Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 9/8 uku. 3
  • Msiba wa Vifo vya Vijana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msiba wa Vifo vya Vijana
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Historia Ndefu ya Vifo vya Vijana
  • Tasmania—Kisiwa Kidogo, Simulizi la Kipekee
    Amkeni!—1997
  • Vijana Wanakabili Matatizo Gani?
    Amkeni!—2009
  • Vijana wa Leo—Matatizo Wanayokabili
    Amkeni!—1991
  • Biblia na Adili ya Utineja
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 9/8 uku. 3

Msiba wa Vifo vya Vijana

“Nahisi tu kwamba kizazi chetu kinakufa.”—Johanna P, mwenye umri wa miaka 18 na ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu, Connecticut, Marekani.

POLISI waliona mambo ya kustaajabisha sana katika shamba moja nje tu ya Hobart, jiji kuu la Tasmania, ambayo ni kisiwa na mkoa wa Australia. Ndani ya nyumba mlikuwamo wasichana wanne wenye umri wa kati ya miaka 10 na 18. Wote walikuwa wamekufa, wakiwa wameuawa na baba yao, ambaye naye alikuwa amelala karibu nao, akiwa amekufa kutokana na jeraha la risasi kichwani. Alikuwa amejikata mkono wa kulia kwa shoka. Hayo mauaji na kujiua yalishtua sana watu wote wa Tasmania. Na yalizusha swali lenye kutatanisha katika akili za watu—Kwa nini? Kwa nini wasichana hao wanne wasio na hatia walikufa?

Ubelgiji ingali imeshtuka kufuatia kisa cha kutendwa vibaya kingono kwa wasichana sita na kuuawa kwa wanne kati yao na mbakaji mmoja ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha nje. Na swali lilelile likazushwa—Kwa nini wasichana hao walikufa? Nchini Argentina akina mama wanaamini kwamba watu wapatao 30,000, wengi wao wakiwa wana wao na binti zao, walitoweka katika ile iliyoitwa vita chafu.a Baadhi yao waliteswa, walileweshwa dawa, kisha wakapelekwa baharini kwa ndege na kutumbukizwa humo. Wengi wao walitupwa wakiwa hai. Kwa nini walikufa? Mama zao wangali wanauliza.

Mnamo mwaka wa 1955 Mkutano wa Ulimwengu wa Akina Mama ulishutumu ubatili wa vita na kutangaza kwamba “zaidi ya jambo jingine lolote [mkutano huo] ni mwito mkubwa, mwito wa kutoa onyo kutoka kwa wanawake wote wanaojitahidi kulinda watoto wao, wakubwa kwa wadogo, dhidi ya maovu ya vita na matayarisho ya vita.” Kwa kushangaza, idadi ya vijana ambao wamekufa katika vita tangu mkutano huo ufanywe inaendelea kuongezeka ulimwenguni pote—kizazi ambacho kingetokeza wazao wenye vipawa mbalimbali kinapotea.

Historia Ndefu ya Vifo vya Vijana

Vijana wengi wamekufa katika historia. Hata katika karne yetu ya 20 iitwayo eti ya elimu, mapigano kati ya jamii na kati ya makabila yamelenga hasa kuua vijana. Yaonekana kwamba vijana wanalazimika kufa kwa makosa na tamaa za wakubwa wao.

Katika nchi moja ya Afrika, kikundi cha vijana wa kidini ambao wamekuwa wanajeshi wanaojiita Lord’s Resistance Army kimefundishwa kikaamini kwamba risasi haziwezi kuwapenya, laripoti jarida la The New Republic. Si ajabu kwamba makala hiyo ina kichwa kinachosema “Vijana Wasio na Uradhi”! Kwa hiyo, kwa haki familia zilizofiwa na wana na binti—ambao risasi zingeweza kuwapenya kwa haki zauliza: Kwa nini vijana wetu walikufa? Kwa nini haya yote yalitukia?

Kuongezea huzuni na mateseko hayo yote, ni ongezeko la kujiua miongoni mwa vijana.

[Maelezo ya Chini]

a Hiyo inayoitwa vita chafu ilitokea wakati wa utawala wa kijeshi (1976-1983) ambapo maelfu ya watu walioshukiwa kuwa wachochezi waliuawa. Makadirio mengine ya idadi ya waliouawa yataja baina ya watu 10,000 na 15,000.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki