Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g23 Na. 1 kur. 9-11
  • Misitu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Misitu
  • Amkeni!—2023
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Tunahitaji Kulinda Misitu Yetu
  • Dunia Yetu Imeumbwa Ikiwa na Uwezo wa Kuokoka
  • Hatua Zinazochukuliwa Sasa
  • Sababu za Kuwa na Tumaini —Biblia Inasema Nini
  • Ni Nani Atakayeokoa Misitu ya Mvua?
    Amkeni!—2003
  • Misitu ya Mvua Je, Inaweza Kuokolewa?
    Amkeni!—2003
  • Manufaa za Misitu ya Mvua
    Amkeni!—1998
  • Kutumiwa Vibaya kwa Misitu ya Mvua
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2023
g23 Na. 1 kur. 9-11
Mwanamke akitembea katika daraja linaloning’inia msituni.

JE, DUNIA YETU ITAOKOKA?

MISITU

MISITU imeitwa kwa kufaa “mapafu na mfumo unaotegemeza uhai duniani.” Miti hufyonza kaboni dioksidi ambayo inaweza kutuletea madhara. Pia, inatoa oksijeni ambayo ni sehemu muhimu sana ya hewa tunayopumua. Asilimia 80 hivi ya mimea na wanyama wanaishi misituni. Kusingekuwa na uhai bila misitu.

Kwa Nini Tunahitaji Kulinda Misitu Yetu

Kila mwaka, mabilioni ya miti hukatwa ili maeneo hayo yatumiwe kwa ajili ya kilimo. Tangu mwishoni mwa miaka ya 1940, nusu ya misitu duniani imetoweka.

Msitu unapoharibiwa, mimea na wanyama walio ndani yake huangamizwa pia.

Dunia Yetu Imeumbwa Ikiwa na Uwezo wa Kuokoka

Baadhi ya misitu ambayo imekatwa imeonyesha uwezo wake wenye kustaajabisha wa kurudia hali yake ya awali na hata kuongezeka. Hivi karibuni, wataalamu wa mazingira wameshangazwa na jinsi ambavyo miti iliyokatwa imekua haraka na kufanyiza misitu maridadi tena. Fikiria mifano ifuatayo:

  • Watafiti wamechunguza ardhi ya misitu iliyokatwa kwa ajili ya kilimo na kisha kutelekezwa. Utafiti katika maeneo 2,200 ya Amerika na Afrika Magharibi, ulionyesha kwamba udongo wa maeneo hayo ungeweza tena kuwa na misitu ndani ya miaka kumi.

  • Kulingana na utafiti uliochapishwa na gazeti la Science, watafiti wanakadiria kwamba ndani ya miaka 100, misitu hiyo inaweza kurudia hali iliyokuwa nayo kabla ya miti kukatwa.

  • Hivi karibuni, wanasayansi nchini Brazili walichunguza ikiwa misitu ya asili hukua kwa kasi zaidi inapolinganishwa na misitu inayopandwa na wanadamu.

  • Likizungumzia utafiti huo, gazeti la National Geographic linasema hivi: “Wanasayansi walifurahi walipogundua kwamba hakukuwa na uhitaji wa kupanda miti.” Baada ya miaka mitano tu, maeneo ambayo hayakuwa yamepandwa miti, “yalikuwa na miti mingi ya asili.”

    JE WAJUA?

    Kutoka Kuwa Mashamba Hadi Misitu

    Mchoro unaoonyesha eneo ambalo miti yake imekatwa kwa ajili ya kilimo na baadaye kutelekezwa. Miaka kumi baadaye, udongo unaweza kurudia hali nzuri. Baada ya miaka mia moja au zaidi, eneo linatazamiwa kuwa msitu.

    Maeneo ambayo misitu yake imekatwa kwa ajili ya kilimo na kisha kutelekezwa, yameonyesha uwezo mkubwa wa kiasili wa kurudia hali yake. Misitu mingine iliyoharibiwa inaweza pia kurudia hali yake nzuri.

Hatua Zinazochukuliwa Sasa

Ulimwenguni pote, jitihada zimefanywa ili kutunza misitu iliyopo na kurudisha ile iliyoharibiwa. Kama matokeo, kulingana na Umoja wa Mataifa, “ukataji miti umepungua kwa asilimia 50 duniani,” ndani ya miaka 25 iliyopita.

Hata hivyo, jitihada hizo hazitoshi kuokoa misitu yetu. Ripoti iliyotolewa na shirika la Global Forest Watch inasema: “Idadi ya misitu inayoharibiwa haijabadilika sana katika kipindi cha miaka michache iliyopita.”

Ukataji wa miti usio halali ni biashara inayoingiza mabilioni ya dola za Marekani, na jambo hilo ni chanzo cha uharibifu wa misitu ya mvua.

Bwana misitu akichunguza miti katika msitu.

Vikundi vya usimamizi wa misitu vinafanya kazi ili kulinda misitu kwa kukata kiwango kidogo cha miti mikubwa na kupanda mingine

Sababu za Kuwa na Tumaini —Biblia Inasema Nini

“Yehovaa Mungu akachipusha ardhini kila mti wenye kupendeza macho na unaofaa kwa chakula.”—Mwanzo 2:9.

Muumba wa misitu yote, aliiumba ikiwa na uwezo wa asili wa kujirekebisha kutokana na uharibifu unaosababishwa na wanadamu. Anataka kuitunza na kuidumisha misitu yetu pamoja na mifumo yake bora ya mazingira.

Biblia inasema kwamba Mungu hataruhusu wanadamu wenye ubinafsi waiharibu dunia yetu na viumbe walio ndani yake. Ona makala yenye kichwa “Mungu Anaahidi Kwamba Dunia Yetu Itaokoka,” katika ukurasa wa 15.

a Yehova ni jina la kibinafsi la Mungu.—Zaburi 83:18.

JIFUNZE MENGI ZAIDI

Wenzi wa ndoa wakifurahia dunia paradiso.

Tunawezaje kuwa na uhakika kwamba ubinafsi wa wanadamu hautasababisha uharibifu wa dunia yetu? Tazama video yenye kichwa, Kwa Nini Mungu Aliiumba Dunia? kwenye jw.org/sw.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki