Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 76 uku. 180-uku. 181 fu. 2
  • Yesu Analisafisha Hekalu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Analisafisha Hekalu
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Anasafisha Hekalu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Yesu Ana Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Kweli
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Yehova
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Bidii kwa Ajili ya Ibada ya Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 76 uku. 180-uku. 181 fu. 2
Yesu akitumia mjeledi kuwafukuza wanyama nje ya hekalu na kupindua meza za wanaobadili pesa

SOMO LA 76

Yesu Analisafisha Hekalu

Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 30 W.K., Yesu alienda Yerusalemu. Watu wengi walienda jijini humo ili kusherehekea Pasaka. Sherehe hiyo ilitia ndani kutoa dhabihu za wanyama hekaluni. Watu fulani walikuja na wanyama wao, lakini wengine waliwanunua huko Yerusalemu.

Yesu alipoenda hekaluni, aliwaona watu wakiuza wanyama ndani ya hekalu. Walikuwa wakijipatia pesa ndani ya nyumba ya ibada ya Yehova! Yesu alitendaje? Alitengeneza mjeledi wa kamba naye akawafukuza kondoo na ng’ombe kutoka hekaluni. Akapindua meza za watu waliokuwa wakibadili pesa na kumwaga sarafu zao chini. Yesu akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa: ‘Ondoeni vitu hivi hapa! Acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara!’

Watu waliokuwa hekaluni walishangazwa na jambo ambalo Yesu alifanya. Wanafunzi wake wakakumbuka unabii huu uliomhusu Masihi: ‘Nitakuwa na bidii nyingi kwa ajili ya nyumba ya Yehova.’

Baadaye, katika mwaka wa 33 W.K., Yesu alisafisha hekalu kwa mara ya pili. Hangemruhusu mtu yeyote aishushie heshima nyumba ya Baba yake.

“Hamwezi kuwa watumwa wa Mungu na wa Utajiri.”—Luka 16:13

Maswali: Yesu alifanya nini alipoona watu wakiuza wanyama hekaluni? Kwa nini Yesu alifanya hivyo?

Mathayo 21:12, 13; Marko 11:15-17; Luka 19:45, 46; Yohana 2:13-17; Zaburi 69:9

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki