Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 6/8 uku. 28
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ugonjwa wa Kipindupindu Waathiri Vibaya Afrika Mashariki
  • Kuwasaidia Wafu?
  • Vito Vyenye Nururishi
  • Mazoea ya Usomaji
  • Dini ya Kujibunia
  • Ugonjwa Ulioogopwa Zaidi Katika Karne ya 19
    Amkeni!—2010
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1998
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1999
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 6/8 uku. 28

Kuutazama Ulimwengu

Ugonjwa wa Kipindupindu Waathiri Vibaya Afrika Mashariki

“Kuzuka kwa kipindupindu kumefikia viwango vya mlipuko katika Afrika Mashariki,” yasema ripoti moja ya Shirika la Associated Press kutoka Nairobi, Kenya. Kipindupindu, ambao ni ugonjwa wenye kuambukiza usababishao kuharisha, waweza kuua usipotibiwa. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), zaidi ya watu 61,000 katika Afrika Mashariki waliambukizwa maradhi hayo katika mwaka wa 1997, na vifo 2,687 viliripotiwa. Milipuko ya kipindupindu ni ya kawaida katika nchi zisizo na njia zifaazo za kuondoa takataka na ukosefu wa vifaa vya kitiba. Hali huwa mbaya zaidi wakati mvua za msimu zipelekapo kinyesi cha watu kwenye maji ya kunywa. Dakt. Maria Neira, msimamizi wa kikosi maalumu cha WHO kinachoshughulikia kipindupindu, alisema kwamba mpaka mabomba ya maji machafu na maji safi yatakapopatikana katika maeneo yote yaliyoathiriwa, huenda eneo hilo lisiweze kujiondolea kabisa kipindupindu.

Kuwasaidia Wafu?

Katika Hong Kong, kudumisha sura sikuzote hakukomi wakati mtu anapokufa—kwa wengine huendelea katika Maisha ya Baadaye. Hii ni kwa sababu ibada ya wazazi wa kale waliokufa ina fungu kubwa sana katika maisha ya kila siku katika utamaduni wa Wachina. Hivyo, “hata katika ulimwengu wa roho wanafikiri ni jambo la muhimu sana kuonyesha mali,” asema mwenye duka mmoja Kwan Wing-ho. Ili kusaidia jamaa na marafiki waliobaki kuboresha hadhi ya mpendwa wao aliyekufa, Bw. Kwan huuza nakala halisi za risiti za mchanganyiko wa bidhaa, kutia ndani simu za kubebeka, kompyuta, majoko ya microwave, na hata gari aina ya Mercedes Benz kubwa. “Mali hizo huchomwa katika siku saba za kwanza baada ya kifo, kwenye siku za ukumbusho, na ikiwa jamaa mmoja aota kwamba mtu aliyekufa anahitaji kufanya ununuzi,” yasema ripoti ya Shirika la Associated Press. “Ni biashara yenye faida,” adai Bw. Kwan, “kwa sababu mteja hawezi kurudi ili kulalamika.”

Vito Vyenye Nururishi

Vito vilivyouziwa mfanya-biashara mmoja katika Bangkok vilizusha tahadhari juu ya biashara ya kimataifa ilipofahamika kwamba vilikuwa na nururishi. Sahabudeen Nizamudeen, mfanya-biashara wa vito aliye mzoefu, hujua kama mapatano fulani ya biashara ni yenye faida. Kwa hiyo wakati mfanya-biashara mmoja kutoka Indonesia alipomtolea vito 50 vyenye kung’aa kwa bei ya chini kuliko ya kawaida, alivichukua mara moja. “Kila kimoja kilikuwa cha rangi ya chokoleti, na kugawanywa kati na nuru ya mlia wa kawaida unaofanana na mboni ya paka iliyopasuliwa, ambacho huwa bei ghali,” laripoti Asiaweek. Hata hivyo, imepatikana kwamba mg’ao wa vito hivyo ulitokana na chanzo kingine. Vilitiwa nururishi ili kuzidisha rangi yao ili thamani yao iongezeke. Jiwe jingine, lililopatikana kwenye maonyesho ya vito katika Hong Kong, lilionekana kuwa limepita mpaka wa usalama wa nururishi wa Asia kwa mara 25. “Kufikia sasa, tatizo hilo linapatikana tu kwa kito chenye kung’aa kiitwacho chrysoberyl,” lasema gazeti hilo.

Mazoea ya Usomaji

Kwa wastani, Wabrazili husoma vitabu 2.3 kila mwaka, laripoti Jornal da Tarde. Baada ya kutoka shuleni, wengi wa Wabrazili hawagusi vitabu kwa vyovyote tena. “Tatizo lenyewe,” asema katibu wa Wizara ya Utamaduni, Ottaviano de Fiore, “ni kwamba asilimia 60 ya vitabu visomwavyo katika Brazili huwa ni usomaji wa lazima” kwa watoto walio shuleni. “Kwa asilimia 40 ibakiyo, vingi ni vya kidini na vitabu vya kikundi fulani tu, vitabu kuhusu ngono, au vitabu vya kujifanyizia vitu,” lasema gazeti hilo la habari. Kuhusu mazoea ya usomaji, De Fiore aonelea: “Watoto hukusanyika pamoja katika familia, shuleni, na mbele ya televisheni. Ikiwa hakuna wasomaji katika familia, hawatapata kichocheo chochote pale.” Aongezea: “Kuhusu televisheni, idhaa kubwa hazitii moyo usomaji.”

Dini ya Kujibunia

Watu wengi kutoka Amerika ya Latini hufuata “dini ya kujibunia,” asema mwanasoshiolojia Fortunato Mallimaci. Watu wanajitenga na makanisa na imani, wakijihisi huru kufuatia mitaala ya yoga, kusoma kitabu kuhusu imani za kimafumbo za Mashariki, kuhudhuria mikutano ambapo wahubiri huponya, au kwenda kwenye sherehe za Wabrazili Weusi. “Jambo hili halimaanishi kuwa watu hawajali dini. Wanaamini, lakini wamebuni dini yao wenyewe,” asema Mallimaci. Akihutubia Mkutano wa Nne wa Mazungumzo ya Watu wa Kawaida katika Vituo vya Kusini vya Amerika ya Latini, mwanasoshiolojia huyo alisema kwamba “Ukatoliki ulikuwa unapatwa na marekebisho yatokezwayo na ‘migawanyiko mikubwa ya ndani na hitilafiano,’” laripoti ENI Bulletin.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki