Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 54
  • “Mkate wa Kweli Kutoka Mbinguni”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Mkate wa Kweli Kutoka Mbinguni”
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu “Mkate wa Kweli Kutoka Mbinguni”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Yesu​—“Mkate wa Uzima”
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Je, Umeonja Mkate wa Uzima?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • “Mkate wa Uzima” Upo kwa Watu Wote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 54

Sura 54

“Mkate wa Kweli Kutoka Mbinguni”

SIKU iliyotangulia ilikuwa imekuwa yenye matukio kweli kweli. Yesu alilisha kimuujiza maelfu ya watu na kisha akaepa jaribio la watu la kumfanya mfalme. Usiku huo yeye alitembea akikanyaga kwa miguu Bahari ya Galilaya yenye dhoruba; akaokoa Petro, aliyeanza kuzama wakati alipotembea juu ya maji yenye kusukwasukwa na dhoruba; na akayatuliza mawimbi ili kuokoa wanafunzi wake wasivunjikiwe merikebu.

Sasa wale watu ambao Yesu alikuwa amelisha kimuujiza kaskazini-mashariki mwa Bahari ya Galilaya wanampata karibu na Kapernaumu na kuuliza: “Ulifika hapa lini?” Akiwakemea, Yesu anasema kwamba wao wamekuja wakimtafuta kwa sababu tu wanatazamia kupata mlo mwingine wa bure. Yeye anawahimiza wafanyie kazi, si chakula ambacho kinaharibika, bali chakula ambacho kinabaki kwa ajili ya uhai wa milele. Kwa hiyo watu hao wanauliza: “Tutafanya nini ili kuzifanya kazi za Mungu?”

Yesu anataja kazi moja tu iliyo ya thamani kubwa zaidi. “Hii ndiyo kazi ya Mungu,” yeye anaeleza, “kwamba nyinyi mjizoeze imani katika yeye ambaye Huyo alituma.”

Hata hivyo, watu hao hawajizoezi imani katika Yesu, ijapokuwa miujiza yote ambayo yeye amefanya. Jambo lisilosadikika ni kwamba, hata baada ya maajabu yote ambayo yeye amefanya, wao wanauliza hivi: “Basi, wewe utafanya nini kama ishara, ili sisi tuone na kukuamini? Ni kazi gani ambayo wewe utafanya? Baba zetu watangulizi waliila mana jangwani, sawasawa na vile imeandikwa, ‘Yeye aliwapa mkate kutoka mbinguni wale.’”

Katika kujibu ombi lao la ishara, Yesu anaeleza wazi Chanzo chenyewe cha maandalizi ya kimuujiza, akisema: “Musa hakuwapa nyinyi mkate kutoka mbinguni, bali Baba yangu awapa nyinyi ule mkate wa kweli kutoka mbinguni. Kwa maana mkate wa Mungu ni yule ambaye anakuja chini kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uhai.”

“Bwana,” wale watu wasema, “utupe sisi mkate huo sikuzote.”

“Mimi ndimi ule mkate wa uhai,” Yesu anaeleza. “Yeye ambaye anakuja kwangu hatapata njaa hata kidogo, na yeye ambaye anajizoeza imani katika mimi hatapata kamwe kiu hata kidogo. Lakini mimi nasema kwenu nyinyi, Nyinyi hata mmeniona, na bado hamwamini. Kila kitu ambacho Baba ananipa kitakuja kwangu, na yule ambaye anakuja kwangu sitamfukuzia mbali kwa vyovyote; kwa sababu mimi nimekuja chini kutoka mbinguni kufanya si mapenzi yangu mimi, bali mapenzi ya huyo ambaye alinituma. Haya ndiyo mapenzi ya huyo ambaye alinituma, kwamba mimi nisipoteze kitu chochote kati ya vyote ambavyo yeye amenipa bali kwamba nikifufue katika ile siku ya mwisho. Kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu, kwamba kila mtu ambaye anaangalia huyo Mwana na kujizoeza imani katika huyo apate kuwa na uhai wa milele.”

Kusikia hivyo wale Wayahudi wanaanza kunung’unikia Yesu kwa sababu yeye alisema, “Mimi ndimi ule mkate ambao ulikuja chini kutoka mbinguni.” Wao hawaoni katika yeye kitu kilicho zaidi ya yeye kuwa mwana wa wazazi wa kibinadamu kwa hiyo kama walivyofanya watu wa Nazareti, wao wanakataa, wakisema: “Je! huyu si Yesu yule mwana wa Yusufu, ambaye baba na mama yake sisi tunajua? Inakuwaje kwamba sasa yeye anasema, ‘Mimi nimekuja chini kutoka mbinguni’?”

“Acheni kunung’unika miongoni mwenu wenyewe,” Yesu anajibu. “Hakuna mtu anayeweza kuja kwangu mimi isipokuwa Baba, ambaye alinituma, anamvuta huyo; nami nitamfufua katika ile siku ya mwisho. Imeandikwa katika wale Manabii, ‘Na wote watafundishwa na Yehova.’ Kila mmoja ambaye amesikia kutoka kwa Baba na amejifunza anakuja kwangu mimi. Si kwamba mtu yeyote ameona Baba, ila yeye ambaye ametoka kwa Mungu; mmoja huyo ameona Baba. Kweli kweli kabisa mimi nasema kwenu nyinyi, Yeye ambaye anaamini ana uhai wa milele.”

Akiendelea, Yesu anarudia: “Mimi ndimi ule mkate wa uhai. Baba zenu watangulizi waliila mana katika lile jangwa na bado wakafa. Huu ndio ule mkate ambao unakuja chini kutoka mbinguni, ili kwamba mtu yeyote apate kula sehemu yao naye asife. Mimi ndimi ule mkate unaoishi ambao ulikuja chini kutoka mbinguni; ikiwa mtu yeyote anakula sehemu ya mkate huo yeye ataishi milele.” Ndiyo, kwa kujizoeza imani katika Yesu, yeye huyo ambaye Mungu alituma, watu wanaweza kuwa na uhai wa milele. Hakuna mana, au mkate mwingine wowote, unaoweza kuandaa hilo!

Mazungumzo hayo yanayohusu ule mkate kutoka mbinguni yanaonekana yalianza muda mfupi baada ya watu hao kupata Yesu karibu na Kapernaumu. Lakini yaendelea, yakifikia upeo baadaye, wakati Yesu anapokuwa akifundisha katika sinagogi katika Kapernaumu. Yohana 6:25-51, 59; Zaburi 78:24; Isaya 54:13; Mathayo 13:55-57, NW.

▪ Ni matukio gani yaliyotangulia mazungumzo ya Yesu kuhusu ule mkate kutoka mbinguni?

▪ Kwa sababu ya mambo ambayo Yesu amefanya sasa hivi, kwa nini lile ombi la ishara halifai kabisa?

▪ Kwa nini Wayahudi wananung’unikia dai la Yesu kwamba yeye ndiye ule mkate wa kweli kutoka mbinguni?

▪ Yale mazungumzo juu ya ule mkate kutoka mbinguni yalitukia wapi?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki