Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 28
  • Aulizwa Maswali Juu ya kufunga

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Aulizwa Maswali Juu ya kufunga
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Aulizwa Maulizo Juu ya Kufunga
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Kwa Nini Wanafunzi wa Yesu Hawafungi?
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Je, Kufunga Ni Njia ya Kumkaribia Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 28

Sura 28

Aulizwa Maswali Juu ya kufunga

KARIBU mwaka mmoja umepita tangu Yesu ahudhurie Sikukuu ya Kupitwa ya 30 W.K. Kufikia sasa, Yohana Mbatizaji amekuwa gerezani kwa miezi kadhaa. Ingawa yeye alitaka wanafunzi wake wawe wafuasi wa Kristo, si wote wamekuwa hivyo.

Sasa baadhi ya wanafunzi hao wa Yohana aliyetiwa gerezani wanamjia Yesu na kuuliza: “Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi?” Mafarisayo wanazoea kufunga mara mbili kwa juma, hiyo ikiwa ni desturi ya dini yao. Na labda wanafunzi wa Yohana wanafuata kawaida inayofanana na hiyo. Huenda pia ikawa kwamba wanafunga ili kuomboleza kufungwa kwa Yohana na wanashangaa ni kwa nini wanafunzi wa Yesu hawajiungi nao katika wonyesho huo wa huzuni.

Kwa kujibu Yesu aeleza: “Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.”

Wanafunzi wa Yohana wapaswa kukumbuka kwamba Yohana mwenyewe alimtaja Yesu kuwa ndiye Bwana-arusi. Kwa hiyo, Yesu akiwa angali yupo, Yohana hangeona inafaa kufunga, wala wanafunzi wa Yesu hawaoni inafaa kufanya hivyo. Baadaye, Yesu afapo, wanafunzi wake wanaomboleza na kufunga. Lakini anapofufuliwa na kupaa mbinguni, hawana tena sababu ya kufunga kwa kuomboleza.

Ndipo Yesu atoa vielezi hivi: “Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi. Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya.” Vielezi hivi vinahusianaje na kufunga?

Yesu alikuwa akisaidia wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wathamini kwamba hakuna mtu aliyepaswa kutazamia wafuasi wake wajipatanishe na mazoea yale ya kale ya dini ya Wayahudi, kama vile kufunga kidesturi. Yeye hakuja kutia viraka wala kuendeleza mifumo ya kale ya ibada iliyochakaa iliyokuwa tayari kuondolewa mbali. Ukristo haungelazimishwa ujipatanishe na dini ya Wayahudi wa siku hizo pamoja na mapokeo yayo ya wanadamu. Hapana, haingekuwa kama kiraka kipya katika vazi kuukuu au kama divai mpya katika kiriba kikuukuu. Mathayo 9:14-17; Marko 2:18-22; Luka 5:33-39; Yohana 3:27-29.

▪ Ni nani wanaozoea kufunga, na kwa kusudi gani?

▪ Kwa nini wanafunzi wa Yesu hawafungi wakati anapokuwa nao, na baadaye sababu ya kufunga itatowekaje upesi

▪ Yesu atoa vielezi gani, navyo vyamaanisha nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki