Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g02 2/8 uku. 3
  • “Siku Yenye Furaha Zaidi Maishani Mwetu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Siku Yenye Furaha Zaidi Maishani Mwetu”
  • Amkeni!—2002
  • Habari Zinazolingana
  • Ongeza Shangwe na Heshima ya Siku Yako ya Arusi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Arusi za Kikristo Zapaswa Kuonyesha Kiasi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Ni Arusi ya Namna Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Sanduku la Swali
    Huduma Yetu ya Ufalme—2008
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2002
g02 2/8 uku. 3

“Siku Yenye Furaha Zaidi Maishani Mwetu”

SIKU ya arusi ni kipindi chenye shangwe. Wenzi wengi wa ndoa wamesema hivi: “Ilikuwa siku yenye furaha zaidi maishani mwetu.” Hata hivyo, inaweza kuwa siku yenye shughuli nyingi sana. Maarusi na familia zao huenda wakachoka na kufadhaishwa sana kwa sababu ya maamuzi mengi ya kufanya na matayarisho mengi na vilevile kwa sababu ya kuwakaribisha wageni wengi siku hiyo.

Siku ya arusi ni mwanzo wa maisha mapya ya maarusi. Lakini si hao wawili tu wanaoathiriwa. Wengine katika familia hufurahi wakati binti, mwana, dada, au ndugu anapofunga ndoa, lakini wao huhuzunika vilevile wakati huyo mpendwa anapowaacha na kuhamia makazi yake mwenyewe.

Desturi za arusi za nchi mbalimbali hutofautiana, na haiwezekani kuzungumzia zote hapa. Mfululizo huu unakazia desturi za nchi za Magharibi na nchi nyingine kama hizo. Kufanya arusi katika nchi hizo kunaweza kugharimu pesa nyingi sana. Baadhi ya watu hutumia fedha nyingi sana kwa mambo ya arusi, kama vile kukodisha jumba au hoteli kwa ajili ya karamu na kuwakaribisha wageni. Gharama ya arusi ya wastani nchini Italia inakadiriwa kufikia zaidi ya dola 10,000 za Marekani. Nchini Japani na katika nchi nyingine gharama zinaweza kuwa juu zaidi. Maarusi huwa hawalipi gharama hizo, bali ni wazazi wao ambao huzilipa.

Kuuza vitu vya arusi ni biashara kubwa. Biashara nyingi huwashawishi watu kuwa na arusi “kamilifu.” Wenye biashara hizo husema kwamba hakupaswi kukosekana chochote; kwani, “hiyo ni siku yenye furaha zaidi maishani mwako!” Kwa hiyo, wao huuza vitu vingi na kutoa huduma mbalimbali, ambazo ni “za lazima” ili kufanya siku yako kuu iwe “kamilifu.” Vitu hivyo vyatia ndani kadi za mwaliko, nguo “maridadi zaidi” ya bibi-arusi, nguo za wasindikizaji wa bibi-arusi, na makoti maalumu au suti za aina moja kwa ajili ya marafiki wanaume wa bwana-arusi. Kisha, kuna maua, magari makubwa ya anasa, hoteli kwa ajili ya karamu, mpiga-picha, wanamuziki, na kadhalika. Orodha ya vitu ambavyo maarusi wangetaka ni ndefu, na vilevile orodha ya gharama, nazo zinaweza kufanya akina baba wengi watetemeke.

Watu wa jamii mbalimbali hufuata sana desturi. Na wanatazamia maarusi wafuate desturi mbalimbali zinazohusu arusi. Ndiyo, kuna mambo mengi yanayopasa kutayarishwa, lakini muda wa kuyapanga ni mfupi.

Je, unasisimuka au unakata tamaa unapofikiria matayarisho hayo yote? Hata jibu lako liwe nini, matayarisho ya arusi hutokeza maswali kadhaa. Kufunga ndoa kunamaanisha nini leo? Je, mambo yote hayo ni ya lazima ili mtu aoe au aolewe “ifaavyo”? Matatizo ya matayarisho na mfadhaiko unaweza kukabiliwa jinsi gani?

Licha ya magumu, wengi wamefanikiwa kupanga arusi yao, nao wamefurahia siku hiyo. Kujua jinsi walivyofanikiwa kunaweza kuwasaidia wengine wanaopanga kufunga ndoa. Na kuna kanuni za Biblia zinazoweza kuwasaidia wale wanaopanga arusi, ili siku hiyo ipate kuwa ya kupendeza, ya kujenga, na ya shangwe.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki