Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 5/22 uku. 11
  • Amaranth—Chakula kutoka kwa waazteki

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Amaranth—Chakula kutoka kwa waazteki
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Waazteki—Pambano Lao Lenye Kuvutia Ili Kuokoka
    Amkeni!—1999
  • Kutoka Mchirizi wa Maziwa Hadi Kijiko cha Maziwa ya Unga
    Amkeni!—1999
  • Waazteki wa Kisasa Wajifunza na Kuwa Wakristo wa Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Kutumikia kwa Moyo Wote Licha ya Majaribu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 5/22 uku. 11

Amaranth—Chakula kutoka kwa waazteki

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA MEXICO

PIPI yenye lishe iitwayo alegría ambayo jina lake la Kihispania hutafsiriwa “shangwe” au “furaha,” kwa kawaida hupatikana katika vibanda vyenye kupendeza vya masoko ya vyakula ya Mexico. Hutengenezwa kutokana na mbegu za amaranth, mti wa kitropiki wenye maua mekundu maangavu. Pipi hii hutengenezwa kwa asali isiyosafishwa na katika pindi fulani hurembwa kwa walnut, kokwa za msonobari, na zabibu kavu. Mbegu za amaranth pia zaweza kusagwa kuwa chakula cha nafaka hasa cha kufungua kinywa au unga, ambao hutumiwa kuokea mikate na keki.

Waazteki walipika chapati ngumu na tamale kutokana na unga wa amaranth. Kwa kuongezea, amaranth ilichangia daraka la maana sana katika sherehe za ibada zao za kidini. Gazeti The News la Mexico City lilisema: “Katika moja ya nyingi za sherehe zao za kidini, Waazteki wangetumbukiza kipande cha mkate uliookwa kwa amaranth ndani ya damu ya mmoja wa watekwa wao na maadui [waliouawa] na kukila.” Desturi nyingine ilihusisha kuchanganya mbegu zilizosagwa za amaranth na mahindi na asali na kuunda mchanganyiko huo kuwa sanamu ndogo au miungu. Baadaye sanamu hizi zililiwa katika sherehe ya kidini iliyofanana na sakramenti ya Komunyo ya Kikatoliki.

Mazoea haya yote yalimkasirisha mshindi Mhispania Hernán Cortés na kumchochea apige marufuku ulimaji na utumizi wa amaranth. Mtu yeyote aliyejaribu kuihalifu amri yake ama aliuawa ama mkono uliovunja sheria ulikatwa. Hivyo, mazao ambayo kwa wakati huo yalikuwa ya maana zaidi katika Mexico yalikuwa karibu kutoweka kabisa.

Hata hivyo, zao la amaranth lilidumu, na kwa njia fulani lilienea kwa njia zisizojulikana kutoka Amerika ya Kati hadi Himalaya. Kwa karne iliyopita, limekuwa chakula kikuu miongoni mwa makabila yaishiyo mlimani ya China, India, Nepal, Pakistan, na Tibet.

Huko nyuma katika Mexico, watafiti wamekuwa wakijaribu kutenga protini za mbegu hiyo ili kutokeza maziwa ya amaranth, kinywaji chenye thamani ya lishe itoshanayo na ya maziwa ya ng’ombe. Mradi wao ni kutumia kinywaji hiki ili kufanya vyakula na vinywaji viwe vyenye nguvu kwa wale wasioweza kununua mayai, maziwa, samaki, au nyama ya ng’ombe, mbuzi, kondoo na kadhalika.

Licha ya historia yenye msukosuko ya amaranth, chakula hiki chenye matumizi mbalimbali, kingali chafurahiwa na watu wengi leo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki