Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gf somo la 13 uku. 21
  • Uganga Na Uchawi Ni Mambo Mabaya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uganga Na Uchawi Ni Mambo Mabaya
  • Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
  • Habari Zinazolingana
  • Ukweli Kuhusu Uchawi na Ulozi
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
  • Je! Kuna Hatari Katika Kufanya Mizungu?
    Amkeni!—1993
  • Unachopaswa Kujua Kuhusu Uchawi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Uchawi Waenea Pote—Je! Ni Hatari?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
Pata Habari Zaidi
Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
gf somo la 13 uku. 21

SOMO LA 13

Uganga Na Uchawi Ni Mambo Mabaya

Shetani anataka wewe ufanye mambo ya kiganga. Watu wengi hutoa dhabihu kwa babu zao wa kale waliokufa au kwa roho ili ziwalinde wasipate madhara. Wao hufanya hivyo kwa sababu wanaogopa nguvu za ulimwengu wa roho. Watu hao huvaa pete au bangili za kiganga. Wao hunywa au kusugua mwilini mwao “dawa” zinazodhaniwa kuwa zina nguvu za kiganga. Watu fulani huficha katika nyumba zao au chini ya ardhi vyombo vinavyoaminiwa kuwa na nguvu za kulinda. Wengine nao hutumia “dawa” za kiganga kwa sababu wanaamini kuwa zitawaletea mafanikio katika biashara, mitihani shuleni, au uchumba.

Ukitaka ulinzi bora zaidi dhidi ya Shetani, wapaswa kuwa rafiki ya Yehova. Yehova Mungu na malaika zake wana nguvu nyingi zaidi kuliko Shetani na roho wake waovu. (Yakobo 2:19; Ufunuo 12:9) Yehova ana hamu ya kutumia nguvu zake kuwasaidia rafiki zake—wale wenye uaminifu-mshikamanifu kabisa kwake.—2 Mambo ya Nyakati 16:9.

Neno la Mungu linasema hivi: “Msifanye kuloga.” Yehova hushutumu uganga na uchawi kwa sababu mazoea hayo yanaweza kumfanya mtu atawaliwe moja kwa moja na Shetani Ibilisi.—Mambo ya Walawi 19:26.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki