Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 64
  • Somo Juu ya Kusamehe

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Somo Juu ya Kusamehe
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Somo la Kusamehe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Umuhimu wa Kusamehe
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kwa Nini Tuwe Wenye Kusamehe?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Mtumwa Asiyesamehe
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 64

Sura 64

Somo Juu ya Kusamehe

INAONEKANA bado Yesu yumo katika ile nyumba katika Kapernaumu pamoja na wanafunzi wake. Yeye amekuwa akizungumza pamoja nao jinsi ya kushughulikia magumu kati ya akina ndugu, kwa hiyo Petro anauliza: “Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atende dhambi dhidi yangu nami nimsamehe?” Kwa kuwa walimu wa kidini walio Wayahudi wananuiza jambo la kutoa msamaha kufikia mara tatu, labda Petro anafikiri ni ukarimu sana kudokeza “mpaka mara saba?”

Lakini lile wazo lote la kuweka kumbukumbu ya namna hiyo ni lenye kosa. Yesu anasahihisha Petro: “Mimi nasema kwako wewe, si, Mpaka mara saba, bali, Mpaka mara sabini na saba.” Yeye anaonyesha kwamba hakuna hadi fulani inayopasa kuwekwa juu ya hesabu ya mara ambazo Petro anapaswa kusamehe ndugu yake.

Ili kukazia juu ya wanafunzi wajibu wao wa kuwa wenye kusamehe, Yesu anawaambia kielezi. Ni juu ya mfalme mmoja ambaye anataka kumaliza hesabu pamoja na watumwa wake. Mtumwa mmoja analetwa kwake ambaye ana deni kubwa sana la dinari 60,000,000. Hakuna njia ambayo kwa vyovyote yeye anaweza kulilipa. Kwa hiyo, kama vile Yesu anavyoeleza, mfalme yule anaagiza kwamba yeye na mke wake na watoto wake wauzwe kisha malipo yafanywe.

Inapokuwa hivyo, mtumwa yule anajiangusha chini ya nyayo za bwana-mkubwa wake na kuomba sana hivi: “Uwe mwenye subira kwangu mimi nami nitalipa kukurudishia kila kitu.”

Kwa kusukumwa na sikitiko juu yake, akiwa amejawa na rehema bwana-mkubwa yule anafuta deni lile kubwa sana la mtumwa yule. Lakini mara tu anapomaliza kufanya hivyo, Yesu anaendelea kusema, mtumwa yule anaenda na kupata mtumwa mwenzake ambaye ana deni lake la dinari 100 tu. Mwanamume yule anamkaba kooni mtumwa mwenzake na kuanza kumsonga pumzi, akisema: “Lipa urudishe chochote kile ambacho wewe una deni.”

Lakini mtumwa mwenzake huyo hana pesa zile. Kwa hiyo yeye anajiangusha kwenye nyayo za mtumwa huyo ambaye anawiwa deni naye, akiomba sana hivi: “Uwe mwenye subira kwangu mimi nami nitalipa nikurudishie wewe.” Kwa kutofanana na bwana-mkubwa wake, mtumwa huyo si mwenye kujawa na rehema, naye anafanya mtumwa mwenzake atupwe ndani ya gereza.

Basi, Yesu anaendelea kusema, watumwa wale wengine ambao waliona lililokuwa limetukia wanaenda na kumwambia bwana-mkubwa. Kwa kasirani yeye anamwita yule mtumwa. “Mtumwa mwovu,” yeye anasema, “mimi nilifuta deni lile lote kwa ajili yako wewe, wakati wewe uliponisihi. Haingalikupasa wewe, nawe, kuwa na rehema juu ya mtumwa mwenzako, kama vile mimi pia nilivyokuwa nimekuwa na rehema juu yako wewe?” Akiwa amechokozeka na kuwa na hasira-kisasi, bwana-mkubwa anamkabidhi mtumwa huyo asiyejawa na rehema mikononi mwa watunza-jela mpaka yeye apaswe kulipa kurudisha vyote ambavyo anawiwa.

Ndipo Yesu anapomalizia hivi: “Kwa namna inayofanana na hiyo Baba yangu wa kimbingu atashughulika na nyinyi pia ikiwa nyinyi hamsamehei kila mmoja ndugu yake kutoka mioyoni mwenu.”

Hilo ni somo zuri kama nini la kusamehe! Kwa kulinganishwa na lile deni kubwa la dhambi ambalo Mungu ametusamehe sisi, mkiuko wowote ambao huenda ndugu yetu Mkristo akafanya ni mdogo kweli kweli. Zaidi ya hilo, Yehova Mungu ametusamehe sisi maelfu ya nyakati. Mara nyingi sisi hata hatung’amui dhambi zetu dhidi yake. Kwa hiyo, je! sisi hatuwezi kusamehe ndugu yetu mara chache, hata ikiwa sisi tuna kisababishi halali cha kulalamika? Kumbuka, kama vile Yesu alivyofundisha katika yale Mahubiri ya Mlimani, Mungu ‘atatusamehe madeni yetu, kama vile sisi pia tumesamehe wadeni wetu.’ Mathayo 18:21-35; 6:12; Wakolosai 3:13, NW.

▪ Ni jambo gani linalotokeza swali la Petro juu ya kusamehe ndugu yake, na kwa sababu gani huenda yeye akafikiri dokezo lake la kumsamehe mtu mara saba ni la ukarimu?

▪ Jibu la mfalme kwa mtumwa wake aliyejitetea aonyeshwe rehema linatofautianaje na lile la mtumwa yule kwa mtumwa mwenzake alipojitetea?

▪ Sisi tunajifunza nini kutokana na kielezi cha Yesu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki