Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 12/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Ugoro—Je, Hauwezi Kudhuru?
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 12/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kumbukumbu Nashukuru sana kwa makala “Unaweza Kuboresha Kumbukumbu Lako.” (Aprili 8, 1996) Katika wakati uliopita nimejaribu kukumbuka majina ya washiriki wote wa kutaniko letu la Mashahidi wa Yehova—bila mafanikio. Mkazo ulizidi hivi majuzi nilipopewa mgawo na Watch Tower Society wa kutumikia nikiwa mhudumu asafiriye. Makala hiyo ilijibu sala zangu! Kwa kutumia madokezo yaliyotolewa, niliweza kukumbuka majina ya zaidi ya nusu ya wale niliokutana nao katika makutaniko manane tofauti-tofauti.

C. E. U., Nigeria

Walimpata Mungu Asanteni sana kwa makala “Mungu Aliacha Tumpate.” (Machi 22, 1996) Nilipokuwa nikiisoma, macho yangu yalijaa machozi ya shangwe kwa ajili ya Scott na Steve Davis. Mambo waliyojionea yameimarisha azimio langu la kuchukua kazi ya maisha ya huduma ya wakati wote baada ya kumaliza shule.

G. G., Italia

Sijapata kamwe kusoma jambo lililoonwa la ajabu na lenye kuchangamsha kama hili! Ni lazima Yehova alikuwa akitabasamu wakati wanaume hawa wachanga walipojaribu sana kumtumikia. Utumishi wao usio na ubinafsi kwa Mungu wastahili kupongezwa sana.

J. D., Marekani

Simulizi la Scott na Steve la kumtafuta Mungu lilikuwa lenye kuchochea kweli. Hata mimi nilimtafuta Mungu katika makanisa mengi lakini sikuridhika kamwe. Nilitaka sana kumpendeza Mungu lakini sikujua jinsi ya kufanya hivyo. Nashukuru kama nini kwamba Yehova alijua matamanio ya moyo wangu! Kumtumikia Yehova kumeokoa uhai wangu na kuniletea amani.

D. C., Marekani

Ulinzi wa Kimungu? Nilikuwa nimeshuka moyo hivi majuzi kwa sababu nilifikiri Yehova hakuwa akisikiliza sala zangu. Hata hivyo, makala “Maoni ya Biblia: Je, Wakristo wa Kweli Wanaweza Kutazamia Ulinzi wa Kimungu?” (Aprili 8, 1996) imenisaidia kuelewa kwamba Mungu hutenda kulingana na makusudi yake na si kulingana na matakwa yetu sikuzote. Yehova na awabariki mnapoandika makala ambazo hutusaidia kuweka tumaini letu kwake.

C. A. A., Brazili

Magari Yaliyotumiwa Asanteni kwa makala “Jinsi ya Kununua Gari Lililotumiwa.” (Aprili 8, 1996) Hivi majuzi, mume wangu nami tulinunua gari lililotumiwa. Kwanza lilionekana kuwa zuri sana, lakini baada ya majuma mawili tulianza kusikia kelele. Baada ya majuma sita gari hilo likaharibika kabisa. Kama tungalipata habari hii nzuri kabla ya kununua gari hilo, labda hatungalikuwa na gari lililoharibika mbele ya nyumba yetu.

M. C., Marekani

Nikiwa fundisanifu wa magari, ningependa kuongeza jambo moja. Kabla ya kununua gari lililotumiwa, chunguza kama nambari zilizo kwenye gari hilo zaambatana na nambari zilizo kwenye hati za umiliki wa gari. Ikiwa haziambatani au ikiwa zimefutwa, huenda unanunua gari lililoibiwa!

M. V., Jamhuri ya Cheki

Asante kwa dokezo hilo lenye msaada.—Mhariri.

Ugoro Asanteni kwa makala “Vijana Huuliza . . . Ugoro—Je, Hauwezi Kudhuru?” (Aprili 22, 1996) Sikuelewa vizuri kichwa hicho, jambo lililonifanya nisome makala hiyo. Ingawa sijapata kuona tatizo hilo hapa Togo, makala hiyo ilinisaidia kuona aina ya matatizo yanayokumba wengine katika sehemu mbalimbali za ulimwengu.

C. H., Togo

Mimi hupenda kusoma makala zenu zote, lakini hiyo ilipita zote. Kuna vijana hapa ambao hutumia ugoro, lakini makala hiyo ilionya kuhusu hatari zao. Sitautumia kamwe.

P. H. W., Brazili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki