SEHEMU YA 6
Wazazi Wako
Wazazi wamejionea mengi maishani. Wakati mmoja walikuwa vijana kama wewe. Kwa sababu hiyo, ingetazamiwa kwamba wao hasa ndio wanaoweza kukupa wewe mwongozo unaohitaji. Hata hivyo, nyakati nyingine huenda ukahisi kwamba baadhi ya matatizo yako yanatokana na wazazi wako. Kwa mfano, huenda ukakabili moja kati ya hali zinazofuata:
□ Wazazi wangu wananilaumu daima.
□ Baba au mama hupenda kulewa au hutumia dawa za kulevya.
□ Wazazi wangu hubishana sikuzote.
□ Wazazi wangu wametengana.
Sura ya 21-25 zitakusaidia kushughulika na matatizo haya na mengine.
[Picha katika ukurasa wa 172, 173]