Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 6/22 uku. 25
  • Televisheni—Ni Hatari Jinsi Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Televisheni—Ni Hatari Jinsi Gani?
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Televisheni Imekubadili Wewe?
    Amkeni!—1991
  • Kudhibiti Utazamaji wa TV
    Amkeni!—2006
  • Kutumia Televisheni kwa Uangalifu
    Amkeni!—2000
  • Dhibiti Televisheni Kabla Haijakudhibiti Wewe
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 6/22 uku. 25

Televisheni—Ni Hatari Jinsi Gani?

Katika Desemba 18, 1997, vichwa vya habari katika magazeti viliripoti kwamba katuni moja ya televisheni iliwafanya watu wengi wawe wagonjwa katika Tokyo, Japani. Mamia walipelekwa hospitalini. “Watoto fulani walitapika damu na wengine walikuwa na mishtuko ya moyo au wakapoteza fahamu,” likaripoti The New York Times. “Madaktari na wanasaikolojia wanaonya kwamba kisa hiki ni kikumbusha chenye kushtua juu ya jinsi ambavyo watoto wanavyoweza kudhuriwa kwa urahisi na vipindi fulani vya kisasa vya televisheni.”

Gazeti la New York Daily News lilisema: “Japani ilishikwa na hofu jana baada ya katuni ya televisheni ya dubwana fulani ilipofumbua macho yake mekundu na mamia ya watoto wakazimia na kufurukuta katika taifa lote.

“Karibu watoto 600 na watu wazima wachache walikimbizwa kwenye vyumba vya dharura Jumanne jioni baada ya kutazama . . . katuni ya televisheni.” Wengine walilazwa kwenye vitengo vya wagonjwa mahututi, wakiwa na matatizo ya kupumua.

Yukiko Iwasaki, mama ya msichana mwenye umri wa miaka minane, alieleza hivi: “Nilishtuka kumwona binti yangu akipoteza fahamu. Alianza kupumua tu nilipomgonga mgongoni.”

Watayarishaji wa vipindi vya televisheni vya watoto hawangeweza kueleza jinsi ambavyo mbinu ya uhuishaji wanayosema imetumiwa “zaidi ya mara mia moja” ingeweza kusababisha hatari na jeuri ya namna hiyo.

Wakitambua hatari za kutazama televisheni, wazazi fulani wamekagua kwa makini utazamaji wa televisheni au hata wakaondoa televisheni nyumbani mwao. Mzazi mmoja katika Allen, Texas, Marekani, aliona kwamba kabla hawajaondoa televisheni nyumbani mwao, watoto wake walikuwa “hawana makini, wenye kukasirika, wenye kukosa kushirikiana, na wenye uchoshi wa kudumu.” Aliendelea kueleza hivi: “Leo, karibu kila mmoja wa watoto wetu watano—walio na umri kuanzia miaka 6 hadi 17—wanafanya vizuri sana katika masomo. Baada ya kuacha kutazama televisheni, upesi wakasitawisha upendezi wa namna nyingi kutia ndani michezo, usomaji, sanaa, kutumia kompyuta, na kadhalika.

“Tukio moja hususa lenye kukumbukwa lilitukia yapata miaka miwili iliyopita. Mwana wangu, ambaye alikuwa na umri wa miaka 9 wakati huo, alipiga simu akitaka kurudi mapema . . . Nilipoenda kumchukua na kuuliza tatizo lilikuwa nini, alisema, ‘Karamu inachosha sana. Wanataka kuketi tu na kutazama televisheni!’”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki