Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/06 kur. 8-9
  • Kudhibiti Utazamaji wa TV

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kudhibiti Utazamaji wa TV
  • Amkeni!—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Dhibiti Televisheni Kabla Haijakudhibiti Wewe
    Amkeni!—1991
  • Je! Televisheni Imekubadili Wewe?
    Amkeni!—1991
  • Kutumia Televisheni kwa Uangalifu
    Amkeni!—2000
  • TV—Je, Ni Mwizi wa Wakati?
    Amkeni!—2006
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2006
g 10/06 kur. 8-9

Kudhibiti Utazamaji wa TV

“BAADA ya kuiwasha, tulitazama kila kitu kilichoonyeshwa, kimoja baada ya kingine,” anasema Claudine. “Hatungeizima hadi pale tulipotaka kwenda kulala.” Wengine husema: “Siwezi kuacha kuikodolea macho,” huku wengine wakisema, “Sitaki kutazama televisheni sana kama nifanyavyo, lakini siwezi kujizuia.” Je, unatumia muda mwingi kutazama televisheni? Je, unahofia athari ambazo huenda televisheni inaletea familia yako? Hapa kuna madokezo kadhaa yanayoweza kukusaidia kudhibiti tabia yako ya kuitazama.

1. UNATUMIA MUDA GANI KUITAZAMA? “Mtu mwerevu huzifikiria hatua zake,” yasema Methali 14:15. Inafaa kuchanganua tabia yako ya kutazama televisheni ili uone ikiwa kuna uhitaji wa kufanya marekebisho. Kwa juma moja andika kiasi cha wakati unaotumia kuitazama. Unaweza pia kuandika vipindi ulivyotazama, mambo uliyojifunza, na jinsi ulivyofurahia vipindi hivyo. Hata hivyo, lililo muhimu hasa ni kujua kiasi cha wakati ambacho unatumia kutazama televisheni. Huenda ukashangaa kujua kiasi cha wakati unachotumia. Huenda ukachochewa kufanya mabadiliko kwa kujua tu unatumia muda gani katika maisha yako kutazama televisheni.

2. PUNGUZA MUDA WA KUITAZAMA. Jaribu kuepuka kutazama televisheni kwa siku, juma, au mwezi mmoja. Au, unaweza kuamua kiasi cha wakati utakachotumia kuitazama kila siku. Ukipunguza wakati unaotumia kutazama televisheni kwa nusu saa kila siku, utakuwa na saa 15 za ziada kila mwezi. Tumia wakati huo kufanya mambo muhimu kama vile mambo ya kiroho, kusoma kitabu kizuri, au kutumia wakati pamoja na familia na marafiki. Uchunguzi mbalimbali umeonyesha kwamba watu ambao hawatazami televisheni sana huifurahia zaidi kuliko wale wanaoitazama kwa muda mrefu.

Njia moja ya kupunguza wakati unaotumiwa kutazama televisheni ni kuiondoa kwenye chumba cha kulala. Watoto walio na televisheni katika vyumba vyao hutumia saa moja na nusu zaidi wakiitazama kuliko watoto wasiokuwa nayo katika vyumba vyao. Isitoshe, mtoto anapokuwa na televisheni katika chumba chake, wazazi hawawezi kujua anatazama nini. Wazazi na wenzi wa ndoa watagundua kwamba wana wakati mwingi zaidi wa kutumia wakiwa pamoja ikiwa wataondoa televisheni katika vyumba vyao vya kulala. Wengine wamechagua kutokuwa na televisheni kabisa nyumbani.

3. CHAGUA UTAKACHOTAZAMA. Bila shaka kuna vipindi vingi vizuri unavyoweza kutazama. Badala ya kubadili-badili vituo au kutazama kitu chochote kinachoonyeshwa, angalia orodha ya vipindi mapema ili uchague vipindi utakavyotazama. Washa televisheni kipindi unachotaka kinapoanza na uizime mara tu kinapokwisha. Au badala ya kutazama kipindi kinapoonyeshwa, huenda ukapenda kukirekodi ili ukitazame baadaye. Hilo litakuwezesha kukitazama wakati unaokufaa zaidi na pia kuruka matangazo ya biashara.

4. UWE MTEUZI. Biblia ilitabiri kwamba wakati wetu kungekuwa na watu “wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda pesa, wenye kujidai, wenye majivuno, wakufuru, wasiotii wazazi, wasio na shukrani, wasio washikamanifu, wasio na upendo wa asili, wasiotaka makubaliano yoyote, wachongezi, wasiojizuia, wakali, wasiopenda wema, wasaliti, wenye vichwa vigumu, wenye kujivuna kwa kiburi, wanaopenda raha badala ya kumpenda Mungu.” Huenda ukakubali kwamba watu wengi wanaoigiza katika vipindi vya televisheni wana sifa hizo. Biblia inahimiza hivi: “Geukia mbali kutoka kwa hao.” (2 Timotheo 3:1-5) Tunaonywa hivi: “Msipotoshwe. Mashirika mabaya huharibu tabia nzuri.”—1 Wakorintho 15:33.

Kuwa mteuzi kunahusisha kujiweza. Je, umewahi kutazama kipindi au sinema fulani na baada ya dakika chache za kwanza ukatambua kwamba si nzuri, lakini bado ukaendelea kuitazama hadi mwisho ili ujue kitakachotokea? Wengi wamefanya hivyo. Hata hivyo, ukijitahidi na kuizima ili ufanye kitu kingine, utagundua kwamba hujali kilichotokea.

Muda mrefu kabla ya televisheni kubuniwa, mtunga-zaburi aliandika hivi: “Sitaweka mbele ya macho yangu kitu chochote kisichofaa.” (Zaburi 101:3) Hilo ni lengo zuri kama nini tunaloweza kuzingatia tunapochagua tutakachotazama! Watu fulani kama Claudine, wameamua kuondolea mbali televisheni zao. Anasema: “Sikutambua jinsi televisheni ilivyonifanya nikose huruma. Sasa ninapopata nafasi ya kutazama televisheni, ninashtuliwa na mambo ambayo hayakuwa yakinihangaisha. Nilifikiri kwamba nilikuwa nateua kwa busara kile ambacho nilitazama, lakini sasa nimetambua sikuwa nikifanya hivyo. Ninapotazama vipindi vizuri, mimi huvifurahia zaidi.”

[Picha katika ukurasa wa 8]

Andika kiasi cha wakati unachotumia kutazama televisheni

[Picha katika ukurasa wa 8]

Fanya mambo muhimu badala ya kutazama televisheni

[Picha katika ukurasa wa 9]

Usisite kuzima televisheni!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki