Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 9/11 uku. 3
  • Ulimwengu Unakumbwa na Poromoko Kubwa la Uchumi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ulimwengu Unakumbwa na Poromoko Kubwa la Uchumi
  • Amkeni!—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Yafaa Kujiingiza Katika Deni?
    Amkeni!—1995
  • Kufutwa Kazi— Hofu ya Mwajiriwa
    Amkeni!—1992
  • Deni! Kuingia Humo Kutoka Humo
    Amkeni!—1991
  • Kukabiliana na Madeni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 9/11 uku. 3

Ulimwengu Unakumbwa na Poromoko Kubwa la Uchumi

“HALI mbaya zaidi ya kiuchumi katika kizazi chote.” Hivyo ndivyo Encyclopædia Britannica Online ilivyofafanua kuzorota kwa uchumi ambako kulitokea hivi karibuni. Hali hiyo mbaya ya kiuchumi iliyoanzia huko Marekani katika mwaka wa 2007 imekuwa mbaya sana na imeathiri nchi nyingi hivi kwamba imeitwa Poromoko Kubwa la Uchumi.

Ni nini kilichoisababisha? Gazeti Newsweek lilitoa jibu hili rahisi: “Msisimuko wa kukopa bila akili.” Lakini ni nini kilichochochea msisimuko huo wa kukopa ili kununua vitu ambavyo watu hawawezi kulipia?

Huenda utakubali kwamba mfumo wa kiuchumi wa ulimwengu ambao unachochea watu kuwa na pupa ndio uliowasukuma watu wakope. Mtazamo ulioenea ulikuwa ni: “Nunua! Nunua! Nunua!” iwe unaweza kulipa au la. “Kizazi chetu kimejionea madhara ya kukopa pesa kupita kiasi,” anaeleza mtaalamu wa uchumi Chris Farrell katika kitabu chake The New Frugality.

Nchi nyingi ziliathiriwa na Poromoko hilo Kubwa la Uchumi. “Ingawa inaonekana ni kana kwamba hali inatulia,” kikasema kichwa fulani kikuu cha mwaka uliopita katika gazeti Sunday Times la Afrika Kusini, “bado watu . . . wanang’ang’ana kupata chakula.” Gazeti hilo liliripoti kwamba “kwa zaidi ya miezi mitatu, watu 3 000 000 hivi [huko Afrika Kusini] hawajalipia huduma wanazopata; na watu 250 000 wanaopata mapato ya kadiri wamepoteza kazi katika miaka miwili iliyopita.”

Makumi ya mamilioni ya watu wamepoteza kazi katika miaka ya karibuni. Ingawa ripoti zinasema kwamba hali nchini Marekani zinaanza kuwa bora, gazeti Financial Times lilisema: “Majaribio ya kurekebisha mambo tangu Juni (Mwezi wa 6) 2009 yanaweza kusemwa kuwa ni yenye kukatisha tamaa kabisa.” Gazeti hilo liliongezea hivi: “Wataalamu wengi wa uchumi wanafikiria kwamba kwa kuwa watu wengi wanahitaji kulipa madeni, hawataweza kununua vitu kwa miaka kadhaa inayokuja, na hivyo kuzuia kukua kwa uchumi.”

Ikiwa wewe umeathiriwa na Poromoko hilo Kubwa la Uchumi, bila shaka unaweza kuelewa mambo ambayo mwandishi David Beart aliandika: “Inaonekana ni kama mambo mengi sana yamesemwa kuhusu matatizo ya uchumi ya ulimwengu, lakini ni habari chache sana zinazotolewa kuhusu njia za kutatua matatizo hayo.”

Habari zinazofuata zimekusudiwa kuwasaidia watu wanaokabiliana na madeni. Maswali yafuatayo yatajibiwa: Kuweka pesa akiba kuna faida gani? Unaweza kufanya nini ikiwa una deni? Unaweza kujifunza jinsi gani kutumia pesa kwa hekima?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki