Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yp1 uku. 48
  • Mfano wa Kuigwa—Yakobo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mfano wa Kuigwa—Yakobo
  • Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
  • Habari Zinazolingana
  • Yakobo na Esau Wafanya Amani
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Je! Unautazamia Urithi kwa Bidii?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Mapacha Waliokuwa Tofauti
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Yakobo Alipewa Urithi
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
Pata Habari Zaidi
Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
yp1 uku. 48

Mfano wa Kuigwa​—Yakobo

Yakobo na ndugu yake, Esau, hawajasemezana kwa miaka mingi. Isitoshe, Esau anamchukia Yakobo. Ijapokuwa Yakobo hajafanya kosa lolote, ndiye anayechukua hatua ya kuziba pengo lililopo kati yao. Anasalimu amri. Lengo lake si kushinda mabishano bali kurudisha hali nzuri kati yake na ndugu yake. Yakobo halegezi msimamo wake, hata hivyo, hasisitizi Esau amwombe msamaha kabla ya kufanya amani naye.—Mwanzo 25:27-34; 27:30-41; 32:3-22; 33:1-9.

Ugomvi unapotokea katika familia yenu, wewe hufanya nini? Huenda nyakati nyingine ukahisi kwamba huna kosa hata kidogo na kwamba bila shaka, ndugu au dada yako au hata mzazi wako ndiye mwenye kosa. Katika hali kama hizo, unaketi kitako na kungoja mpaka wao wachukue hatua? Au unaweza kufuata mfano wa Yakobo? Ikiwa hakuna kanuni ya Biblia inayovunjwa, uko tayari kusalimu amri ili kuwe na amani? (1 Petro 3:8, 9) Yakobo hakuruhusu kiburi kigawanye familia yao. Alijinyenyekeza mbele ya ndugu yake nao wakafanya amani. Je, wewe, utafanya hivyo pia?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki