Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gf somo la 14 kur. 22-23
  • Rafiki za Mungu Huepuka Mabaya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Rafiki za Mungu Huepuka Mabaya
  • Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
  • Habari Zinazolingana
  • Mazoea Ambayo Mungu Huchukia
    Mungu Anataka Tufanye Nini?
  • Tunapaswa Kufanya Nini ili Kumpendeza Mungu?
    Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Sehemu ya 13
    Msikilize Mungu
  • Je! Mungu Ataharibu Wabaya Tena?
    Furahia Milele Maisha Duniani!
Pata Habari Zaidi
Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
gf somo la 14 kur. 22-23

SOMO LA 14

Rafiki za Mungu Huepuka Mabaya

Shetani huwashawishi watu wafanye mambo mabaya. Mtu anayetaka kuwa rafiki ya Mungu lazima achukie mambo ambayo Yehova huchukia. (Zaburi 97:10) Hapa pana mambo kadhaa ambayo rafiki za Mungu huyaepuka:

Dhambi zinazohusu ngono. “Usizini.” (Kutoka 20:14) Ni kosa pia kufanya ngono kabla ya ndoa.—1 Wakorintho 6:18.

Ulevi. “Walevi . . . hawatarithi ufalme wa Mungu.”—1 Wakorintho 6:10.

Uuaji, Utoaji-Mimba. “Usiue.”—Kutoka 20:13.

Wizi. “Usiibe.”—Kutoka 20:15.

Kusema Uwongo. Yehova huchukia “ulimi wa uongo.”—Mithali 6:17.

Jeuri na Hasira Isiyodhibitiwa. Yehova humchukia “mwenye kupenda udhalimu [“jeuri,” NW].” (Zaburi 11:5) “Kazi za mwili [hutia ndani] . . . hasira za ghafula.”—Wagalatia 5:19, 20.

Kucheza Kamari. “Mkome kuchangamana katika ushirika pamoja na yeyote . . . ambaye ni . . . mtu mwenye pupa.”—1 Wakorintho 5:11.

Chuki za Kijamii na za Kikabila. “Endeleeni kupenda maadui wenu na kusali kwa ajili ya wale wanaowanyanyasa nyinyi.”—Mathayo 5:43, 44.

Mambo ambayo Mungu anatuambia hutunufaisha. Si rahisi sikuzote kuepuka kufanya mambo mabaya. Yehova na Mashahidi wake wanaweza kukusaidia kuepuka kufanya mambo yanayomchukiza Mungu.—Isaya 48:17; Wafilipi 4:13; Waebrania 10:24, 25.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki