Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 5/22 uku. 3
  • “Nina Umri wa Miaka Saba”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Nina Umri wa Miaka Saba”
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Maskini Waweza Kuwa Wafuataji Haki?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kwa Kazi Ngumu ya Watoto
    Amkeni!—1999
  • Walijitoa Wenyewe kwa Hiari—Nchini Mexico
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Kutumia Neno la Mungu Katika Jamaa Zetu Wenyewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 5/22 uku. 3

“Nina Umri wa Miaka Saba”

Jambo. Jina langu ni Amelia, ninaishi Karibea. Nina umri wa miaka saba. Hapo awali wazazi wangu maskini walinikabidhi kwa familia tajiri inayoishi jijini.

Leo, kama siku nyinginezo, niliamka saa 11 alfajiri. Nikateka maji kutoka kisima kilicho karibu. Haikuwa rahisi kusawazisha chungu hicho kizito kwenye kichwa changu, lakini nilifaulu—kama sivyo, ningepigwa sana. Kisha nikatayarisha na kuandalia familia kifungua-kinywa. Nilichelewa kidogo kuandaa kifungua-kinywa, kwa hiyo bwana-mkubwa akanicharaza kwa ukanda wa ngozi.

Baadaye, nilimpeleka shuleni mwana wa familia hiyo mwenye umri wa miaka mitano. Kisha, nikasaidia katika kupika na kuandalia familia chakula cha mchana. Licha ya kutayarisha milo, nililazimika kununua chakula sokoni na kufanya kazi nyingine, kuwasha jiko la makaa, kufagia ua, kufua nguo, kusafisha vyombo na jikoni. Nilimnawisha miguu bibi mwenye nyumba pia. Leo alikuwa amekasirishwa na jambo fulani, akanipiga kofi kwa hasira. Ninatumaini kwamba kesho atahisi vizuri.

Nilipewa kiporo nile—angalau kilikuwa bora kuliko sima niliyoila jana. Mavazi yangu ni matambara, nami sina viatu. Mabwana wangu hawajaniruhusu kamwe nioge kwa maji ninayoyateka kwa ajili ya familia. Jana usiku nililala nje; nyakati nyingine wao huniruhusu kulala sakafuni. Nasikitika kwa kuwa singeweza kuandika barua hii mwenyewe. Siruhusiwi kwenda shuleni.

Uwe na siku njema. Amelia.

IJAPOKUWA jina lake halisi si Amelia, hali yake mbaya ni halisi.a Amelia ni mmojawapo wa mamilioni ya watoto wanaolazimika kufanya kazi—na mara nyingi chini ya hali mbaya zaidi. Kuajiriwa kwa watoto ni tatizo kubwa sana katika nyakati zetu. Ni suala zito lisilokuwa na utatuzi sahili. Ni jambo lililoenea sana, linalovunja jamii, na lenye kufisha, ni katili kwa watoto na hutweza adhama ya binadamu.

Kuajiriwa kwa watoto kumeenea kadiri gani? Ni nini chanzo cha tatizo hili, na ni kazi za aina gani wanazofanya? Je, kutapata kuwa wakati ambapo watoto—sehemu dhaifu na iliyo rahisi kushambuliwa ya familia ya kibinadamu—hawataishi tena kamwe kwa taabu na kutumiwa vibaya?

[Maelezo ya Chini]

a Kisa chake kiliripotiwa katika kichapo The State of the World’s Children 1997.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki