Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 12/8 uku. 31
  • Fahari za Kimbingu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Fahari za Kimbingu
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • “Alfa na Omega” Ni Nani au Ni Nini?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Alpha na Omega
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Jinsi Yehova Anavyotupatia Uhakikisho wa Ahadi Yake ya Paradiso
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Nyota na Mwanadamu—Je! Kuna Uhusiano?
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 12/8 uku. 31

Fahari za Kimbingu

Miongoni mwa fahari zenye utukufu zaidi za kimbingu ni makundi ya kitufe ya nyota. Haya yana umbo la mviringo, na kila moja lina kati ya makumi ya maelfu na mamia ya maelfu ya nyota. Kuna makundi ya kitufe karibu 100 yanayojulikana katika galaksi yetu ya Njia ya Kimaziwa.

Katika ujirani wetu wa ile Njia ya Kimaziwa, nyota zimepangwa kwa wastani wa miaka-nuru minne hadi mitano kutoka moja hadi nyingine.a Katika kundi la kitufe, nyota zimesongamana sana, karibu sehemu moja ya kumi ya mwaka-nuru mmoja kutoka nyota moja hadi nyingine.

Kundi linaloonekana pichani ni Omega Centauri. Likitazamwa kwa macho, linaonekana kama nyota moja. Hata hivyo, kupitia darubini-upeo kubwa, linageuka kuwa kundi lenye kung’ara la nyota nyingi, jumla ya milioni moja hivi. Kundi la Omega Centauri laweza kuonekana vizuri zaidi katika Kizio cha Kusini, ingawa jioni za masika na kiangazi kufikia katikati ya latitudo za kaskazini, linaweza kuonwa chinichini kwenye upeo wa macho katika anga la kusini.

Kipenyo cha Omega Centauri ni karibu miaka-nuru 150; ingechukua karibu miaka 150 ili nuru isafiri kutoka chini hadi juu ya picha hii! Umbali wa kutoka kwenye dunia hadi Omega Centauri unakadiriwa kuwa miaka-nuru 17,000.

Kwa muda mrefu, Omega lilijulikana kuwa ni nyota moja. Katika karne ya 17, mwastronomia Mjerumani asiye stadi sana Johann Bayer alilipatia jina la herufi ya Kigiriki Omega (ω). Hata hivyo, aliyelichunguza kwanza kuwa ni kundi la kitufe alikuwa mwastronomia Mwingereza Edmond Halley katika mwaka wa 1677.

Katika Kizio cha Kaskazini, mojawapo ya makundi bora zaidi kutazama ni M13, katika kundi la nyota la Hercules. Lina nyota karibu milioni moja na liko umbali wa miaka-nuru 4,000 zaidi kutoka kwetu kuliko lilivyo Omega Centauri. Hivyo laonekana kuwa dogo zaidi.

Ukipata fursa ya kuchunguza kundi la kitufe kupitia darubini-upeo kubwa kiasi, fanya hivyo kwa vyovyote. Ni moja ya uumbaji wenye kuvutia zaidi unaoweza kuona katika anga la usiku.

[Maelezo ya Chini]

a Mwaka-nuru mmoja ni sawa na kilometa 9,460,530,000,000.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Omega Centauri

[Hisani]

National Optical Astronomy Observatories

[Picha katika ukurasa wa 31]

M13

[Hisani]

Kilimia na M13: Courtesy United States Naval Observatory

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki