Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 89
  • Yesu Anasafisha Hekalu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Anasafisha Hekalu
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Analisafisha Hekalu
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Yehova
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Yesu Ana Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Kweli
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 89
Yesu akiwafukuza watu waliokuwa wakibadili pesa kutoka hekaluni na kuzipindua meza zao

HADITHI YA 89

Yesu Anasafisha Hekalu

YESU amekasirika sana hapa, sivyo? Unajua kwa nini amekasirika hivyo? Kwa sababu watu hawa katika hekalu la Mungu katika Yerusalemu wana tamaa sana. Wanataka kupata fedha nyingi kwa watu waliokuja hapa kumwabudu Mungu.

Unawaona ng’ombe wachanga wote hao na kondoo na njiwa? Watu hao wanauza wanyama hao katika hekalu. Unajua sababu? Waisraeli wanataka sana wanyama na ndege wamtolee Mungu zawadi.

Sheria ya Mungu ilisema Mwisraeli akifanya kosa, amtolee Mungu zawadi. Nyakati nyingine, pia, iliwapasa Waisraeli watoe zawadi hizo. Lakini Mwisraeli angepata wapi ndege na wanyama wa kumtolea Mungu?

Waisraeli wengine walifuga ndege na wanyama. Hivyo wangeweza kuwatoa hao. Lakini Waisraeli wengi hawakuwa na wanyama wala ndege. Wengine walikaa mbali sana na Yerusalemu wasiweze kufikisha wanyama wao hekaluni. Basi watu walikuja hapa na kununua wanyama au ndege waliotaka. Lakini watu hawa walitaka watu walipe fedha nyingi mno. Walikuwa wakidanganya watu. Tena, hawana ruhusa ya kuuza katika hekalu la Mungu.

Ndiyo sababu Yesu amekasirika. Hivyo anapindua meza za watu wenye fedha na kutawanya fedha zao. Tena, anafanya fimbo ya kamba na kufukuza wanyama wote hekaluni. Anawaamuru watu wanaouza njiwa hivi: ‘Waondoeni humu! Acheni kufanya nyumba ya Baba yangu mahali pa biashara.’

Wafuasi wengine wa Yesu wako pamoja naye humu hekaluni katika Yerusalemu. Wanashangaa kuona Yesu akifanya hivyo. Ndipo wanakumbuka mahali ambapo Biblia inasema juu ya Mwana wa Mungu: ‘Kupenda nyumba ya Mungu kutawaka ndani yake kama moto.’

Yesu akiwa bado Yerusalemu akihudhuria Sikukuu ya Kupitwa, anafanya miujiza mingi. Kisha, Yesu anaondoka Yudea na kuanza kurudi Galilaya. Lakini njiani, anapitia wilaya ya Samaria. Na tuone yanayotokea huko.

Yohana 2:13-25; 4:3, 4.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki