Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 15 kur. 63-66
  • Mtumwa Asiyesamehe

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtumwa Asiyesamehe
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Tuwe Wenye Kusamehe?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Somo Juu ya Kusamehe
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Somo la Kusamehe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Umuhimu wa Kusamehe
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 15 kur. 63-66

Sura ya 15

Mtumwa Asiyesamehe

YE YOTE amepata kukutenda jambo baya? Alikuumiza au akasema vibaya kwako? Uliona vibaya, sivyo?—

Jambo kama hilo litukiapo, je! utamtenda vibaya mtu mwingine kwa njia ile ile aliyokutenda wewe? Watu wengi wangefanya hivyo.

Lakini Mwalimu Mkuu alisema imetupasa tusamehe wale wanaotutenda mabaya. Kuonyesha namna kusamehe ni kwa maana sana, Yesu alisimulia hadithi. Ungependa kuisikia?—

Palikuwa na mfalme. Alikuwa mfalme mzuri. Alikuwa mwenye huruma sana. Hata angekopesha watumwa wake fedha walipotaka msaada.

Lakini ikaja siku wakati mfalme alipotaka fedha yake ilipwe. Basi akawaita watumwa wake waliomkopa fedha, akawaambia wamlipe. Basi, mtu mmoja alimkopa mfalme vipande vya fedha milioni sitini! Ni fedha nyingi sana hizo. Ni fedha nyingi zaidi kuliko ambazo nimekuwa nazo katika maisha yangu yote.

Mtumwa huyu alikuwa amekula fedha za mfalme asiwe na kitu cha kulipa. Basi mfalme akaamuru mtumwa huyo auzwe. Tena mfalme akasema kuuza mke wa mtumwa na watoto wake na kila kitu kilichokuwa mali ya mtumwa. Ndipo kwa mnada huo zingepatikana fedha za kumlipa mfalme. Wewe wadhani hili lilimfanya mtumwa aoneje?—

Yule mtumwa akamwomba mfalme: ‘Tafadhali, usinitende hivyo. Nipe nafasi zaidi, nami nitakulipa kila kitu ninachodaiwa na wewe.’ lkiwa ungekuwa mfalme, ungalimtendaje mtumwa yule?—

Mfalme mzuri akamsikitikia mtumwa wake. Basi akamwambia mtumwa kwamba haikuwa lazima alipe ile fedha. Haikuwa lazima alipe cho chote cha vipande vya fedha milioni sitini! Lo! mtumwa yule alifurahi kama nini!

Lakini ndipo mtumwa yule akafanya nini? Akaondoka akamkuta mtumwa mwingine aliyemkopa vipande vya fedha mia moja tu. Hizo si fedha nyingi hata zikilinganishwa na vipande milioni sitini. Yule mwanamume akamkamata mtumwa mwenzake akamshika koo. Akamwambia: ‘Lipa zile fedha mia moja ulizonikopa.’

Unaweza kuwazia mtu akifanya jambo kama hilo? — Yule mtumwa alikuwa amesamehewa sana na mfalme mzuri. Na sasa kageuka kamdai mtumwa mwenzake alipe fedha mia moja. Hili halikuwa jambo zuri kufanya.

Basi, yule mtumwa aliyekopa fedha mia moja tu alikuwa maskini. Hakuweza kulipa fedha mara hiyo. Hivyo akaanguka miguuni pa mtumwa mwenzake akamwomba: ‘Tafadhali nipe nafasi zaidi, nami nitakulipa unachonidai.’ Je! ingalifaa yule mtu ampe mtumwa mwenzake nafasi zaidi?— Wewe ungalifanya hivyo?—

Basi, mtu huyu hakuwa na huruma, kama alivyokuwa mfalme. Kwa sababu mtumwa mwenzake hakuweza kumlipa mara hiyo, alimtu-pia kifungoni. Hakika hakuwa mwenye kusamehe.

Watumwa wengine waliona yote haya yakitukia. Wakamwambia mfalme juu yake. Mfalme alimkasirikia sana yule mtumwa asiyesamehe. Basi akamwita, akasema: ‘Wee mtumwa mbaya, je! mimi sikusamehe ulichonikopa? Hivyo, je! isingalikupasa umsamehe mtumwa mwenzako?’

Ingalimpasa afuate mfano wa mfalme mzuri. Lakini hakuufuata. Sasa basi mfalme akaamuru mtumwa asiyesamehe atupwe kifungoni mpaka alipe vile vipande vya fedha milioni sitini. Bila shaka, huko kifungoni asingeweza kuchuma fedha za kulipa deni. Hivyo angekaa huko mpaka kufa.

Yesu alipomaliza kusimulia hadithi hii, akawaambia wafuasi wake: ‘Katika njia iyo hiyo Baba yangu wa mbinguni atawatenda ninyi msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.’—Mathayo 18:21-35.

Unaona, sisi sote tuna deni nyingi sana kwa Mungu. Uhai wetu watoka kwa Mungu, lakini kwa sababu tunafanya mabaya yeye angeweza kutunyang’anya. Ikiwa tungejaribu kumlipa Mungu kwa fedha, katika muda wetu wote wa maisha tusingeweza kuzipata fedha za kutosha kumlipa deni yetu.

Inapolinganishwa na kile tunachomkopa Mungu, ambacho watu wengine wanatukopa ni kidogo sana. Wanachotukopa ni kama vipande vya fedha mia moja ambavyo mtumwa mmoja alimkopa mwingine. Lakini tunachomkopa Mungu ni kama vipande vya fedha milioni sitini ambavyo mtumwa yule alimkopa mfalme.

Mungu ni mwenye huruma sana. Ingawa tumefanya mambo mabaya mengi, yeye atatusamehe. Yeye hatataka tulipe kwa kutunyang’anya maisha zetu milele. Lakini yeye anatusamehe sisi hapo tukimwamini Mwanawe Yesu tu, na tukisamehe watu wengine wanaotutenda mabaya. Hilo ni jambo la kufikiria, sivyo?—

Basi, mtu akikutenda vibaya, halafu anasema anasikitika, utafanyaje? Utamsamehe?— Na ikitukia mara nyingi je? Bado utamsamehe?—

lkiwa tungekuwa mtu aliyekuwa akiomba kusamehewa, tungetaka mtu mwingine atusamehe, sivyo?— Imetupasa tumtende vivyo hivyo. Haitupasi kusema tu kwamba tumemsamehe, bali imetupasa kweli tumsamehe kwa moyo wetu. Tufanyapo kila, tunaonyesha kweli twataka tuwe wafuasi wa Yesu.

(Kutia mikazo ukubwa wa kuwa mwenye kusamehe, soma tena Mathayo 6:14, 15, Luka 17:3, 4 na Mithali 19:11.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki