Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 12/8 uku. 5
  • Je, Ni Mapema Sana au Ni Kuchelewa Mno?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Ni Mapema Sana au Ni Kuchelewa Mno?
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Milenia ya Tatu Inaanza Lini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Milenia Mpya—Unaweza Kutarajia Nini Wakati Ujao?
    Milenia Mpya—Unaweza Kutarajia Nini Wakati Ujao?
  • Mileani (Miaka Elfu)—Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Mileani Ya Tatu—Je! Itatimiza Matumaini Yako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 12/8 uku. 5

Je, Ni Mapema Sana au Ni Kuchelewa Mno?

MAMBO mengi yanasemwa sasa kuhusu mwanzo wa karne ya 21 na milenia ya tatu baada ya Yesu Kristo kuzaliwa. Gazeti Newsweek lilisema kwamba “karne ya 20, iliyoanza kama Karne ya Vita Kamili na kukua hadi kuwa Muhula wa Atomu, inaisha ikiwa Enzi ya Vitumbuizo.” Katika toleo lake la Januari 22, 1997, liliripoti: “Tayari hoteli zimejaa ulimwenguni pote” kwa ajili ya sherehe za Siku ya Kuamkia Mwaka Mpya, Desemba 31, 1999.

Hata hivyo, watu fulani wanasema kwamba sherehe hizo zinafanyika mapema zaidi. Wanasema kwamba kinyume cha itikadi ya wengi, karne ya 21 na milenia mpya haianzi Januari 1, 2000, bali Januari 1, 2001. Kwa kuwa hakukuwa na mwaka wa 0, karne ya kwanza ilianza mwaka wa 1 hadi wa 100, karne ya pili ikaanza 101 hadi 200, na kadhalika. Hivyo, inadaiwa kwamba karne ya 20 iliyoanza Januari 1, 1901, na milenia ya pili, iliyoanza Januari 1, 1001, itaisha Desemba 31, 2000.

Kuna hoja nyingine ya ziada ya kufikiriwa. Kalenda yetu hugawanya wakati kwa msingi wa ama kabla ama baada ya kuzaliwa kwa Kristo. Sasa wasomi wanatambua kwamba Yesu alizaliwa mapema zaidi ya walivyofikiri hapo awali, hivyo kufanya sehemu ya kalenda iliyo ya maana sana isiwe sahihi. Kuna maoni tofauti kuhusu wakati alipozaliwa Yesu, lakini kronolojia ya Biblia huelekeza kwenye mwaka wa 2 K.W.K. Kwa kutegemea hesabu hiyo, milenia ya tatu baada ya kuzaliwa kwa Kristo kwa kweli ilianza katika vuli ya mwaka huu! Habari zaidi yaweza kupatikana katika toleo la Amkeni! la Mei 22, 1997, kwenye ukurasa wa 28, na la Desemba 22, 1975, la Kiingereza, kwenye ukurasa wa 27.a

Kwa vyovyote vile, ni jambo la hekima kutosema kwa dhati kwamba karne ya 21 na milenia mpya itaanza baada ya majuma machache tu. Hata hivyo, kwa kuzingatia maoni yanayopendwa na wengi, gazeti la Amkeni! laona inafaa wakati huu kuzungumzia habari “Karne ya 20—Miaka Muhimu ya Badiliko.”

[Maelezo ya Chini]

a Ona pia toleo la Mnara wa Mlinzi la Novemba 1, 1999.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki