Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 10/1 kur. 8-9
  • Yesu “Mkate wa Kweli Kutoka Mbinguni”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu “Mkate wa Kweli Kutoka Mbinguni”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Habari Zinazolingana
  • “Mkate wa Kweli Kutoka Mbinguni”
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Yesu​—“Mkate wa Uzima”
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Je, Umeonja Mkate wa Uzima?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • “Mkate wa Uzima” Upo kwa Watu Wote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 10/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Yesu “Mkate wa Kweli Kutoka Mbinguni”

SIKU ilikuwa imekuwa yenye matukio kweli kweli. Yesu alilisha kimwujiza maelfu ya watu na kisha akaepa jaribio la watu la kumfanya mfalme. Usiku huo yeye alitembea akikanyaga kwa miguu bahari ya Galilaya yenye dhoruba; akaokoa Petro, aliyeanza kuzama wakati alipotembea juu ya maji yenye kusukwasukwa na dhoruba; na akayatuliza mawimbi ili kuokoa wanafunzi wake wasivunjikiwe merikebu.

Siku iliyofuata watu ambao Yesu alikuwa amelisha kimwujiza kaskazini mashariki mwa bahari ya Galilaya wanampata karibu na Kapernaumu. Akiwakemea wao, Yesu anasema kwamba wao wamekuja wakimtafuta yeye kwa sababu wanatazamia mlo mwingine wa bure. Yeye anawahimiza wafanye kazi, si kwa ajili ya chakula ambacho kinapotea, bali kwa ajili ya chakula ambacho kinabaki kwa uzima wa milele. Kwa hiyo watu hao wanauliza: “Tutafanya nini sisi kuzifanya kazi za Mungu?”

Yesu anataja jina la kazi moja tu iliyo ya thamani kubwa zaidi. “Hii ndiyo kazi ya Mungu,” yeye anaeleza, “kwamba ninyi mjizoeze imani katika yeye ambaye Mmoja huyo alimtuma.”

Hata hivyo, watu hao hawajizoezi imani katika Yesu, ijapokuwa miujiza yote ambayo yeye amefanya. Siku iliyokuwa kabla ya hii, yeye alilisha kimwujiza wanaume 5,000, na pia wanawake na watoto, na hata hivyo sasa, kwa njia isiyoweza kuaminika, wao wanauliza hivi: “Basi, ni nini ambalo wewe utafanya kama ishara, ili sisi tulione na kukuamini wewe? Ni kazi gani ambayo wewe utafanya? Baba zetu wa kwanza waliila mana katika lile jangwa, sawasawa na vile imeandikwa, ‘Yeye aliwapa wao mkate kutoka mbinguni wale.’”

Katika kujibu ombi lao la ishara, Yesu anaelewesha wazi Chanzo cha maandalizi ya kimwujiza, akisema; “Musa hakuwapa ninyi ule mkate kutoka mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi ule mkate wa kweli kutoka mbinguni. Kwa maana mkate wa Mungu ndiye mmoja ambaye anakuja chini kutoka mbinguni na kupa uzima kwa ulimwengu.”

“Bwana,” watu wale wanasema, “sikuzote tupe sisi mkate huo.”

“Mimi ndimi ule mkate wa uzima,” Yesu anaeleza. “Yeye ambaye anakuja kwangu mimi hatapata njaa hata kidogo, na yeye ambaye anajizoeza imani katika mimi hatapata kamwe kiu hata kidogo. Lakini mimi nasema kwenu ninyi, Ninyi hata mmeniona mimi, bado hamwamini. Kila kitu Baba anachonipa mimi kitakuja kwangu mimi, na mmoja ambaye anakuja kwangu mimi sitamfukuzia mbali kwa vyo vyote; kwa sababu mimi nimekuja chini kutoka mbinguni kufanya, si mapenzi yangu mimi, bali mapenzi ya huyo ambaye alinituma mimi. Haya ndiyo mapenzi ya huyo ambaye alinituma mimi, kwamba mimi nisipaswe kupoteza kitu cho chote kati ya vyote ambavyo yeye amenipa mimi bali kwamba nipaswe kukifufua kwenye ile siku ya mwisho. Kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu, kwamba kila mtu ambaye anaangalia yule Mwana na kujizoeza imani katika huyo apaswe kuwa na uzima wa milele.”

Kwa jambo hilo, Wayahudi hao wanaanza kunung’unikia Yesu kwa sababu yeye alisema, “Mimi ndimi ule mkate ambao ulikuja chini kutoka mbinguni.” Wao hawaoni kitu cho chote katika yeye isipokuwa mwana wa wazazi wa kibinadamu kwa hiyo wanakataa kwa njia ile ile kama walivyofanya watu wa Nazareti: “Je! huyu si Yesu yule mwana wa Yusufu, ambaye baba na mama yake sisi tunajua? Ni jinsi gani kwamba sasa yeye anasema, ‘Mimi nimekuja chini kutoka mbinguni’?”

“Acheni kunung’unika miongoni mwenu wenyewe,” Yesu anajibu. “Hakuna mtu anayeweza kuja kwangu mimi isipokuwa Baba, ambaye alinituma mimi, anamvuta huyo; na mimi nitafufua huyo katika ile siku ya mwisho. Imeandikwa katika wale Manabii, ‘na hao watafundishwa wote na Yehova.’ Kila mmoja ambaye amesikia kutoka kwa Baba na amejifunza anakuja kwangu mimi. Si kwamba mtu ye yote ameona Baba, ila yeye ambaye ametoka kwa Mungu; mmoja huyo ameona Baba. Kwa kweli zaidi sana mimi nasema kwenu ninyi, Yeye ambaye anaamini ana uzima wa milele.”

Akiendelea, Yesu anarudia “Mimi ndimi ule mkate wa uzima. Baba zenu wa kwanza waliila mana katika lile jangwa na bado walikufa. Huu ndio ule mkate ambao unakuja chini kutoka mbinguni, ili kwamba mtu ye yote apate kula sehemu ya huo na asife. Mimi ndimi ule mkate unaoishi ambao ulikuja chini kutoka mbinguni; ikiwa mtu ye yote anakula sehemu ya mkate huu yeye ataishi milele.” Ndiyo, kwa kujizoeza imani katika Yesu, mmoja huyo ambaye Mungu alituma, watu wanaweza kuwa na uzima wa milele. Hakuna mana, au mkate mwingine wo wote kama huo, unaoweza kuandaa hilo!

Mazungumzo yale yanahusu ule mkate kutoka mbinguni yanaonekana yalianza muda mfupi baada ya watu hao kupata Yesu karibu na Kapernaumu. Lakini yaliendelea, yakifikia upeo baadaye, wakati Yesu alipokuwa akifundisha katika sinagogi katika Kapernaumu. Yohana 6:26-51, 59; Zaburi 78:24; Isaya 54:13; Mathayo 13:55-57, NW.

◆ Ni matukio gani yaliyotangulia mazungumzo ya Yesu kuhusu ule mkate kutoka mbinguni?

◆ Kwa sababu ya mambo ambayo Yesu amefanya sasa hivi tu, kwa sababu gani lile ombi la ishara ni lisilofaa sana?

◆ Kwa sababu gani Wayahudi wananung’unikia dai la Yesu kwamba yeye ndiye ule mkate wa kweli kutoka mbinguni?

◆ Yale mazungumzo juu ya ule mkate kutoka mbinguni yalitukia wapi?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki