Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g00 3/8 uku. 31
  • Eneo la Makaburi Lisilo la Kawaida

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Eneo la Makaburi Lisilo la Kawaida
  • Amkeni!—2000
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Ambavyo Wengine Hutoa Upaji kwa Ajili ya Kazi ya Kuhubiri Ufalme
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Sababu kwa Nini Trakti ni Zenye Thamani Katika Huduma Yetu Leo
    Huduma Yetu ya Ufalme—1993
  • Ekuado—Nchi Inayovuka Ikweta
    Amkeni!—1998
  • Kuchapa na Kugawanya Neno Takatifu la Mungu Mwenyewe
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2000
g00 3/8 uku. 31

Eneo la Makaburi Lisilo la Kawaida

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA EKUADO

KATIKA mji wa Ibarra, kaskazini ya jiji kuu la Ekuado, Quito, kuna eneo la makaburi lisilo la kawaida—el cementerio de los pobres (Makaburi ya Watu Maskini). Ni nini kinachofanya eneo hilo lisiwe la kawaida? Michoro iliyo kwenye ukuta wa nje ni picha kutoka kwa vichapo vya Watch Tower Society zilizonakiliwa kikamili na kufanywa kubwa!a Kuna mchoro wa mtume Yohana katikati, ulionakiliwa kutoka ukurasa wa 7 wa kitabu cha Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu! Juu ya Yohana, kuna andiko hili katika Kihispania: “Ufalme wa Mungu wamaanisha uadilifu na amani na shangwe. Waroma 14:17.” Kati ya hizo picha mbili kuna maneno ya Mathayo 11:28: “Njoni kwangu, nyingi nyote mnaomenyeka na kulemezwa mizigo, nami hakika nitawaburudisha nyinyi,” yaliyofasiliwa kutoka kwa Tafsiri ya Ulimwengu Mpya. Bila shaka ukuta huu wa eneo hilo la makaburi unaelekeza watu kwa Neno la Mungu.

[Maelezo ya Chini]

a Ili kutekeleza matakwa ya kisheria, ni lazima idhini itolewe kabla ya kunakili makala au kuchora picha kutoka kwenye vichapo vya Watch Tower, na yapasa kuonyeshwa kwamba zimetoka kwa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki