Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jy sura 28 uku. 70-uku. 71 fu. 6
  • Kwa Nini Wanafunzi wa Yesu Hawafungi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Wanafunzi wa Yesu Hawafungi?
  • Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Habari Zinazolingana
  • Aulizwa Maswali Juu ya kufunga
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Aulizwa Maulizo Juu ya Kufunga
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Je, Kufunga Ni Njia ya Kumkaribia Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
jy sura 28 uku. 70-uku. 71 fu. 6
Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wamuuliza Yesu kuhusu kufunga

SURA YA 28

Kwa Nini Wanafunzi wa Yesu Hawafungi?

MATHAYO 9:14-17 MARKO 2:18-22 LUKA 5:33-39

  • WANAFUNZI WA YOHANA WAMUULIZA YESU KUHUSU KUFUNGA

Yohana Mbatizaji amekuwa gerezani kwa kipindi fulani baada ya Yesu kuhudhuria Pasaka ya mwaka wa 30 W.K. Yohana alitaka wanafunzi wake wawe wafuasi wa Yesu, lakini si wote wanaofanya hivyo miezi inayofuata baada ya Yohana kufungwa gerezani.

Sasa, Pasaka ya mwaka wa 31 W.K. inapokaribia, baadhi ya wanafunzi wa Yohana wanamjia Yesu na kuuliza: “Kwa nini sisi na Mafarisayo hufunga lakini wanafunzi wako hawafungi?” (Mathayo 9:14) Mafarisayo hufunga kwa kuwa ni desturi yao ya kidini. Baadaye, hata Yesu anatumia mfano wa Farisayo anayejiona mwadilifu na kusali hivi: “Ee Mungu, ninakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine . . . Mimi hufunga mara mbili kwa juma.” (Luka 18:11, 12) Labda pia wanafunzi wa Yohana walikuwa na desturi ya kufunga. Au huenda walikuwa wakifunga ili kuombolezea kifungo cha Yohana gerezani. Wengine pia wanashangaa kwa nini wanafunzi wa Yesu hawafungi, labda ili kuonyesha kwamba wao pia wanahuzunishwa na mambo ambayo Yohana ametendewa.

Yesu anawajibu kwa kutumia mfano: “Rafiki za bwana harusi hawahitaji kuomboleza bwana harusi anapokuwa pamoja nao, sivyo? Lakini siku zitakuja ambapo bwana harusi ataondolewa kwao, ndipo watakapofunga.”—Mathayo 9:15.

Yohana mwenyewe alimtaja Yesu kuwa bwana harusi. (Yohana 3:28, 29) Kwa hiyo, Yesu akiwapo wanafunzi wake hawahitaji kufunga. Baadaye, Yesu atakapokufa, wanafunzi wake wataomboleza na hawatakuwa na hamu ya kula. Hata hivyo, mambo yatabadilika sana atakapofufuliwa! Wakati huo hawatakuwa na sababu ya kuomboleza na kufunga.

Kisha, Yesu anawapa mifano hii miwili: “Hakuna mtu anayeshona kiraka cha kitambaa kipya juu ya vazi la nje la zamani; kwa maana hicho kitambaa kipya kitatoka kwenye hilo vazi nalo litararuka vibaya zaidi. Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vya divai vilivyochakaa. Wakifanya hivyo, viriba hivyo vitapasuka na divai itamwagika navyo viriba vitaharibika. Lakini watu huweka divai mpya katika viriba vipya vya divai.” (Mathayo 9:16, 17) Yesu anamaanisha nini?

Yesu anawasaidia wanafunzi wa Yohana Mbatizaji waelewe kwamba mtu yeyote asitarajie kwamba wafuasi wa Yesu watafuata desturi za zamani za Kiyahudi, kama vile desturi ya kufunga. Hakuja kuweka viraka na kuendeleza mfumo wa zamani wa ibada uliochakaa, uliokuwa karibu kutupiliwa mbali. Ibada ambayo Yesu anapendekeza si ile inayofuata dini ya Kiyahudi ya wakati huo na desturi zake za wanadamu. Hapana, Yesu hajaribu kuweka kitambaa kipya juu ya vazi la zamani au divai mpya kwenye kiriba cha zamani kilichokauka.

MIFANO KUHUSU KUFUNGA

Chombo cha ngozi

Yesu alitumia mfano ambao wasikilizaji wengi wangeelewa kwa urahisi—kushona. Ikiwa mtu angeshona kitambaa kipya, ambacho hakijachakaa juu ya vazi lilotumika au la zamani, ni nini ambacho kingetokea? Ikiwa vazi hilo lingefuliwa, kitambaa kipya kingejikunja na kutoka kwenye nguo ya zamani, na hivyo kuirarua.

Pia, wakati mwingine divai iliwekwa katika vyombo vilivyotengenezwa kwa ngozi ya wanyama. Baada ya muda mrefu, ngozi ingekauka na kupoteza uwezo wake wa kutanuka. Ingekuwa hatari kuweka divai mpya katika chombo kama hicho. Divai mpya inaweza kuendelea kuumuka na kusababisha shinikizo. Hilo linaweza kupasua ngozi hiyo iliyochakaa na kukauka.

  • Katika siku za Yesu, ni nani waliokuwa na zoea la kufunga, na kwa nini?

  • Kwa nini wanafunzi wa Yesu hawafungi Yesu akiwa pamoja nao, hata hivyo ni nini kinachoweza kufanya wafunge baadaye?

  • Mifano ambayo Yesu anatoa kuhusu kitambaa kipya na divai mpya inamaanisha nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki