Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jy sura 64 uku. 152-uku. 153 fu. 2
  • Umuhimu wa Kusamehe

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Umuhimu wa Kusamehe
  • Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Habari Zinazolingana
  • Somo Juu ya Kusamehe
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Somo la Kusamehe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Kwa Nini Tuwe Wenye Kusamehe?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Mtumwa Asiyesamehe
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
jy sura 64 uku. 152-uku. 153 fu. 2
Mtumwa anamshika mtumwa mwenzake na kuanza kumkaba koo

SURA YA 64

Umuhimu wa Kusamehe

MATHAYO 18:21-35

  • JE, INATOSHA KUSAMEHE MARA SABA?

  • MFANO WA MTUMWA ASIYE NA REHEMA

Petro amesikia ushauri wa Yesu kuhusu jinsi ya kusuluhisha kutoelewana kati ya ndugu, yaani kujitahidi kusuluhisha bila kuwahusisha watu wengine. Lakini inaonekana Petro anataka kujua idadi hususa ya mara ambazo mtu anapaswa kusamehe.

Petro anauliza: “Bwana, ndugu yangu atanitendea dhambi mara ngapi nami nimsamehe? Mpaka mara saba?” Viongozi fulani wa kidini wanafundisha kwamba mtu anapaswa kusamehe hadi mara tatu. Basi huenda Petro akahisi kwamba atakuwa mkarimu sana ikiwa atamsamehe ndugu yake “mpaka mara saba.”—Mathayo 18:21.

Hata hivyo, wazo la kuweka hesabu ya mara ambazo mtu amekukosea halipatani na mafundisho ya Yesu. Basi anamrekebisha Petro: “Ninakuambia, si mpaka mara saba, bali mpaka mara 77.” (Mathayo 18:22) Kwa maneno mengine, anamaanisha hakuna mwisho. Hakuna idadi hususa ya mara ambazo Petro anapaswa kumsamehe ndugu yake.

Mfalme anafuta deni la mtumwa

Kisha Yesu anamsimulia Petro na wale wengine mfano ili kusisitiza wajibu walio nao wa kuwasamehe wengine. Unahusu mtumwa anayekataa kumwiga bwana wake mwenye rehema. Mfalme anataka kufanya hesabu na watumwa wake. Mtumwa mmoja aliye na deni kubwa la talanta 10,000 [dinari 60,000,000] analetwa kwake. Kwa kweli, hana uwezo wa kulipa deni hilo. Basi mfalme anaagiza kwamba mtumwa huyo, mke wake, na watoto wake wauzwe ili kulipia deni hilo. Anaposikia hivyo, mtumwa huyo anaanguka miguuni pa bwana wake na kumsihi: “Naomba univumilie, nitakulipa kila kitu.”—Mathayo 18:26.

Mtumwa anamfanya mtumwa mwenzake atupwe gerezani

Mfalme anamwonea huruma na kwa rehema anafuta deni kubwa la mtumwa huyo. Baada ya mfalme kufanya hivyo, mtumwa huyo anaenda na kumpata mtumwa mwenzake aliye na deni lake la dinari 100. Anamshika na kuanza kumkaba koo akisema: “Nilipe ninachokudai.” Lakini mtumwa huyo anaanguka miguuni pa mtumwa anayemdai na kumsihi: “Naomba univumilie, nami nitakulipa.” (Mathayo 18:28, 29) Hata hivyo mtumwa ambaye deni lake lilifutwa na mfalme hamwigi bwana wake. Anaagiza mtumwa mwenzake aliyekuwa na deni dogo kuliko lake atupwe gerezani hadi atakapolipa deni hilo.

The king has the unmerciful slave taken to prison

Kisha, Yesu anasimulia kwamba watumwa wengine ambao wanaona tendo hilo lisilo la rehema wanaenda na kumweleza bwana wao, ambaye kwa hasira anamwita mtumwa huyo na kumwambia: “Mtumwa mwovu, nilifuta deni lako lote uliponisihi. Je, hukupaswa pia kumwonyesha rehema mwenzako kama nilivyokuonyesha rehema?” Kisha mfalme akiwa amekasirika anamkabidhi mtumwa huyo asiye na rehema kwa walinzi wa jela hadi atakapolipa deni lote. Yesu anamalizia kwa kusema: “Baba yangu wa mbinguni atawatendea ninyi vivyo hivyo ikiwa kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni.”—Mathayo 18:32-35.

Tunajifunza somo muhimu sana kuhusu kusamehe kutokana na mfano huo! Mungu ametusamehe deni kubwa la dhambi. Makosa yoyote ambayo Mkristo mwenzetu anaweza kututendea ni madogo zaidi. Na Yehova anatusamehe si mara moja tu bali mara nyingi sana. Je, hatuwezi kumsamehe ndugu yetu mara kadhaa, hata tunapokuwa na sababu ya kulalamika? Kama Yesu alivyofundisha katika Mahubiri ya Mlimani, Mungu ‘atatusamehe madeni yetu, kama vile tunavyowasamehe wadeni wetu.’—Mathayo 6:12.

  • Ni nini kinachomfanya Petro aulize swali kuhusu kumsamehe ndugu, na kwa nini huenda akahisi kumsamehe mtu mara saba ni kuonyesha ukarimu?

  • Kuna tofauti gani kati ya jinsi mfalme anavyomtendea mtumwa ambaye anamsihi amwonyeshe rehema na jinsi mtumwa huyo anavyomtendea mtumwa mwenzake?

  • Tunajifunza somo gani kutokana na mfano aliotoa Yesu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki