Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 55
  • Wanafunzi Wengi Waacha Kufuata Yesu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wanafunzi Wengi Waacha Kufuata Yesu
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Wanafunzi Wengi Waacha Kufuata Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Maneno ya Yesu Yawashtua Wengi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • “Nitamfufua Katika Siku ya Mwisho”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • “Mkate wa Uzima” Upo kwa Watu Wote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 55

Sura 55

Wanafunzi Wengi Waacha Kufuata Yesu

YESU anafundisha katika sinagogi moja katika Kapernaumu kuhusu fungu lake akiwa ule mkate wa kweli kutoka mbinguni. Hotuba yake kwa wazi ni mpanuo wa mazungumzo ambayo yalianza na wale watu wakati walipomkuta waliporudi kutoka upande wa mashariki wa Bahari ya Galilaya, ambako walikuwa wamekula kutokana na mikate na samaki walioandaliwa kimuujiza.

Yesu anaendeleza maneno yake, akisema: “Ule mkate ambao mimi nitatoa ni mnofu wangu kwa ajili ya uhai wa ulimwengu.” Miaka miwili tu kabla ya hapo, katika masika ya 30 W.K., Yesu aliambia Nikodemo kwamba Mungu aliupenda ulimwengu sana hivi kwamba yeye aliandaa Mwana wake awe Mwokozi. Hivyo, Yesu sasa anaonyesha kwamba mtu yeyote wa ulimwengu wa wanadamu ambaye anakula mnofu wake kwa njia ya kitamathali, kwa kujizoeza imani katika ile dhabihu ambayo yeye atafanya karibuni, anaweza kupokea uhai wa milele.

Hata hivyo, watu wale wanajikwaa juu ya maneno ya Yesu. “Mtu huyu anawezaje kutupa mnofu wake tule?” wanauliza. Yesu anataka wasikilizaji wake wafahamu kwamba kule kula sehemu ya mnofu wake kungefanywa kwa njia ya kitamathali. Kwa hiyo, ili akazie hilo, yeye anasema jambo fulani la kuchukiza hata zaidi ikiwa linachukuliwa kwa njia halisi.

“Msipoula mnofu wa Mwana wa binadamu na kunywa damu yake,” Yesu anatangaza, “nyinyi hamna uhai ndani yenu wenyewe. Yeye ambaye anajilisha mnofu wangu na kunywa damu yangu ana uhai wa milele, na mimi nitamfufua katika ile siku ya mwisho; kwa maana mnofu wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Yeye ambaye anajilisha mnofu wangu na kunywa damu yangu anabaki katika muungano pamoja na mimi, na mimi katika muungano pamoja naye.”

Ni kweli, fundisho la Yesu lingesikika kuwa lenye kuchukiza kabisa ikiwa yeye alikuwa akidokeza kula nyama ya mwanadamu. Lakini, bila shaka, Yesu haungi mkono kula mnofu au kunywa damu kwa uhalisi. Yeye anakazia tu kwamba wote ambao watapokea uhai wa milele lazima wajizoeze imani katika ile dhabihu ambayo yeye atafanya wakati yeye atoapo mwili wake mkamilifu wa kibinadamu na kumwaga damu ya uhai wake. Lakini, hata wengi wa wanafunzi wake hawafanyi jaribio lolote la kufahamu fundisho lake na kwa hiyo wanapinga hivi: “Usemi huu unachukiza mno; ni nani anayeweza kuusikiliza?”

Akijua kwamba wengi wa wanafunzi wake wananung’unika, Yesu anasema: “Je! hilo linawakwaza? Basi, namna gani ikiwa ingewapasa nyinyi kuona Mwana wa binadamu akipaa kwenda mahali ambako yeye alikuwa kwanza? . . . Semi ambazo mimi nimesema kwenu ni roho na ni uhai. Lakini kuna baadhi yenu ambao hawaamini.”

Yesu anaendelea: “Hii ndiyo sababu mimi nimesema kwenu, Hakuna yeyote ambaye anaweza kuja kwangu isipokuwa jambo hilo limepewa kwake na Baba.” Inapokuwa hivyo, wengi wa wanafunzi wake wanaondoka na hawafuati yeye tena. Kwa hiyo Yesu anageukia mitume wake 12 na kuuliza: “Nyinyi hamtaki kwenda pia, je! mwataka?”

Petro anajibu: “Bwana, sisi tutaenda zetu kwa nani? Wewe una semi za uhai wa milele; nasi tumeamini na tumekuja kujua kwamba wewe ndiwe Yule Mtakatifu wa Mungu.” Ni wonyesho mzuri kama nini wa ushikamanifu, hata ingawa Petro na mitume wale wengine huenda wakawa hawakufahamu kwa ukamili fundisho la Yesu juu ya jambo hilo!

Ingawa jibu la Petro linampendeza, Yesu anaonelea hivi: “Mimi nimechagua nyinyi kumi na wawili, sivyo? Hata hivyo mmoja wenu ni mchongezi.” Yeye anasema juu ya Yuda Iskariote. Inawezekana kufikia hapa Yesu anagundua katika Yuda “mwanzo” fulani, au hatua ya kwanza, ya mwendo mbaya.

Yesu ametamausha watu sasa hivi tu kwa kukinza jaribio lao la kumfanya mfalme, nao huenda wakawa wanasababu hivi, ‘Huyu angewezaje kuwa ndiye Mesiya ikiwa yeye hataki kutwaa cheo ambacho ni haki ya Mesiya?’ Hili, pia, lingekuwa jambo ambalo lingali limo akilini mwa watu hao. Yohana 6:51-71; 3:16, NW.

▪ Yesu anatoa mnofu wake kwa ajili ya nani, nao ‘wanakulaje mnofu wake’?

▪ Ni maneno gani zaidi ya Yesu ambayo yanachukiza watu hao, hata hivyo yeye anakazia jambo gani?

▪ Wakati wengi wanapoacha kufuata Yesu, Petro anajibu nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki