Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 3/1 kur. 8-9
  • Somo la Kusamehe

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Somo la Kusamehe
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Somo Juu ya Kusamehe
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Umuhimu wa Kusamehe
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kwa Nini Tuwe Wenye Kusamehe?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Mtumwa Asiyesamehe
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 3/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma na Yesu

Somo la Kusamehe

INAONEKANA bado yumo katika ile nyumba katika Kapernaumu pamoja na wanafunzi wake. Yeye amekuwa akizungumza pamoja nao jinsi ya kushughulikia magumu kati ya akina ndugu, kwa hiyo Petro anauliza: “Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atende dhambi dhidi yangu mimi na mimi nimsamehe yeye? ” Kwa kuwa walimu wa kidini walio Wayahudi wananuiza jambo la kutoa msamaha kufikia mara tatu, Petro labda anafikiri ni ukarimu sana kudokeza hivi: “Mpaka mara saba?”

Lakini lile wazo lote la kuweka kumbukumbu ya namna hiyo ni lenye makosa. Yesu anasahihisha Petro: “Mimi nasema kwako wewe, si, Mpaka mara saba, bali, Mpaka mara sabini na saba.” Yeye anaonyesha kwamba hakuna hadi fulani inayopasa kuwekwa juu ya hesabu ya mara ambazo Petro anapaswa kusamehe ndugu yake.

Kukazia juu ya wanafunzi wajibu wao wa kuwa wenye kusamehe, Yesu anaendelea mbele kusimulia kielezi. Ni juu ya mfalme mmoja ambaye anataka kumaliza mahesabiano pamoja na watumwa wake. Mtumwa mmoja analetwa kwake ambaye ana deni kubwa sana la dinari 60,000,000 (karibu dola 50,000,000). Hakuna njia ambayo yeye anaweza kulipa deni hilo. Kwa hiyo, kama vile Yesu anavyoeleza, mfalme yule anaagiza mtu huyo na mke wake na watoto wake wauzwe kisha malipo yafanywe.

Mambo yanapokuwa hivyo, mtumwa yule anajiangusha chini ya nyayo za bwana-mkubwa wake na kuombaomba hivi: “Uwe mwenye subira kwangu mimi na mimi nitalipa kukurudishia wewe kila kitu.”

Kwa kusukumwa na sikitikio, akiwa amejawa na rehema bwana-mkubwa yule anafuta deni lile kubwa sana la mtumwa yule. Lakini mara tu anapomaliza kufanya hivyo, Yesu anaendelea kusema, mtumwa yule anaenda na kupata mtumwa mwenzake ambaye ana deni lake la dinari 100 tu (zapata dola 90). Mwanamume yule anamkaba kooni mtumwa mwenzake na kuanza kumsonga pumzi, akisema: “Lipa kurudisha chochote kile ambacho wewe una deni.”

Lakini mtumwa mwenzake huyo hana pesa zile. Kwa hiyo yeye anajiangusha kwenye nyayo za mtumwa huyo ambaye anawiwa deni naye, akiomba-omba hivi: “Uwe mwenye subira kwangu mimi na mimi nitalipa kukurudishia wewe.” Kwa kutofanana na bwana-mkubwa wake. mtumwa huyo si mwenye kujawa na rehema, naye anafanya mtumwa mwenzake atupwe ndani ya gereza.

Basi, Yesu anaendelea kusema, watumwa wale wengine ambao waliona lililokuwa limetukia wanaenda na kuambia bwana-mkubwa. Yeye, naye, anaitisha kwa kasirani kwamba mtumwa yule aletwe. “Mtumwa mwovu,” yeye anasema, “mimi nilifuta deni lile lote kwa ajili yako wewe, wakati wewe uliponinasihi mimi. Haingalikupasa wewe, nawe, kuwa na rehema juu ya mtumwa mwenzako, kama vile mimi pia nilivyokuwa nimekuwa na rehema juu yako wewe?” Akiwa amechokozeshwa kuwa na hasira-kisasi, bwana-mkubwa anamtolea mtumwa huyo asiyejawa na rehema mikononi mwa watunzajela mpaka yeye apaswe kulipa kurudisha vyote ambavyo anawiwa deni.

Ndipo Yesu anapomalizia hivi: “Kwa namna inayofanana na hiyo Baba yangu wa kimbingu atashughulika na ninyi pia ikiwa ninyi hamsamehei kila mmoja ndugu yake kutoka kwenye mioyo yenu.”

Hilo ni somo zuri kama nini la kusamehe! Kwa kulinganishwa na lile deni kubwa la dhambi ambalo Mungu ametusamehe sisi, mkiuko wo wote ambao huenda ukafanywa dhidi yetu sisi na ndugu Mkristo ni mdogo kweli kweli. Zaidi ya hilo, Yehova Mungu ametusamehe sisi maelfu ya nyakati. Mara nyingi sisi hata hatung’amui dhambi zetu dhidi yake. Kwa hiyo, je! sisi hatuwezi kusamehe ndugu yetu mara chache, hata ikiwa sisi tuna kisababishi halali cha kulalamika? Kumbuka, kama vile Yesu alivyofundisha katika yale Mahubiri ya Mlimani, Mungu ‘atatusamehe madeni yetu, kama vile sisi pia tumesamehe wadeni wetu.’ Mathayo 18:21-35; 6:12; Wakolosai 3:13, NW.

◆ Ni jambo gani linalotokeza swali la Petro juu ya kusamehe ndugu yake, na kwa sababu gani huenda yeye akafikiri dokezo lake la mara saba ni la ukarimu?

◆ Jibu la mfalme kwa jiteteo la mtumwa wake lilitofautiana jinsi gani na lile la mtumwa yule kwa jiteteo la mtumwa mwenzake?

◆ Sisi tunajifunza nini kutokana na kielezi cha Yesu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki