Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 11/1 kur. 8-9
  • Yale Mazizi ya Kondoo na Yule Mchungaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yale Mazizi ya Kondoo na Yule Mchungaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Mazizi ya Kondoo na Mchungaji
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Mchungaji Mwema na Mazizi ya Kondoo
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Mchungaji Mwema na “Zizi Hili” Lake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • “Mchungaji Mwema” na Lile “Kundi Dogo”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 11/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Yale Mazizi ya Kondoo na Yule Mchungaji

YESU yumo katika Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Wakfu (ya kutabaruku, UV), au Hanukkah, sikukuu ambayo inaadhimisha kufanywa upya kwa wakfu wa hekalu kwa Yehova. Katika 168 K.W.K., karibu miaka 200 mapema kidogo, Antioko wa Nne Epifane alikuwa ameteka Yerusalemu na kuumbua utakatifu wa hekalu na madhabahu yalo. Hata hivyo, miaka mitatu baadaye Yerusalemu ilitekwa upya na hekalu likafanyiwa wakfu upya. Baada ya hapo, mwadhimisho wa kufanya wakfu upya ulishikwa kila mwaka.

Hii Sikukuu ya Wakfu hutukia katika Chislev 25, huo ukiwa ni mwezi wa Kiyahudi unaolingana na sehemu ya mwisho ya Novemba na sehemu ya kwanza ya Desemba katika kalenda yetu ya ki-siku-hizi. Hivyo, ni muda unaozidi kidogo tu siku mia moja ambao umebakia kabla ya ile sikukuu ya Kupitwa iliyo maarufu ya 33 W.K. Kwa sababu hayo ni majira ya hali-hewa iliyo baridi, mtume Yohana anayaita “wakati wa baridi.”

Sasa Yesu anatumia kielezi ambamo yeye anataja mazizi matatu ya kondoo na fungu ambalo yeye anatimiza akiwa yule Mchungaji Mwema. Zizi la kwanza la kondoo ambalo ananena habari zalo linatambulishwa kuhusiana na mpango wa agano la Sheria ya Musa. Sheria hiyo ilitumika kuwa kama ua uliotenganisha Wayahudi kutoka kwenye mazoea yenye kufisidi ya watu wale wasiokuwa katika agano hili la pekee pamoja na Mungu. Yesu anaeleza hivi: “Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.”

Wengine walikuwa wamekuja na kudai kuwa ndio Mesiya, au Kristo, lakini hawakuwa yule mchungaji wa kweli ambaye Yesu anaendelea kunena habari zake: “Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo kwa majina yao, na kuwapeleka nje. Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia . . . Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.”

“Bawabu” wa zizi la kwanza la kondoo alikuwa Yohana Mbatizaji. Akiwa ndiye bawabu [mtunza-mlango], Yohana ‘alimfungulia’ Yesu kwa kumtambulisha yeye kwa kondoo hao wa ufananisho ambao angewaongoza nje kwenye malisho. Kondoo hao ambao Yesu anawaita kwa majina na kuwaongoza nje wanaruhusiwa mwishowe kuingia kwenye zizi jingine la kondoo, kama vile yeye anavyoeleza: “Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo,” yaani, mlango wa zizi jipya la kondoo. Wakati Yesu anapoanzisha lile agano jipya pamoja na wanafunzi wake na akiwa mbinguni anamimina roho takatifu juu yao wakati wa Pentekoste inayofuata, wao wanaruhusiwa kuingia kwenye hilo zizi jipya la kondoo.

Akieleza zaidi juu ya fungu ambalo yeye anatimiza, Yesu anasema: “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. . . . Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. . . . Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.”

Hapo juzijuzi, Yesu alikuwa amefariji wafuasi wake, akisema: “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.” Hilo kundi dogo, ambalo mwishowe hesabu yalo inakuwa 144,000, linakuja ndani ya zizi hilo la kondoo lililo jipya, au lililo la pili. Lakini Yesu anaendelea kuonelea hivi: “Kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; nao hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.”

Kwa kuwa wale “kondoo wengine” si “wa zizi hili,” lazima wawe ni wa zizi jingine, la tatu. Mazizi hayo mawili ya mwisho, au viboma vya kondoo, yana mahali tofauti-tofauti pa kwenda. Lile “kundi dogo” lililo katika zizi moja litatawala pamoja na Kristo mbinguni, na wale “kondoo wengine” walio katika zizi lile jingine wataishi juu ya dunia iliyo Paradiso. Hata hivyo, wajapokuwa katika mazizi mawili, kondoo hao hawana wivu, wala hawahisi wakiwa wametenganishwa kiubaguzi, kwa maana, kama vile Yesu anavyosema, wao ‘wanakuwa kundi moja’ chini ya “mchungaji mmoja.”

Yule Mchungaji Mwema, Yesu Kristo, anatoa uhai wake kwa nia kwa ajili ya mazizi yote mawili ya kondoo. “Mimi nautoa mwenyewe,” yeye anasema. “Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.” Wakati Yesu anaposema hivyo, mgawanyiko unatokea miongoni mwa Wayahudi.

Wengi kati ya umati wanasema: “Ana pepo huyu, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza?” Lakini wengine wanajibu hivi: “Maneno hayo siyo ya mtu mwenye pepo.” Halafu, kwa uwazi wakirejeza nyuma miezi kadhaa kwenye wakati ambapo yeye aliponya mwanamume yule aliyezaliwa kipofu, wao wanaongezea hivi: “Je! pepo aweza kuwafumbua macho vipofu?” Yohana 10:1-22; 9:1-7; Luka 12:32; Ufunuo 14:1, 3; 21:3, 4; Zaburi 37:29.

◆ Ni nini ile Sikukuu ya Wakfu, na inasherehekewa wakati gani?

◆ Ni nini zizi la kwanza la kondoo, na ni nani bawabu walo?

◆ Ni jinsi gani bawabu anavyofungulia yule Mchungaji, na baada ya hapo kondoo hao wanaruhusiwa kuingia kwenye nini?

◆ Ni nani walio mazizi yale mawili ya Mchungaji Mwema, nao wanakuwa makundi mangapi?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki