amenaswa katika ua wa waya, aliokolewa na kupewa Karen, ambaye alimnywesha kwa chupa kwa majuma machache. Alinawiri na kubaki karibu na shamba hilo la ng’ombe wa maziwa ambamo Karen na familia yake waliishi, mara nyingi akicheza na watoto na mbwa. Hata hivyo, pole kwa pole alielekea porini hadi, alipokomaa, hakuonekana tena karibu na shamba hilo.

Miaka miwili baadaye, alipokuwa akiendesha gari kwenye barabara ya shamba, Karen alishangaa kwamba tandala jike mja-mzito hakutoroka gari lake lilipokaribia. Wala hakukimbia alipoanza kutembea kumwelekea. Kufikia wakati huu alijua kwamba lazima huyu alikuwa mnyama yuleyule aliyemnywesha kwa chupa, kwa hiyo alizungumza kwa wanana alipokuwa akimkaribia kimya-kimya. Tandala huyo alikuwa amemtambua pia, kwa kuwa aliteremsha kichwa chake chini na kumgusa-gusa Karen kwa pua yake akimruhusu amkumbatie!

Miezi kadhaa baadaye, tandala huyo alikuwa barabarani tena—wakati huu akiwa na ndama mdogo sana. Karen alihisi kwamba ndama huyo alikuwa akijulishwa kwake na mama yake, ambaye kwa mara nyingine alijiruhusu akumbatiwe. Jambo lilo hilo lilitukia majuma machache baadaye wakati ilionekana kana kwamba tandala huyo alikuwa akimngoja Karen hasa.

Miezi kadhaa ilipita, na wafanyakazi wa shambani waliripoti kwamba walimwona tandala huyohuyo akiwa na kamba kuzunguka shingo yake. Walikuwa wamejaribu kumkaribia ili kumtoa kamba hiyo, lakini tandala huyo alikimbia. Kwa hiyo Karen akaenda kumtafuta kichakani, akiita alipokuwa akienda. Muda si muda, tandala huyo alijitokeza mbele yake. Karen kwa ufikirio alikuwa ameleta mkate, ambao tandala huyo alikuwa amependa sana, na huku akipewa chakula hicho kitamu, mume wa Karen alikata kamba hiyo yenye kusumbua.

Kifungo cha wazi ambacho kilidumu kwa muda mrefu sana kati ya mwanadamu na mnyama kilileta furaha kubwa kwa familia hii.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki