Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 6/1 kur. 8-9
  • Aulizwa Maulizo Juu ya Kufunga

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Aulizwa Maulizo Juu ya Kufunga
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Aulizwa Maswali Juu ya kufunga
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Kwa Nini Wanafunzi wa Yesu Hawafungi?
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Je, Kufunga Ni Njia ya Kumkaribia Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 6/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Aulizwa Maulizo Juu ya Kufunga

KARIBU mwaka mmoja umepita tangu Yesu alipohudhuria Sikukuu ya Kupitwa mwaka 30 W.K. Kufikia sasa, Yohana Mbatizaji amekuwa gerezani kwa miezi kadha. Ingawa yeye alitaka wanafunzi wake wawe wafuasi wa Kristo, si wote wamekuwa hivyo.

Sasa baadhi ya wanafunzi hao wa Yohana aliyetiwa gerezani wanamjia Yesu na kuuliza: “Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi? ” Mafarisayo wanazoea kufunga mara mbili kwa juma, hiyo ikiwa desturi ya dini yao. Na labda wanafunzi wa Yohana wanafuata kawaida inayofanana na hiyo. Huenda pia ikawa kwamba wanafunga ili kuomboleza kufungwa kwa Yohana na wanashangaa ni kwa nini wanafunzi wa Yesu hawajiungi nao katika wonyesho huo wa huzuni.

Kwa kujibu Yesu anaeleza hivi: “Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.”

Wanafunzi wa Yohana wanapaswa kukumbuka kwamba Yohana mwenyewe alimtaja Yesu kuwa ndiye Bwana-arusi. Kwa hiyo, Yesu akiwa angali yupo, Yohana hangeona inafaa kufunga, wala wanafunzi wa Yesu hawaoni inafaa kufanya hivyo. Baadaye, Yesu anapokufa, wanafunzi wake wanaomboleza na kufunga. Lakini anapofufuliwa na kupaa mbinguni, hawana tena sababu ya kufunga kwa kuomboleza.

Ndipo Yesu anapoeleza mifano hii: “Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi. Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya.” Mifano hii inahusianaje na kufunga?

Yesu alikuwa akisaidia wanafunzi wa Yohana wathamini kwamba hakuna mtu aliyepaswa kutazamia wafuasi wake wajipatanishe na mazoea yale ya kale ya dini ya Wayahudi, kama vile kufunga kidesturi. Yeye hakuja kutia viraka wala kuendeleza mifumo ya kale ya ibada iliyochakaa iliyokuwa tayari kuondolewa mbali. Ukristo haungelazimishwa ujipatanishe na dini ya Wayahudi wa siku hizo pamoja na mapokeo ya wanadamu yaliyokuwamo. Hapana, haingefanywa iwe kama kiraka kipya katika vazi kuukuu au kama divai mpya katika kiriba kikuukuu. Mathayo 9:14-17; Marko 2:18-22; Luka 5:33-39; Yohana 3:27-29.

◆ Ni nani waliozoea kufunga, na kwa kusudi gani?

◆ Kwa sababu gani wanafunzi wa Yesu hawakufunga alipokuwa pamoja nao, na ni jinsi gani baadaye sababu ya kufunga ilivyomalizika upesi?

◆ Yesu alieleza mifano gani, nayo inamaanisha nini?

[Picha ya ukurasa nzima katika ukurasa wa 8]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki