Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g04 8/8 uku. 31
  • Vitu Bora vya Kuchezea

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vitu Bora vya Kuchezea
  • Amkeni!—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Vitu vya Kuchezea vya Zamani na vya Sasa
    Amkeni!—2005
  • Vichezeo vya Leo—Hufundisha Watoto Wetu Nini?
    Amkeni!—1994
  • Wazazi—Chagueni Vichezeo vya Mtoto Wenu kwa Hekima
    Amkeni!—1994
  • Wazazi—Mtoto Wenu Anacheza na Nini?
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2004
g04 8/8 uku. 31

Vitu Bora vya Kuchezea

Nimnunulie mtoto wangu kitu gani cha kuchezea? Nitumie pesa ngapi kukinunua? Ikiwa wewe ni mzazi, huenda umeuliza maswali hayo mara nyingi. Ama kweli, utafurahi kujua kwamba vitu bora vya kuchezea havigharimu pesa nyingi.

Kitabu Motivated Minds—Raising Children to Love Learning kinasema: “Watoto hufaidika zaidi wanaposhiriki na kuchunguza mambo kuliko wanapokuwa watazamaji tu, hivyo vitu sahili vya kuchezea vinavyowachochea kuwa wabunifu ni bora kuliko magari ya kuchezea yanayoendeshwa kwa betri au wanasesere wanaozungumza, kwani vitu hivyo vinamzuia mtoto kufanya mambo mengi.” Vitu hivyo vya kuchezea vilivyotajwa mwisho vinaweza “kufurahisha mwanzoni, lakini kwa kawaida watoto huacha kupendezwa navyo upesi kwa sababu haviwawezeshi kuchunguza, kuvumbua, na kubuni mambo.”

Ikitegemea umri wa mtoto, vitu vya kuchezea vinavyochochea akili vinaweza kutia ndani vidude vya kujengea vitu, boksi tupu, karatasi, vitu vya kuchorea, na hata mchanga na maji. Kitabu Motivated Minds kinasema: “Vitu vidogo vya kuchezea kama vile vinavyofanana na wanyama wa kufugwa, vitamwezesha mtoto kutenganisha na kulinganisha vitu na kujua lugha kwa kutunga hadithi.” Kitabu hicho pia kinapendekeza watoto watumie ala sahili za muziki, kwani zinawawezesha kujua sauti na mpangilio wake, maadamu mzazi yuko tayari kuvumilia kelele.

Watoto ni wabunifu sana na wanapenda kujifunza na kucheza. Kwa hiyo, wasaidie kufanya mambo hayo matatu kwa kuwachagulia kwa hekima vitu vya kuchezea.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki