Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 90
  • Pamoja na Mwanamke Penye Kisima

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pamoja na Mwanamke Penye Kisima
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Mwanamke Kisimani
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Kufundisha Mwanamke Msamaria
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Amfundisha Mwanamke Msamaria
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kufundisha Mwanamke Msamaria
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 90
Yesu anaongea na mwanamke Msamaria penye kisima

HADITHI YA 90

Pamoja na Mwanamke Penye Kisima

YESU amekaa akipumzika karibu na kisima Samaria. Wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. Mwanamke anayesema na Yesu amekuja kuteka maji. Yesu amwambia: ‘Nipe maji ninywe.’

Mwanamke anashangaa sana kusikia hivyo. Unajua sababu? Yesu ni Myahudi, na mwanamke ni Msamaria. Na Wayahudi wengi hawapendi Wasamaria. Hawataki hata kusema nao! Lakini Yesu anapenda watu wa namna zote. Amwambia mwanamke hivi: ‘Wewe ukimjua anayekuomba maji, ungemwomba akupe maji yanayotoa uzima.’

‘Bwana,’ mwanamke asema, ‘kisima ni kirefu, na huna ndoo. Utapata wapi maji hayo yanayotoa uzima?’

‘Ukinywa maji ya kisima hiki utaona kiu tena,’ Yesu amweleza. ‘Lakini maji nitakayotoa yanaweza kumfanya mtu aishi milele.’

‘Bwana,’ mwanamke asema, ‘nipe maji hayo! Nisione kiu tena. Nisije tena huku kuteka maji.’

Mwanamke huyo anadhani Yesu anasema maji halisi. Lakini anasema juu ya kweli ya Mungu na ufalme wake. Kweli hiyo ni kama maji yanayotoa uzima. Inaweza kumpa mtu uzima wa milele.

Sasa Yesu anamwambia mwanamke hivi: ‘Nenda kamwite mume wako urudi.’

‘Sina mume,’ anajibu.

‘Umejibu sawa,’ Yesu asema. ‘Lakini umekuwa na waume watano, na yule uliye naye sasa si mume wako.’

Yule mwanamke astaajabu, kwa sababu yote hayo ni kweli. Yesu alijuaje hayo? Ni kwa vile Yesu Ndiye aliyeahidiwa akatumwa na Mungu, naye Mungu anamjulisha hayo. Wakati huo wanafunzi wa Yesu wanarudi, nao wanashangaa kumwona akizungumza na mwanamke Msamaria.

Twajifunza nini kwa hayo? Kwamba Yesu anapenda watu wa mataifa yote. Sisi pia tuwe hivyo. Tusidhani watu wengine ni wabaya kwa sababu ni wa taifa fulani. Yesu anataka watu wote waijue kweli inayoongoza kwenye uzima. Na sisi pia yatupasa tuwe na nia ya kusaidia watu wajifunze kweli.

Yohana 4:5-43; 17:3.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki