Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jy sura 23 uku. 60-uku. 61 fu. 5
  • Yesu Afanya Miujiza Huko Kapernaumu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Afanya Miujiza Huko Kapernaumu
  • Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Habari Zinazolingana
  • Miujiza Zaidi Katika Kapernaumu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Miujiza Mingi Zaidi Katika Kapernaumu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Miujiza Ambayo Yesu Alifanya Katika Mji Alimokaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Sinagogi—Mahali Ambapo Yesu na Wanafunzi Wake Walihubiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
jy sura 23 uku. 60-uku. 61 fu. 5
Wagonjwa wanakusanyika kwenye nyumba ya Petro, naye Yesu anawaponya

SURA YA 23

Yesu Afanya Miujiza Huko Kapernaumu

MATHAYO 8:14-17 MARKO 1:21-34 LUKA 4:31-41

  • YESU AMFUKUZA ROHO MWOVU

  • MAMA MKWE WA PETRO APONYWA

Yesu amewaalika wanafunzi wanne—Petro, Andrea, Yakobo, na Yohana—wawe wavuvi wa watu. Ni siku ya Sabato na wote wanaenda kwenye sinagogi fulani huko Kapernaumu. Yesu anafundisha katika sinagogi, na kwa mara nyingine tena watu wanashangazwa na njia yake ya kufundisha. Anafundisha kama mtu mwenye mamlaka na si kama waandishi wao.

Siku hii ya Sabato mtu fulani aliye na roho mwovu amehudhuria. Papo hapo katika sinagogi, mtu huyo anapaza sauti na kusema: “Kwa nini unatusumbua, wewe Yesu Mnazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninajua wewe ni nani, Mtakatifu wa Mungu!” Yesu anamkemea roho mwovu anayemwongoza mtu huyo kwa kusema: “Nyamaza, na umtoke!”—Marko 1:24, 25.

Papo hapo, yule roho mwovu anamwangusha mtu huyo chini na kumfanya agaegae na kupiga kelele kwa sauti kubwa. Lakini yule roho mwovu anamtoka mtu huyo “bila kumuumiza.” (Luka 4:35) Watu waliomzunguka katika sinagogi wanashangaa sana! “Ni jambo gani hili?” wanaulizana. “Hata anawaamuru roho waovu kwa mamlaka, nao wanamtii!” (Marko 1:27) Inaeleweka kwamba habari kuhusu tukio hilo la kushangaza zinaenea katika Galilaya yote.

Baada ya kutoka katika sinagogi, Yesu na wanafunzi wake wanaenda nyumbani kwa Simoni, yaani, Petro. Mama mkwe wa Petro ni mgonjwa sana, anaugua homa kali. Wanamwomba Yesu amsaidie. Basi Yesu anamkaribia, anamshika mkono, na kumwinua. Mara moja anaponywa na kuanza kumhudumia Yesu na wanafunzi walio pamoja naye, labda anawaandalia chakula.

Inapokaribia jioni, watu kutoka kila mahali wanakuja nyumbani kwa Petro wakiwa na wagonjwa. Baada ya muda mfupi ni kana kwamba jiji lote limekusanyika mlangoni. Kwa nini? Wanataka kuponywa. Kwa kweli, ‘wote waliokuwa na watu wenye magonjwa mbalimbali wanawaleta kwake. Anawaponya kwa kuweka mikono yake juu ya kila mgonjwa.’ (Luka 4:40) Naam, hata wawe na ugonjwa gani, Yesu anawasaidia, kama ilivyotabiriwa. (Isaya 53:4) Hata anawaweka huru wale walio na roho waovu. Roho waovu wanapotoka, wanapaza sauti: “Wewe ndiye Mwana wa Mungu.” (Luka 4:41) Lakini Yesu anawakemea na hawaruhusu wazungumze tena. Wanajua kwamba Yesu ndiye Kristo, naye hataki waonekane kana kwamba wanamtumikia Mungu wa kweli.

KUINGIWA NA ROHO WAOVU

Roho mwovu au roho waovu walipomwingia mtu, walisababisha mateso mengi. (Mathayo 17:14-18) Lakini mtu huyo alipowekwa huru kutokana na roho waovu, alirudi katika hali ya kawaida kimwili na kiakili. Yesu alionyesha tena na tena nguvu zake za kuwafukuza roho waovu kwa kutumia roho takatifu ya Mungu.—Luka 8:39; 11:20.

  • Ni nini kinachotokea katika sinagogi huko Kapernaumu siku ya Sabato?

  • Yesu anapotoka katika sinagogi anaenda wapi, na anafanya nini huko?

  • Watu katika jiji wanatendaje baada ya kuona jambo ambalo Yesu amefanya?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki