Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 21 kur. 87-90
  • Umesamehewa Dhambi Zako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Umesamehewa Dhambi Zako
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Tunakuwa Wagonjwa?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Kwa Sababu Gani Watu Wanakuwa Wagonjwa na Kufa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Amerudi Nyumbani Katika Kapernaumu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Arudi Nyumbani Kapernaumu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 21 kur. 87-90

Sura ya 21

Umesamehewa Dhambi Zako

UNAFURAHI wakati unapofanya vizuri, sivyo?— Unajua kwamba baba na mama yako wanapendezwa, na Yehova Mungu vile vile. Lakini hata kama tujaribu sana, mara nyingine tunafanya kosa, sivyo?— Wakati tunapofanya ambayo Mungu anasema ni kosa, hii ni dhambi.

Mwalimu Mkuu, Yesu Kristo, alionyesha kwamba dhambi inatufanyia mabaya sisi sote. Alionyesha hivi wakati alipofanya mmojawapo wa miujiza yake.

Wakati huu Yesu alikuwa akikaa mjini karibu na Bahari ya Galilaya. Watu wengi wakaja kumwona huko. Watu wengi sana wakaja hata kusiwe na nafasi tena kwa wengine kuingia katika nyumba. Hakuna mwingine ambaye aliweza hata kukaribia mlango.

Lakini watu zaidi waliendelea kuja. Kikundi kimoja cha watu kilimleta mwanamume aliyekuwa mgonjwa sana. Alikuwa amepooza. Ilitaka wanaume wanne wamchukue katika kitanda kidogo, kwa sababu hakuweza kutembea.

Unajua sababu gani walitaka kumleta mgonjwa kwa Yesu?— Waliamini Yesu angeweza kumponya na ugonjwa ule.

Lakini, na watu wote hao nyumbani, wangewezaje kumfikisha mtu aliyepooza kwa Yesu?— Wanaume waliona njia. Walipanda juu ya dari. Lilikuwa dari la tambarare. Nao wakatoboa tundu. Kisha wakamtelemsha mgonjwa ka-tika kitanda chake katika tundu lile mpaka chumbani. Lo! walikuwa na imani gani!

Watu wote nyumbani walishangaa walipoona lililokuwa likitukia. Mwenye kupooza katika kitanda chake alitelemshwa mpaka kuingia chumbani. Je! Yesu alikasirika kwa sababu ya jambo ambalo wale wanaume walikuwa wamefanya?— Hata kidogo! Alifurahi kuona imani yao. Akamwambia mwenye kupooza: “Umesamehewa dhambi zako.”

Wengine kati ya watu hawakufikiri ilikuwa vizuri Yesu kusema hivyo. Hawakufikiri alikuwa na uwezo wa kusamehe dhambi. Hivyo, kuonyesha kwamba kweli alikuwa na uwezo, Yesu alimwambia yule mtu: Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.

Yesu aliposema hivyo, yule mtu alipona! Hakupooza tena. Sasa hakutaka watu wengine wamchukue. Aliweza kusimama mwenyewe na kutembea na tena kuchukua kitanda chake.

Watu walioona hili walishangaa. Katika maisha zao zote walikuwa hawajaona kabisa ajabu yo yote kama hiyo.—Marko 2:1-12.

Twajifunza nini kwa mwujiza huu?— Twajifunza kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa kusamehe dhambi na kuponya wa-gonjwa. Lakini twajifunza tena jambo jingine. Twajifunza kwamba watu wanakuwa wagonjwa kwa sababu ya dhambi.

Umepata kuwa mgonjwa?— Kwa kuwa sote twaweza kuwa wagonjwa, je! hii inamaanisha kwamba sisi sote ni wenye dhambi?— Ndiyo, Biblia inasema kwamba sote tunazaliwa katika dhambi.

Unajua maana yake nini kuzaliwa katika dhambi?— Maana yake kwamba sote tunazaliwa bila kukamilika. Sote tunafanya makosa mara nyingine hata tusipotaka. Tukawa hivi kwa sababu mwanamume na mwanamke wa kwanza, Adamu na Hawa, hawakumtii Mungu. Walifanya dhambi walipovunja sheria ya Mungu. Na sisi sote tukapata dhambi kutoka kwa Adamu.

Unajua namna tulivyopata dhambi yetu kutoka kwake?— Acha nijaribu kueleza katika njia ambayo unaweza kufahamu. Pengine umefanyiza maandazi ya matope katika kikaangio. Itakuwaje na maandazi ya matope ukibonyeza vishimo katika kikaangio? Unajua?— Alama ile ile itaonekana penye maandazi yote ya matope ambayo unafanyiza katika kikaangio hicho, sivyo?—

Adamu alikuwa kama kikaangio hicho, na sisi tuko kama maandazi ya matope. Akawa asiyekamilika alipovunja sheria ya Mungu. Ilikuwa kana kwamba alipokea kishimo au alama mbaya. Basi wakati angezaa watoto, wangefanana na nini?— Watoto wake wote wangepokea alama ii hii ya kutokukamilika.

Karibu watoto wote hawazaliwi wakiwa na kutokukamilika kukubwa uwezako kuona. Hawana mkono mpungufu, au shimo ubavuni mwao. Lakini kutokukamilika kwao ni kukubwa sana hata wanakuwa wagonjwa na, mwisho, wanakufa.

Bila shaka, watu wengine wanakuwa wagonjwa mara nyingi zaidi kuliko wengine. Sababu gani iko hivyo? Je! ni kwa sababu wanazaliwa wakiwa na dhambi zaidi?— Hapana. Bali huenda ikawa kwa sababu hawana chakula cha kutosha. Au pengine wanakula mno tamutamu na peremende. Pengine wanashinda mno usiku wasipate usingizi wa kutosha. Au pengine hawavai nguo za kujikinga na mvua au baridi.

Je! kutakuwako wakati ambapo hatutakuwa wagonjwa? Je! tutaondolewa dhambi?— Basi, Yesu alifanya nini kwa mtu yule mwenye kupooza?— Alisamehe dhambi zake, akamponya. Katika njia hii Yesu alionyesha atakalofanyia wale wote wanaojitahidi kufanya mazuri.

Tukionyesha kwamba hatupendi dhambi, kwamba tunachukia kosa, atatuponya. Ataondoa dhambi tuliyo nayo sasa. Atatufanyia hivi karibuni kwa njia ya ufalme wa Mungu.

Dhambi haitaondolewa mara moja. Hiyo itafanywa polepole. Halafu, dhambi yetu iondokapo kabisa, hatutakuwa wagonjwa tena. Sisi sote tutakuwa na afya kabisa. Lo! hiyo itakuwa baraka gani!

(Kwa mawazo zaidi yenye msaada juu ya namna dhambi inavyompata kila mtu na tuwezalo kufanya juu yake, soma Warumi 3:23; 5:12; 6:12-14, 23 na 1 Yohana 2:1.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki