Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 7/22 uku. 3
  • Kuteswa na Woga

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuteswa na Woga
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Kudhibiti Hali ya Kuogopa Watu
    Amkeni!—1998
  • Kuwasaidia Watu Wenye Ugonjwa wa Wasiwasi Kupita Kiasi
    Amkeni!—2012
  • Macho Yote Yakuangaliapo
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 7/22 uku. 3

Kuteswa na Woga

“Mara nyingi woga umekuwa jambo la kudhihakiwa. Lakini huo si jambo la ‘kuchekesha’ kamwe.”—Jerilyn Ross, mkurugenzi wa hospitali ya magonjwa ya wasiwasi

NENO “woga” linarejezea hofu nyingi isiyofaa ya kitu, tukio, au hisia. Lakini ufafanuzi huo pekee hauwezi kuonyesha lile ogofyo na upweke ambao huwapata wale walio na huo woga. Raeann Dumont, ambaye ametibu wenye matatizo ya woga kwa zaidi ya miongo miwili, asema: “Watu wenye woga huelekea kuepuka hali nyingi sana hivi kwamba wanakuwa wafungwa nyumbani, au wao wanaweza kuishi wakiwa na wasiwasi wa daima dawamu, au wanaweza kuondoa wasiwasi wao kwa kunywa vileo, jambo liwezalo kuzidisha matatizo.”

Woga wa vitu upo katika kikundi kiitwacho magonjwa ya wasiwasi.a Inakadiriwa kwamba asilimia 12 ya watu wazima nchini Marekani watapatwa na woga wa vitu fulani katika pindi fulani ya maisha yao. Wengi wao wataugua kwa ukimya kwa miaka mingi. “Kwa ubaya,” laripoti Shirika la Marekani la Magonjwa ya Wasiwasi, “robo tatu hivi ya watu wenye woga hawapati msaada. Watu wengi wenye woga husita kutafuta msaada kwa sababu ya kuona aibu. Wengine hawaelewi tatizo lao au hawajui watapata msaada wapi, na wengine huogopa hata tiba yenyewe.”

Kuna mamia ya woga ujulikanao, lakini wataalamu mara nyingi huyaainisha katika vikundi vitatu. Woga wa kawaida huwa woga wa kitu fulani au hali fulani hususa kama wadudu, wanyama, kuogopa kupanda ndege, na woga wa kuwa katika sehemu zisizo wazi. Woga wa kuwa katika sehemu za peupe mara nyingi huandamana na hofu za ghafula. Mwenye woga huo huogopa kupatwa na hofu za ghafula hivi kwamba yeye huepuka sehemu zote na hali zote ambako alishikwa na hofu za ghafula. Kuogopa watu ni woga wa kuaibika mbele za watu, kama kuongea mbele ya wasikilizaji.

Fikiria mojawapo tu ya aina hizi tatu za woga—kuogopa watu. Gazeti The Washingtonian lataarifu: “Aina zote za woga wa kawaida zikijumlishwa pamoja, kama woga wa nyoka au wa kupanda ndege, hizo hazihuzunishi kama kuogopa watu.” Je, hiyo ni kweli? Ikiwa ndivyo, kwa nini? Ebu tuone.

[Maelezo ya Chini]

a Magonjwa mengine ya wasiwasi yanatia ndani hofu za ghafula, ugonjwa wa misukumo na mishurutisho, ugonjwa wa mkazo unaotokana na masaibu, na ugonjwa wa kawaida wa wasiwasi. Kwa habari zaidi, ona Amkeni! la Februari 8, 1996, “Mwenendo wa Kushurutisha—Je, Huo Hudhibiti Maisha Yako?” na Juni 8, 1996, “Kukabiliana na Mishiko ya Hofu ya Ghafula.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki