Je, Unautambua Wimbo Huo?
KUUTAMBUA wimbo upi? Je, ni wimbo fulani wa kale uliopendwa sana? Naam, ni nyimbo za kale sana, na huenda ziwe nyimbo za kale zaidi kuwahi kusikiwa duniani. Ni nyimbo zipi hizo? Nyimbo za ndege.
Watu wengi huwatambua ndege kwa rangi zao, umbo lao, mitindo yao ya kupuruka, na mazoea yao ya kutengeneza viota. Lakini je, umewahi kusikiliza kwa makini ili uweze kuwatambua ndege kwa nyimbo zao?
Ni rahisi sana kuweza kuwatambua ndege fulani kwa nyimbo, kwa kuwa milio yao si ya namna nyingi. Kwa mfano, hebu fikiria kunguru mwenye utundu. Ajapokuwa mmojawapo wa ndege wenye akili sana, mlio wake wa kukwaruza wa “kao, kao” humtambulisha mara moja. Ndege aina ya rook hutambuliwa pia kwa sababu ya mlio wao wa ‘kao’ wenye kelele. Ndege mwingine, ambaye anaweza kukuudhi sana usiku kwa mlio wake wa huzuni ni whippoorwill. Jina lake lashabihi mlio wake, unaoendelea bila kukoma, hasa unapotaka kulala.
Kinyume na hao, “marsh wren kwa kawaida huweza kuimba nyimbo zaidi ya 100; ndege mwigo, nyimbo zipatazo 100 hadi 200. Ndege mmoja aina ya brown thrasher aliimba nyimbo zaidi ya 2,000”!—Kichapo Audubon, Machi-Aprili 1999.
Kwa kawaida ni ndege wa kiume wanaoimba ili kutenga maeneo yao na kuvutia wa kike. Ingawa nyakati nyingine ndege fulani wa kike hujiunga na korasi hiyo ya ndege. Hilo ni kweli kwa habari ya ndege aina ya Baltimore, au Northern, kirumbizi, cardinal wa Amerika Kaskazini, na grosbeak wenye kifua chekundu.
Je, wewe wajua ndege wa eneo lenu? Katika nchi nyingi kuna mirekodi ya nyimbo za ndege inayoweza kukusaidia utambue ndege kwa milio yao. Hata unaweza kununua saa zinazoashiria kupita kwa muda wa saa kwa wimbo wa ndege tofauti-tofauti. Angalau utajifunza nyimbo 12 upesi sana!
[Picha katika ukurasa wa 31]
Marsh wren
[Picha katika ukurasa wa 31]
Grosbeak mwenye kifua chekundu
[Picha katika ukurasa wa 31]
Cardinal