Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 8/22 uku. 31
  • Huwalinda Kondoo Dhidi ya Mbwa-mwitu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Huwalinda Kondoo Dhidi ya Mbwa-mwitu
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Maajabu ya Sufi
    Amkeni!—1992
  • Zuru Bara, Zuru Kondoo!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Kufuga Kondoo Ndiyo Kazi Yetu
    Amkeni!—1993
  • Mchungaji Mwenye Upendo
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 8/22 uku. 31

Huwalinda Kondoo Dhidi ya Mbwa-mwitu

MBWA-MWITU ni tisho kubwa kwa riziki ya wafugaji wa kondoo katika magharibi ya Marekani. Katika mwaka wa 1996 pekee, watu waliokuwa na idhini ya serikali ya kuwanasa waliua hao mbwa-mwitu zaidi ya 82,000, na tangu mwaka wa 1990, zaidi ya 600,000 wameuawa. Lakini wafugaji fulani wa kondoo wamegundua njia nyingine ya kulinda makundi yao. Wameleta lama kutoka Amerika Kusini.

Lama wana uhusiano na ngamia. Kwa kweli, mapema mwaka huu mbegu ya ngamia wa kiume iliunganishwa na ya lama wa kike, na pakazaliwa mnyama anayefanana na ngamia. Lama aweza kuwa na uzito wa kilogramu 100 na ana kimo cha wastani cha sentimeta 120 kwenye mabega. Ana singa ndefu ambazo kwa kawaida zina rangi nyeupe lakini zaweza pia kuwa za rangi ya kikahawia au nyeusi. Lakini jambo lililo la maana kwa wafugaji wa kondoo ni kwamba, lama hupendezwa na kondoo na huwafukuza mbwa-mwitu.

“Huwapiga mateke na kuzungusha kichwa chake,” aeleza mfugaji wa kondoo Becky Weed. “Kondoo wetu hawajaliwa na mbwa-mwitu kwa miaka minne.” Lakini akikiri kwamba lama si suluhisho kamili, Weed alisema: “Tulikuwa na dubu katika kundi letu na kuwapoteza kondoo wanne.”

Kikundi chenye kujali mazingira cha wafugaji wa kondoo kimeunda Ushirika wa Wafugaji wa Kondoo. Hilo ni shirika ambalo huuza sufu inayotajwa kuwa “isiyodhuru wanyama-wawindaji” yaani sufu kutoka kwa wafugaji wa kondoo ambao hutumia njia za kudhibiti wanyama-wawindaji bila kuwaua. Mbali na lama, mbwa walinzi na punda wadogo hutumiwa pia kuwalinda kondoo.

Ushirika wa Wafugaji wa Kondoo umefanya mkataba na wafumaji wa nyumbani ili kushona mavazi ya sufu. Sufu hiyo hutozwa zaidi, na sweta, kofia, blanketi na vitu vingine vinavyoshonwa kutokana nayo huwa ghali zaidi. Je, watu watalipia zaidi kwa vitu hivi? “Wao hulipa ninapowaelezea aina ya shamba la mifugo ilipotoka,” aeleza mwenye duka mmoja katika Chatham, New York. “Watu wanaipenda kwa sababu ya kisa kinachohusiana na sweta hiyo.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki