Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 3/8 uku. 13
  • Baada ya Dhoruba Ukristo Ulidhihirishwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Baada ya Dhoruba Ukristo Ulidhihirishwa
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Wakristo Walivyotunza Waliokumbwa na Mafuriko Msumbiji
    Amkeni!—2001
  • Mungu Amekuwa Msaidiaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Roho ya Kujitolea Huleta Baraka
    Huduma ya Ufalme—2006
  • Kujenga Pamoja Duniani Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 3/8 uku. 13

Baada ya Dhoruba Ukristo Ulidhihirishwa

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA MSUMBIJI

MNAMO jioni ya Machi 2, 1998, jiji la Maputo, nchini Msumbiji, lilipigwa na dhoruba kali ya mvua. Kesho yake asubuhi, uharibifu mkubwa wa dhoruba ulienea kila mahali. Miti iliyoanguka ilitapakaa kila mahali kandokando ya ufuo, barabara ziliharibiwa na mafuriko, paa za nyumba fulani ziling’oka, na nyumba nyingine zilikuwa zimebomoka.

Majengo ya ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova yalisimama imara. Lakini nyumba moja sahili ya jirani ambayo ilikuwa imejengwa kwa nguzo za mbao na paa ya mabati, haikuweza kustahimili. Nyumba hiyo ilikuwa dhaifu mno kuweza kukinza pepo zenye nguvu, ikaanguka. Kwa uzuri, wote waliokuwamo, mwanamke mmoja na watoto wake watano, hawakujeruhiwa. Lakini, walipoteza karibu mali zao zote.

Mapema asubuhi, wafanyakazi wenye kujitolea kutoka kwenye ofisi ya tawi ya Watch Tower Society walizuru familia hiyo wakawapata wakitafuta mali zao chache kwenye mabaki hayo. Kupoteza mali kulizidisha huzuni yao, kwa kuwa hawakuwa na fedha za kutosha za kujenga nyumba nyingine. Bila baba, familia hiyo ilikuwa na mapato kidogo tu, ambayo walipata kwa kuuza vyakula katika soko la kwao.

Baada ya kuchunguza hali hiyo, Mashahidi wa Yehova wakajitolea haraka wakasaidie. Iliamuliwa kwamba vifaa vya ujenzi vilivyobaki kutokana na nyumba iliyoanguka havikufaa kutumika tena. Basi, ­kikundi cha wafanyakazi wenye kujitolea kikatafuta vifaa vinavyohitajika kikaanza kujenga nyumba ndogo yenye nguvu zaidi.

Mwanzoni majirani walikuwa wadadisi, lakini upesi wakapigwa na butaa walipoona kazi hiyo ikisonga mbele haraka sana. Kwa siku tano tu nyumba ilikuwa imejengwa upya kabisa na tayari kukaliwa. Mwanamke huyo alipoingia katika nyumba yake mpya, alibaki ameduwaa asijue la kusema. Lakini, haikuwa lazima aseme, kwa kuwa furaha ya mama na watoto wake ilidhihirika wakati wafanyakazi hao walipoona nyuso zao zenye tabasamu na macho yao yaliyoonyesha uthamini sana.

Wafanyakazi hao wenye kujitolea wakafurahi vilevile. Walifurahi kwamba walipata fursa ya kudhihirisha kwa njia halisi roho ya Ukristo wa kweli.—Wagalatia 6:10.

[Picha katika ukurasa wa 13]

Machi 5

Machi 6

Machi 7

Mashahidi wa huku walijenga upya nyumba ya familia hii

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki