Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 12/22 uku. 25
  • Wimbo Asioweza Kuusahau

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wimbo Asioweza Kuusahau
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Jitihada Yangu ya Kufanya Uchaguzi Wenye Hekima
    Amkeni!—2000
  • Yehova Hutenda kwa Uaminifu-Mshikamanifu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Tulipata Kazi Yenye Kuridhisha Zaidi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Msifu Yehova kwa Shangwe Kupitia Nyimbo
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 12/22 uku. 25

Wimbo Asioweza Kuusahau

“NIKIWA shuleni niliimba wimbo wa dini wenye maneno, ‘Yehova mkuu aliyetawazwa katika utukufu wake.’ Mara nyingi nilijiuliza, ‘Huyu Yehova ni nani?’”

Maneno hayo ya Gwen Gooch, ambaye ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova na ambaye simulizi lake la maisha lilichapishwa katika Mnara wa Mlinzi, lilifanya angalau msomaji mmoja ahisi namna hiyo.a Vera, kutoka Seattle, Washington, Marekani, akumbuka, “nilipatwa na jambo hilo hilo nikiwa katika shule ya sekondari.”

Baada ya kusikia wimbo fulani, Vera, kama ilivyokuwa na Gwen, alitaka sana kujua huyo Yehova angeweza kuwa nani. Vera aliridhika mnamo mwaka wa 1949 wakati ndugu yake alipomwambia kwa mara ya kwanza kuhusu Yehova, jina la kibinafsi la Mungu katika Biblia.

Vera amekuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova kwa muda upatao nusu karne sasa. Lakini hakusahau kamwe wimbo huo wa dini tangu wakati alipokuwa katika shule ya sekondari. “Kwa miaka mingi,” asema, “nimejaribu kutafuta chanzo chake.” Hatimaye, kwa msaada wa duka la muziki, alifanikiwa. Wimbo huo ulitungwa na Franz Schubert mwaka wa 1825. Kwa kweli maneno ya muziki huo humsifu Yehova. Kwa mfano, haya ni baadhi ya maneno hayo:

“Yehova ni mkuu, yule Bwana! kwa kuwa Mbingu na Dunia hutangaza uwezo wake wa ajabu. . . . Unausikia kwenye dhoruba isiyotulia, iliyochafuka, palipo na mngurumo wa kijito . . . Unausikia palipo na sauti za mwitu na misitu, unauona kwenye mhindi unaopeperuka wa rangi ya kidhahabu katika maua yanayonukia vizuri kwenye mpangilio maridadi, katika nyota zinazoijaza anga ya Mbingu ya rangi ya buluu . . . Uwezo wa Yehova ni wenye kutia hofu unavuma kwa mpigo wa radi na mng’ao wa umeme angani. Lakini kwa kiasi kikubwa sana moyo wako unaodunda ungali unatangaza uwezo wa Yehova, . . . Bwana Mungu wa milele. Mwadhimishe na utazamie mazuri na rehema. . . . Yehova ni mkuu, na Bwana!”

Vera asema: “Nyakati nyingine nimetumia maneno ya wimbo huo kuonyesha watu kwamba katika miaka ya 1800 kulikuwa na watu waliojua jina la Mungu na kumsifu pia.” Ukweli ni kwamba kutoka nyakati za mapema zaidi wanaume na wanawake wenye imani wamechochewa kumsifu Yehova kwa nyimbo. Ni jambo litakaloendelea milele, kwa kuwa hatutakosa kamwe sababu za kumsifu Muumba wa mbingu na dunia.

[Maelezo ya Chini]

a Ona Mnara wa Mlinzi, Machi 1, 1998.

[Picha katika ukurasa wa 25]

Vera

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki