Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 18
  • Yohana Apungua, Yesu Azidi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yohana Apungua, Yesu Azidi
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Yohana Anapungua, Yesu Anazidi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Yesu Aongezeka Naye Yohana Apungua
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Je! Yohana Alikosa Imani?
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Je! Yohana Alikuwa na Ukosefu wa Imani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 18

Sura 18

Yohana Apungua, Yesu Azidi

BAADA ya Sikukuu ya Kupitwa katika masika ya 30 W.K., Yesu na wanafunzi wake waondoka Yerusalemu. Lakini, hawarudi kwao Galilaya bali waingia nchi ya Yudea, ambako wabatiza watu. Yohana Mbatizaji amekuwa akifanya kazi iyo hiyo kwa muda wa mwaka mmoja sasa, na bado ana wanafunzi wanaoshirikiana naye.

Kwa kweli, Yesu mwenyewe habatizi watu, bali wanafunzi wake ndio wanaofanya hivyo kwa mwelekezo wake. Ubatizo wafanyao una maana moja na ule ufanywao na Yohana, kwa kuwa ni ufananisho wa toba ya Myahudi juu ya dhambi zake dhidi ya agano la Sheria la Mungu. Hata hivyo, baada ya ufufuo wake, Yesu awaagiza wanafunzi wake wafanye ubatizo ambao una maana tofauti. Ubatizo wa Kikristo leo ni ufananisho wa wakfu wa mtu atumikie Yehova Mungu.

Hata hivyo, hapo mapema mwanzoni mwa huduma ya Yesu, wote wawili Yohana na yeye, ingawa wafanya kazi wakiwa mbalimbali, wafundisha na kubatiza wenye kutubu. Lakini wanafunzi wa Yohana waona wivu na kumpelekea malalamiko juu ya Yesu: “Rabi, . . . tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea.”

Badala ya kuwa mwenye wivu, Yohana ashangilia mafanikio ya Yesu na pia ataka wanafunzi wake washangilie. Awakumbusha hivi: “Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake.” Halafu atumia kielezi kizuri sana: “Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. Basi hii furaha yangu imetimia.”

Yohana, akiwa ndiye rafiki ya Bwana-arusi, alishangilia karibu miezi sita kabla ya hapo wakati alipojulisha wanafunzi wake kwa Yesu. Baadhi yao wakawa wenye kutazamiwa kuwa washiriki wa jamii ya bibi-arusi wa kimbingu wa Kristo ambayo wanayoishiriki ni Wnakristo wapakwa-mafuta kwa roho. Yohana awataka wanafunzi wake wa sasa pia wamfuate Yesu, kwa kuwa kusudi lake ni kutayarisha njia ili huduma ya Kristo ipate mafanikio. Ni kama vile Yohana Mbatizaji aelezavyo: “Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.”

Yohana, mwanafunzi mpya wa Yesu, ambaye mapema kidogo alikuwa pia mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji, aandika kuhusu asili ya Yesu na fungu Lake la maana katika wokovu wa binadamu, akisema: “Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. . . . Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake. Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.”

Muda usio mrefu baada ya Yohana Mbatizaji kuzungumza juu ya kupungua kwa utendaji wake, yeye akamatwa na Mfalme Herode. Herode amemchukua Herodia, mke wa Filipo ndugu yake, awe mke wake mwenyewe, na wakati Yohana afunuapo wazi mbele ya watu wote kwamba vitendo vyake havifai, Herode aagiza afungwe gerezani. Yesu apatapo habari za kukamatwa kwa Yohana, aondoka Yudea kwenda Galilaya akiwa pamoja na wanafunzi wake. Yohana 3:22-4:3; Matendo 19:4; Mathayo 28:19; 2 Wakorintho 11:2; Marko 1:14; 6:17-20.

▪ Ni nini maana ya mabatizo yaliyofanywa kwa mwelekezo wa Yesu kabla ya ufufuo wake? Na baada ya ufufuo wake?

▪ Yohana aonyeshaje kwamba lalamiko la wanafunzi wake halifai?

▪ Kwa nini Yohana afungwa gerezani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki