Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 80
  • Mazizi ya Kondoo na Mchungaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mazizi ya Kondoo na Mchungaji
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Yale Mazizi ya Kondoo na Yule Mchungaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Mchungaji Mwema na Mazizi ya Kondoo
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Mchungaji Mwema na “Zizi Hili” Lake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • “Mchungaji Mwema” na Lile “Kundi Dogo”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 80

Sura 80

Mazizi ya Kondoo na Mchungaji

YESU amekuja Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Wakfu, au Hanuka, sikukuu ambayo husherehekea kuwekwa hekalu wakfu upya kwa Yehova. Katika 168 K.W.K., yapata miaka 200 mapema, Antioko wa 4 Epifane aliteka Yerusalemu na kulitia unajisi hekalu na madhabahu yalo. Hata hivyo, miaka mitatu baadaye Yerusalemu lilitekwa upya na hekalu likafanywa wakfu upya. Baada ya hapo, mwadhimisho wa kufanya wakfu upya ulishikwa kila mwaka.

Hii Sikukuu ya Wakfu hutukia katika Kislevu 25, huo ukiwa ni mwezi wa Kiyahudi unaolingana na sehemu ya mwisho ya Novemba na sehemu ya kwanza ya Desemba katika kalenda yetu ya ki-siku-hizi. Hivyo, ni muda unaozidi kidogo tu siku mia moja ambao umebaki kabla ya ile Sikukuu ya Kupitwa iliyo maarufu ya 33 W.K. Kwa sababu hayo ni majira ya hali-hewa iliyo baridi, mtume Yohana anayaita “wakati wa kipupwe.”

Sasa Yesu anatumia kielezi ambamo yeye anataja mazizi matatu ya kondoo na fungu ambalo yeye anatimiza akiwa yule Mchungaji Mwema. Zizi la kwanza la kondoo ambalo ananena habari zalo linatambulishwa kuhusiana na mpango wa agano la Sheria ya Musa. Sheria hiyo ilitumika kuwa kama ua, ukitenganisha Wayahudi na mazoea yenye kufisidi ya wale watu wasiokuwamo katika agano hili la pekee pamoja na Mungu. Yesu anaeleza hivi: “Kweli kweli kabisa mimi nasema kwenu, Yeye ambaye haingii ndani ya zizi la kondoo kupitia mlango lakini anapanda juu mahali penginepo, huyo ni mwizi na mporaji. Bali yeye ambaye huingia kupitia ule mlango ni mchungaji wa kondoo.”

Wengine walikuwa wamekuja na kudai kuwa yule Mesiya, au Kristo, lakini wao hawakuwa yule mchungaji wa kweli ambaye kwa habari zake Yesu anaendelea kusema: “Yule mlinda-mlango anamfungulia huyo, nao wale kondoo husikiliza sauti yake, naye huita kondoo wake mwenyewe kwa jina na kuwaongoza kwenda nje. . . . Mgeni hawatamfuata kwa vyovyote bali watamkimbia, kwa sababu wao hawaijui sauti ya wageni.”

Yule “mlinda-mlango” wa lile zizi la kwanza alikuwa Yohana Mbatizaji. Akiwa mlinda-mlango, Yohana ‘alifungulia’ Yesu kwa kumtambulisha kwa hao kondoo wa ufananisho ambao angeongoza kwenda nje kwenye malisho. Kondoo hawa ambao Yesu aita kwa jina na kuongoza kwenda nje wanaingizwa hatimaye kwenye zizi jingine, kama yeye aelezavyo: “Kweli kweli kabisa mimi nasema kwenu nyinyi, Mimi ndimi mlango wa kondoo,” yaani, ule mlango wa zizi jipya la kondoo. Yesu aanzapo lile agano jipya na wanafunzi wake na kumimina kutoka mbinguni roho takatifu juu yao Pentekoste iliyofuata, wao wanaingizwa katika hili zizi jipya la kondoo.

Akieleza zaidi kwenye fungu analotimiza, Yesu anasema: “Mimi ndimi mlango; yeyote aingiaye kupitia mimi ataokolewa, naye ataingia na kutoka na kupata malisho. . . . Mimi nimekuja ili wawe na uhai na ili wawe nao kwa utele. . . . Mimi ndimi yule mchungaji mwema, nami najua kondoo wangu na kondoo wangu wanijua, kama vile Baba anijuavyo nami najua Baba; nami natoa nafsi yangu kwa ajili ya wale kondoo.”

Hivi majuzi, Yesu alikuwa amefariji wafuasi wake, akisema: “Msiwe na hofu, kundi dogo, kwa sababu Baba yenu ameidhinisha kuwapa nyinyi ule ufalme.” Hili kundi dogo, ambalo hatimaye huwa na hesabu ya 144,000, huingia ndani ya hili zizi la kondoo jipya, au la pili. Lakini Yesu anaendelea kuonelea hivi: “Mimi nina kondoo wengine, ambao si wa zizi hili; hao pia lazima niwalete, nao watasikiliza sauti yangu, nao watakuwa kundi moja, mchungaji mmoja.”

Kwa kuwa hao “kondoo wengine” “si wa zizi hili,” lazima wao wawe ni wa zizi jingine, la tatu. Haya mazizi mawili ya mwisho, au nyugo za kondoo, zaenda mahali tofauti. Lile “kundi dogo” katika zizi moja litatawala pamoja na Kristo mbinguni, na wale “kondoo wengine” katika lile zizi jingine wataishi katika dunia Paradiso. Na bado, wajapokuwa katika mazizi mawili, hao kondoo hawana wivu, wala hawahisi kutenganishwa, kwa maana kama asemavyo Yesu, wao “wanakuwa kundi moja” chini ya “mchungaji mmoja.”

Yule Mchungaji Mwema, Yesu Kristo, atoa uhai wake kwa moyo wa kupenda kwa ajili ya mazizi yote mawili. “Mimi nautoa kwa kujichukulia hatua ya kwanza mimi mwenyewe,” yeye asema. “Mimi nina mamlaka niutoe, na nina mamlaka niupokee tena. Ile amri juu ya hilo niliipokea kutoka kwa Baba yangu.” Yesu anaposema hivyo, mgawanyiko unatokea miongoni mwa Wayahudi.

Walio wengi wa ule umati wanasema: “Yeye ana roho mwovu na ana kichaa. Kwa nini nyinyi mwamsikiliza.” Lakini wengine wanaitikia: “Hizi si semi za mtu mwenye kupagawa na roho mwovu.” Ndipo, kwa wazi wakirejezea nyuma miezi kadhaa alipoponya mwanamume aliyezaliwa akiwa kipofu, wanaongeza hivi: “Roho mwovu hawezi kufumbua macho ya watu walio vipofu, sivyo?” Yohana 10:1-22; 9:1-7; Luka 12:32; Ufunuo 14:1, 3; 21:3, 4; Zaburi 37:29, NW.

▪ Ile Sikukuu ya Wakfu ni nini, nayo inasherehekewa wakati gani?

▪ Ni nini zizi la kwanza la kondoo, na ni nani mlinda-mlango walo?

▪ Mlinda-mlango anafunguliaje yule Mchungaji, na baada ya hapo kondoo hao wanaruhusiwa kuingia katika nini?

▪ Ni nani wanaojumuika kuwa yale mazizi mawili ya Mchungaji Mwema, nao wanakuwa makundi mangapi?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki