Wimbo 22
Kutii Ujumbe wa Yuda
(Yuda 21)
1. Onyo lake Yuda
lagusa moyo sana.
Ni kwa faida yetu
Na tusianguke.
Mashauri hayo mema.
Yanatutia nguvu.
Yatatuhifadhi imani.
2. Na maonyo makali
yanatufaidi.
Shetani hataki
tutii maagizo
Ya Mungu, na kwa usemi
wa udanganyifu,
anajaribu kutuangusha!
3. Japo vishawishi
Vya waovu vya hila.
Tubaki kwake Mungu,
Tushikane naye.
Ujumbe wa Yuda bora,
unatuweka chonjo!
Twepuke uasi imani.
4. Pigania imani
na uwe shujaa.
Rehema na amani,
Upendo uzidi.
Kwake Yehova, Mwokozi,
Kwa Yesu Bwana wetu,
Na tuheshimiane sote.